TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,436
- 3,558
Maisha Yana siri na siri hiyo ndio maisha yenyewe.
Kuna watu wamekazana kusema binadamu wote ni sawa, sijui wanajifariji na umasikini wao ama vipi? Labda kama wanamaanisha ni sawa katika maumbile ya kibinadamu, lakini si katika uwezo wa kuyamiliki maisha.
Kuna watu wanakula maisha na kuna wale tunao liwa na maisha.
Mimi natembelea Raum, lakini kuna dogo anamiliki Cadillac ya mwaka 2024 na magari mengine ya bei mbaya.
Kuna watu hulipia watoto wao ada shule ya msingi 21M-60M+ kwa mwaka, halafu kuna wale watoto wetu wanasoma shule ya msingi Nachingwea, wakiwa na kidumu cha maji na mfagio mkononi.
Mimi nimepanga kwa Mzee Komba, nyumba rangi inabanduka ukigusa ukuta umechafuka, lakini kuna watu wanaishi kwenye nyumba ambazo kuta zimepigwa mawe ya Tanga kama siyo tiles za kisasa. Binadamu wote ni sawa au siooo? Wacha tujifariji.
Kuna watu wanamiliki minjengo ya mabilioni kwa pesa zao wenyewe, halafu kuna bwana mwalimu Selemani amejenga kakibanda kake ka 40M kwa mkopo kutoka NMB na ana vimba noma.
Nina kafeni ka Aliyons kananengua kiuno usiku kucha na bado ninasweat ile mbaya, halafu kuna wale wanaoishi kwenye nyumba zenye kiyoyozi full-time na wanajifunika mablanketi ya kutengeneza joto kwa umeme.
Kuna wana zizi la ng’ombe limewekwa kiyoyozi na ceiling fan, chini pamepigwa tiles maalum na kuna wafanyakazi wakusafisha banda kuondoa kinyesi kila ng’ombe anapojisaidia ili asichafuke. Sasa nadhani yatosha kusema kati ya anayeishi kwenye kageto ka 25k na makolokolo yote humo na huyo ng’ombe, ng’ombe amejulikana.
Kuna watu wameajiriwa, wanasubiri wastaafu wapewe kiinua mgongo ambacho ni 40M-1B, na kuna watu huingiza hiyo pesa kwa siku, wiki, au mwezi.
Maisha hayajawahi kuwa sawa, na binadamu hawajawahi kuwa sawa except katika uumbaji tu.
Unakutana na demu kapiga makeup ya bundi 5 na joto la Dar hata unyunyu wa 25k umemshinda; anakujiremba kote lakini anatema kikwapa ile mbaya. Halafu kuna demu akikatiza kwako hana makeup ila anavutia, ananukia vizuri. (Kuna wanaoweka unyunyu lakini bado wanatema.)
Kuna watu wakienda hospitali kutibiwa, bili ikitoka 100k wanalalama kama king’ora cha ambulance iliyobeba mgonjwa mahututi. Halafu kuna wale matibabu yao bili ni 10M na analipa cash bila zengwe; yaani wanaranda na begi la minoti hospitalini, ilhali wale wa kwa Mtogole pesa ipo kwenye akaunti ya Tigo Pesa.
Binadamu hatujawahi kuwa sawa na haitatokea tukawa sawa. Huu usemi ni manipulation za kuwafariji masikini tu. Mtu anatumia simu ya 8-20M na anazo kama tano, halafu kuna Ashura pale kwa Tegeta kwa Ndevu anachombo cha mawasiliano Infinix Hot 10 kaivalisha cover la kamdoli kapusi na ananata noma. (Anyway mtu chake bwana.)
Kuna watu wanakufa na kuna watu wanafariki. Kuna watu wanazikwa na kuna watu wanafukiwa. (Elewa hii dhana.) Kuna watu wanafariki si kwa kukosa matibabu, bali kwa sababu tatizo lake madaktari waligonga mwamba katika kila kona za dunia. Halafu kuna watu wanakufa kwa malaria au septicemia ambayo matibabu yake ni 20k tu.
Yamkini binadamu hatujawahi kuwa sawa, na haiji kutokea. Kila mmoja apambane amiliki pesa kwa namna yoyote ile. Kikubwa uwe nazo lakini usimwage damu. Pambana.
Kuna watu wakiumwa watoto wao wanawapeleka hospitali za bei mbaya si kwa sababu wameshindwa kuzimudu gharama. Lahasha, wanajisikia fahari kuwahudumia maana pesa ipo kwa kila mtu wa damu yao. Halafu kuna sisi, wazazi wetu wanatutegemea kwa kila kitu na hatumudu.
Tujitahidi kutengeneza mfumo wa kuingiza pesa kwa vizazi vyote. Mfumo usio kufa ili tuache kujifariji kishamba. Binadamu hatujawahi kuwa sawa na haiji kuwa hivyo.