Aloo, sisi wengine tutaambiwa twamwandama mno JK, lakini ukweli usemwe. Mkuu wetu huyu kwa kweli sijui nisemeje: hana common sense....vile...?
Nimetazama ule mkutano wa Davos na aliekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown. Mpaka ilipofikia yule Heikal kulalamika juu ya bandwidth. Odinga akasema Kenya imerahisisha maambo katika uwekezaji katika reli ya kutoka Msa kwenda Uganda, lakini hajui matatizo ya bandwidth. Ilipofika zamu ya JK kujibu akawa anatoa maneno kama mhuni wa Kariakoo vile, mbele ya mahafali ya dunia!
'Wee Heykal, sisi twataka watu wa kuchangia mpango wa reli kutoka TZ, Rwanda na Burundi, wewe unataka kujenga reli ambayo tayari ipo....Kenya hadi Uganda. Si uje unione badala ya kupiga kelele oh bandwidth nk?'
Nilihuzunika sana.
-Kuna umuhimu gani wa mwekezaji hadi amwone rais wa nchi? Kwani hakuna taaasisi zinazoshughulikia mambo hayo? Moja kwa moja ika click kuwa haya ni yale mambo ya 10% na suti!
Rais anawezaje kutaka kukutana na mfanyibiashara na kutoa wito huo mbele ya mahafali ya Kimataifa?
Infact, JK yaelekea hakuelewa hata kikao kile kilikuwa cha kuzungumzia nini! Bworn aliweka wazi tangu mwanzo kwamba kilichokuwa chatakikana ni fikra gani mpya za kuichukua Afrika kutoka hapa ilipo kuelekea mustakbali.