Utawala wa CCM na Uchakachuaji wa Demokrasia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utawala wa CCM na Uchakachuaji wa Demokrasia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 7, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tanzania Daima
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeweza kutawala taifa letu kwa muda huu mrefu na chaweza kuendelea kutawala kwa muda mrefu baadaye kwa kile ambacho nakitambulisha kwenu kuwa ni uchakachuaji wa demokrasia. Ndugu zangu, ninapozungumzia uchakachuaji wa demokrasia ninazungumzia mjumuisho wa taratibu, mikakati, mbinu, sheria, mipango na mfumo mzima ambapo kanuni za demokrasia zimechanganywa na kuharibiwa na kanuni za utawala wa kibabe, kimabavu au wa kiimla (kidikteta).
  Demokrasia imechakachuliwa pale ambapo vitu ambavyo ni kinyume na demokrasia vimeingizwa ndani yake na kupitishwa kwa furaha kuwa ni demokrasia alimradi nchi inakwenda.
  Wazo hili la kuchakachuliwa kwa demokrasia ni rahisi kuelewa kama utachukua muda kuelewa mojawapo ya mambo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kwa muda mefu kuhusu suala la mafuta ya magari kuchanganywa na mafuta ya taa au vitu vingine ili kuweza kuyapa wingi usiostahili ilikuweza kusababisha faida zaidi kwa wamiliki wa vituo vya mafuta.
  Demokrasia nayo imechakachuliwa ili hatimaye kuongeza faida za haraka haraka kwa chama tawala. Mambo haya yamefanywa kwa makusudi na mtu yeyote anaweza kuyaona kwa urahisi endapo ayatasogelea akiwa na fikra huru na zilizo wazi.
  Nitatoa mifano michache ili muweze kuona kuwa Tanzania hatuna demokrasia halisi bali tunayo ile iliyoingizwa kanuni za utawala wa kidikteta au wa kibabe.
  Kwa muda mrefu tumekuwa tukililia uwepo wa tume huru ya uchaguzi. Na kwa muda mrefu serikali ya CCM imekataa kuweka utaratibu wa kuunda tume huru ya uchaguzi hasa kwa upande wa bara.
  Matokeo yake ni kuwa tume ipo ya uchaguzi lakini haina uhuru ule tunaouhitaji kwenye demokrasia yaani kuanzia kuundwa kwake, ufanyaji kazi wake, bajeti yake n.k
  Au tuangalie uundwaji wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Ukiangalia kwa haraka haraka unaweza kudhania kuwa ni ofisi huru lakini nayo ukiiangalia kwa karibu utaona kuwa nayo imechakachuliwa kwa kuingizwa vitu ambavyo ni kinyume na demokrasia. Kwa mfano, Mbunge wa CCM (chama tawala) ambaye ni waziri anayeshughulikia masuala ya kisiasa ana kauli katika masuala ya usajili wa vyama na utendaji wa sheria za gharama ya uchaguzi yeye akiwa ni mtu ambaye anaweza kuamua kiasi gani kitumike kwenye jimbo gani!
  Au nitoe mfano mwingine ambao nina uhakika watu wengi hawaufahamu. Sheria ya Madaraka ya Rais wakati wa Dharura yanampa nguvu rais kuzuia gazeti au chombo chochote cha habari kuandika au kufanya kazi zake kwa sababu ya “hali ya hatari” ambayo yeye ndiye mtu pekee anayeweza kuitangaza.
  Kwa mujibu wa sheria hiyo rais ana uwezo wa kidikteta siyo katika kuzuia tu hata kutaifisha mara moja vyombo hivyo.
  Mfano mzuri wa jambo hili lilitokea Kenya ambapo wakati wa machafuko yaliyofuatia uchaguzi mkuu, Rais wa Kenya akitumia sheria kama ya kwetu aliweza kuzuia vyombo vya habari kutangaza kilichokuwa kinatokea wakati ule.
  Sasa, mtu ambaye hana uwezo mzuri wa kufikiri japo anaweza kuwa ameenda shule na kuhitimua atasema kuwa “hilo ni jambo zuri kwa sababu hatutaki vyombo vya habari vichochee watu kwa kutangaza yanayoendelea nchini wakati wa hali ya hatari”.
  Kwa maneno mengine, sheria yetu inataka wananchi waweke imani yao kwa asilimia mia moja kwenye mikono ya rais kuwa hatofanya jambo lolote baya na kuwa wananchi wasitake kujua serikali yao inafanya nini wakati kama huo.
  Kidemokrasia hii ni sheria mbaya na ni kweli ni “ya hatari wakati wa hali ya hatari”. Ni mbaya kwa sababu demokrasia inataka wananchi wajue kile ambacho serikali yao inafanya wakati wote. Na hakuna wakati muhimu kwa wananchi kujua kile kinachofanywa kwa jina lao kama wakati wa hatari. Wakati wowote ule watawala wanaweza kufanya mambo kwa siri kwa kisingizio kuwa ni “kwa ajili ya usalama wa taifa” au kwa sababu ya “hali ya hatari” basi watawala wanakuwa hatimaye wamejipatia leseni ya kufanya lolote walipendalo kwani hakuna chombo kinachoweza kuandika habari hizo.
  Wakati watawala wanaruhusiwa kufanya mambo wayatakayo wakiwa wanakingwa na tangazo la hali ya hatari historia imekuja kugundua mauaji yaliyofanywa na tawala mbalimbali katika majaribio ya kuzima ukimya.
  Mfano mzuri ni tawala za Serbia wakati wa kuvunjika iliyokuwa Yugoslavia. Lakini ukweli ni kuwa demokrasia inahitaji vyombo huru zaidi vya habari wakati wa hali ya hatari kuliko wakati mwingine wowote.
  Kwa sababu endapo katika wakati wa hatari hatuwezi kujua watawala wetu wanafanya nini itakuwaje wakati ambapo si wa hatari?
  Demokrasia imechakachuliwa vile vile katika mojawapo ya mambo ya ajabu kabisa kuwahi kutokea nchini. Wakati CCM inaamini kabisa kuwa ipo haki ya msingi kwa mtu kuchagua na kuchaguliwa wameona kuwa mtu asiye mwanachama wa chama cha siasa anaweza kupiga kura kumchagua mtu mwingine lakini hawezi kufanya hivyo kwa yeye mwenyewe kuchaguliwa bila kuwa na chama cha siasa.
  Yaani, wanaamini mtu asiye na chama ana akili na utimamu wa kuweza kuchagua na uchaguzi wake kuheshimiwa lakini linapokuja suala la yeye mwenyewe kuchaguliwa au kugombea tunaambiwa kuwa Watanzania hawana akili nzuri ya kuweza kutambua nani anawafaa au kujua mgombea mzuri hata asiye na chama! Huku ni kuchakachukuliwa kwa demokrasia.
  Naweza kutolea mifano ya Bunge, Mahakama, Polisi, Usalama wa Taifa n.k katika kila sehemu nikaonesha pasipo jitihada kubwa ni jinsi gani kanuni za demokrasia zimechakachuliwa na kutufanya tuchanganyikiwe kama ndio demokrasia yenyewe au mfanano wake tu.
  Fikiria wakati tunaaminishwa kuwa mahakama yetu iko huru ukweli ni kuwa ni huru kwa kadiri ya kwamba rais ameona ni huru, uteuzi wa majaji wake haufanyiwi usaili na wawakilishi wa wananchi na sote tunatakiwa tuamini tu kuwa rais anatuchaguliwa majaji wazuri!
  Demokrasia imechakachuliwa nchini kiasi kwamba kama tungekuwa na uthubutu na ukali kama wa Wanyarwanda tungewarudishia demokrasia “yao” kwani haitufai.
  Kama vile mafuta yanavyochakachuliwa na kusababisha matatizo kwenye magari (hata ya Ikulu!) ndivyo hivyo hivyo demokrasia inapochakachuliwa husababisha matatizo kwa watawala, naam hata Ikulu!
  Wito wangu ni kuwa kama taifa tuna uamuzi wa kuamua kufanya kazi kwa kutumia demokrasia iliyochakachuliwa au kuanza kuisafisha na kukataa ili hatimaye tuwe na demokrasia ya kweli isiyo na nyongeza ya kanuni haramu za utawala wa kifisadi, kidikteta au kibabe.
  Kwa vile tunafikiri (kwa ujumla wetu) kuwa demokrasia iliyochakachuliwa itafutikisha tunavyokwenda kama tunavyoamini kuwa mafuta yaliyochakachuliwa yanaweza kutufaa siku moja tutajikuta tunalipa gharama kubwa kwa sababu demokrasia hata siku moja haifanyi kazi inapochakachuliwa na inaweza kwenda tu kwa kiasi fulani lakini itafika mahali itakwama.
  Siku itakapokwama ndipo tutajua kwanini mafuta yaliyochakachuliwa hayafai kwenye mashine kama vile demokrasia ilivyochakachuliwa haifai kwenye utawala. Hapo ndipo tutajua kuwa CCM inastahili lawama zote kama vile wamiliki wa vituo vinavyohusika na kuchakachua maisha.
  Lakini yawezekana kama vile wachakachuaji mafuta hawapati adhabu kali ndivyo hivyo hivyo CCM hawaadhibiwi kwa sababu hatuoni hatari ya demokrasia isiyo demokrasia. Lakini tukitaka twaweza kuwaadhibu kama vile tunavyofanya haraka na hasira kuwaadhibu wenye vituo vya mafuta yaliyochakachuliwa.
  La kwanza hata hivyo ni kuamini kuwa ninachosema ni kweli.
   
 2. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  MKJJ umeeleza vyema lakini sioni kama kuna wakati tutajitoa kwenye mtego huu.

  CCM wakifanikiwa kurekebisha hayo uliyoyasema ndiyo utakuwa mwanzo wa kujimaliza wenyewe. na wao wanajua fika sidhani kama watadhubutu kufanya hayo makosa.Nafikiri Umma ndiyo unapaswa kujua hilo na kutoa maamuzi yaliyosahihi katika kuchagua serikali.

  lakini pia tukumbuke kuwa kila atayeingia madarakani, hatapenda yeye au marafiki zake waachie madaraka kirahisi. hii ipo hata kwenye taasisi ndogo ndogo hizi, watu wanajijengea base. let's think and act
   
 3. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi nzuri mwanakijiji, umejenga hoja ikajengeka, kuna mambo mengi sana tumeyachakachua, angalia hata utamaduni wa mtanzania umechakachuliwa (kama nitatumia neno hili kwa muktadha huu)
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  na hili ndilo tatizo kubwa kwa muda mrefu tumeendelea kukumbatia na kufanya kazi katika hii demokrasia iliyochakachuliwa kiasi kwamba tumejiaminisha kuwa 'it works'. Ukweli ni kuwa demokrasia yetu bado haijajaribiwa. Haijatikiswa bado.
   
 5. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji; nimeyapenda mawazo yako, ila ndugu yangu wewe unapiga kelele ukiwa nje ya nchi, pale Tarime tumekuwa tukionesha kamwanga lakini wakuwapi ndugu zetu watuunge Mkono? wewe mwenyewe ndiyo umeamua kufia ughaibuni, sawa sisi kwa haka kaimani ketu siku moja tutatoa mwanga.

  Mzee Mwanakijiji; Lengo litatimia kama tutakuwa ving'ang'anizi, watu wa kuiuliza serikali yetu face to face, siyo ukiwa mbali kaka, usisahau tena umri wako unasonga kila kukicha mkuu.

  Mzee Mwanakijiji; ningependa kukuuliza swali dogo tu, hebu wewe utakumbukwa kwa kitu gani? Inawezekana ni kwa haya machapisho yako? Kwa mtizamo unaonekana kama mpiganaji ila uko mbali Mkuu, na kama ujuavyo fimbo ya mbali haiuwi nyoka.

  Mzee Mwanakijiji; iko haja ya kurudi home uje ili tuwe nyuma yako, kwa gharama yoyote.

  Mzee Mwanakijiji; hapo tunaweza kuzuia uchakachuaji huu unaoendelea hapa nyumbani
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  MKJJ, njoo huku battle field tupambane nao!!!

  Hivi wakuu wote wa JF kwa nini tusiunde jeshi letu la kujitolea, tutengeneze bajeti ya miaka minne (tuchange hela, tufanye harambee etc kuraise fedha za kutuwezesha), twende vijijini kuwaelimisha watu wetu misingi ya demokrasia; tuwaeleshe haki zao kama raia wa TZ, waelewe thamani ya kura yao, waelewe haki zao za kimsingi ambazo zinapaswa kutekelezwa na serikali. Waelelwe umaana wa kubadili vyama vya siasa. Wakiiva ndipo turejee na kudai CCJ yetu, Chadema yetu na CUF yetu vipambane kwa uwazi 2015.

  Maana kila nikiangalia hakuna njia nyingne yoyote ya kuwa ng'oa CCM!!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ukweli hauitaji umbali na si wote tunataka uongozi wa namna hiyo. Wengine wito wetu ni kuwa panda ya ukweli, sauti ya kinabii katika jamii; hatutaki kuwa wafalme! Moto wetu wa mabadiliko ni mkali mno kiasi kwamba ukichanganya na madaraka tunaweza kuwa watu wa hatari sana! Ndio maana mahali fulani iliandikwa kuwa yule tajiri alipomwambia baba Ibrahimu kuwa amtume Lazaro kwenda kuwaambia watu machungu ya motoni, Ibrahim alimjibu kwa kumwambia kuwa "wanao Musa na Manabii wawasikilize hao kwani hata akija mtu kutoka huku hawatamsikiliza".

  Ndugu yangu, mnao kina Slaa na Zitto na wengine wengi tu muwasikilize hao! Lakini endapo wito wangu utabadilika you betcha utaniona tu...
   
Loading...