Utawala huu utaanguka kwasababu ya kodi ya kizalendo

Mtoto wa Nyerere

Senior Member
May 21, 2021
129
688
Naliona anguko kubwa la utawala huu.

Wamejitenganisha na uzalendo wa Rais Magufuli aliokuwa nao kwa nchi wameanza kuchezea nchi.

Pamoja na kwamba Magufuli alikuwa na ukorofi wa kutopenda kukosolewa ila asingeweza kuruhusu ujinga huu.

1: Tozo kwenye simu (double taxation)

2: Tozo kwenye kila line ya simu inaanza wiki ijayo yaani kila ukiweka salio hata kabla ujajiunga na kifurushi utakatwa salio lako hii maana yake ukiweka elfu 1 huwezi kujiunga kifurushi cha elfu moja.

3: Hamjatosheka mkaja tena kwenye Simu Banking, Mfano Mimi halotel nilikuwa naingia bure menu ya NMB *150*66# ila kuanzia wiki ijayo ukiingia utakatwa shilling 100.

Jamani tukimbilie wapi? Watanzania tumemkosea nini Mungu.

Bahati mbaya polisi wamekubari kutunika Ku push hii kodi ya wizi na unyang'anyi kwa kuacha Siasa za Mbowe zitrend wakati wanajua kabisa wanawamiza watu mara mbili.

Mama yangu amenipigia simu jana kijijini analia wamemtumia pesa imeshindwa kutoka kwenye simu kama alivyotaka nikamueleza juu ya kupanda kwa kodi!

Kaongea maneno yenye uchungu sana bahati mbaya vijiji hakuna bank angetumia Mimi nikampoza na kumtumia pesa ziada.

Jamani serikali tunatiana umasikini maisha yamekuwa magumu unaongezea kodi walala hoi.

Mimi Mshahara wangu laki 8 ukiweka kodi, Bima, Loan board, NSSF unakuta nabaki na 55% ya mshahara huu mshahara nianze tena kuweka makato ya simu na vocha na Tigo pesa na mpesa nitabaki na nini?

Jiulize sasa kwa mtu ambaye hana mshahara mnamuumiza kiasi gani kumbuka kuna watu wanategemea vimiamala tu kuishi kiukweli inauma.

Wabunge, Mawaziri, Makatibu na Rais wao wala hawana habari na kulipa kodi!

Nimelikatia tamaa hili taifa, taifa limepotea Bora pamoja na mapungufu yake Magufuli alikula na Masikini.
 
Huyu Bibi sijui tumetokana wapi naye!!!
 
Umeongea kwa uchungu mno... Huo ndio uhalisia...lakini bado ma ana nafasi ya kuondoa huu uchungu mpya mioyoni mwa wananchi wengi wasiojiweza
 
Back
Top Bottom