Utawala bora wa serikali ya kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utawala bora wa serikali ya kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 24, 2010.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Harufu kali ya rushwa ndani ya CCM kwa wanachama wa chama hicho wakati wa kura za maoni ilinishtua, na taasisi ya kuzuia rushwa ilionekana imekamilika kulivalia njuga. Karibu kila kona ya nchi kwenye kura za maoni ya chama cha mapinduzi zilitawala habari za rushwa tu. Nikabaki mdomo wazi kama mambo ni hivyo kwa chama chenye kushika dola kwa nusu karne itakuwaje katika vyama vingine vilivyochipukia tu? Nikabaki vuta subira nione na vyama vingine vemejipaka manukato yenye harufu mbaya ya rushwa kama sisiemu au la.

  Hatimaye vyama vingine navyo vikaanza mbio za maratoni kwa wagombea nafasi mbalimbali kutafuta ridhaa ya vyama vyao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Cha ajabu sijasikia malalamiko ya pekee kuona wagombea wa vyama vingine kuwa na mchakacho wa sura yenye harufu ya rushwa hadi mradi huo unakamilika. Nilichosikia na kusoma kwenye vyombo vya habari wagombea wa vyama vingine vya siasa kurubuniwa na wagombea wa CCM kuhongwa wasirejeshe form za kugombea ili wapite bila kupingwa ingawa habari hizo hazina uthibitisho. Kwa mantiki hiyo rushwa ni ndani ya viongozi wa CCM kwa uthibitisho wa kura za maoni ndani ya chama cha CCM.

  Kipindi cha kampeni tumeshuhudia vyama vingi kulalamikia chama cha mapinduzi kuvuruga mikutano ya vyama vyao pale ilipoonekana vyama hivyo vinamvuto zaidi yao. Na kabisa chama kilichoonekana ni mpinzani mkubwa zaidi wa CCM ndio mikutano yake imekuwa na vurugu kubwa toka chama cha CCM. Ilitokea hata mgombea wa CCM kuzidisha muda wa kampeni majira ya jioni isivyo halali na vyombo husika kuona inafaa lakini chama kingine kikifanya vingine vilitishiwa kuchukuliwa hatua kwa kuzidisha muda wa kampeni kama ilivyotokea mgombea urais ccd katika moja ya mikutano yake kule mbeya kutishiwa na kiongozi wa polisi wilaya na kukataa kulinda chopa yake. Mwendelezo huo ulihitimishwa kwa malalamiko makubwa katika hatua ya kutangaza matokeo ambayo yalitangazwa na Nec kutofautiana na yale yaliyotolewa vituoni.

  Habari mbaya zinazojitokeza sasa hivi kwa uchaguzi wa mameya katika majiji na wenyeviti wa halmashauri, hali ikiwa mbaya na tete katika majiji na halmashauri zinazoongoza kwa wingi na wajumbe kutoka vyama vya upinzani. Vurugu hizo zimefikia hatua ya vyombo vya dola kuchukua hatua ya hoja ya nguvu dhidi ya viongozi waliochaguliwa na wananchi. Hata hivyo serikali haijatamka lo lote katika matokeo hayo ingawa inasisitiza utawala bora unaofuata sheria. Pamoja na kauli ya serikali ya kusema inafuata utawala bora wa sheria, lakini imeonekana wakurugenzi na waandamizi wa chama tawala kupindisha sheria kwa makusudi ili mradi kuendeleza wimbi la kushinda hata uchaguzi wa mameya katika mazingira yasiyopokeleka, ili mradi kushika hatamu za uongozi.
  Kwa matokeo hayo inaweza tafsiriwa kwamba mipango na maelekezo ni kutoka juu na wachini lazima wafuate maelekezo. Kama si mipango toka juu iweje wahusika katika idara zote za juu wakae kimya bila kutoa tamko lo lote na wakati hayo yanaonekana wazi ni machafuka katika uchaguzi wa mwaka huu? Ndivyo tunavyoonekana kimataifa sasa kwani siyo siri tulikuwa tunajitahidi kufunika jipu sasa linazidi kuiva na tusipojitahidi laweza pasuka na kutoa usaha wenye harufu mbaya kuliko ya harufu ya rushwa na ufisadi.
  Huo ndio utawala bora unaofuata sheria tunaoimba kila siku?

  Tanzania imekuwa na jina zuri, na viongozi wake wamekuwa wakitoka vifua mbele ya mataifa na kufanya kama mfano wa kuigwa na mataifa mengine, leo hayo yamegeuka wakati wananchi wanazidi kuamka na kuongeza kasi ya demokrasi. Huenda viongozi walikuwa wanatamba hivyo kimataifa kwa sababu watanzania wengi tulikuwa hatujaamka. Kwa bahati mbaya waliobahatika kupata madaraka yamewalewesha na hivyo kutofuata haki ya demokrasia na utawala bora, baada ya kunogewa wanapotakiwa wawapishe wapendelewa na wananchi basi mfumo wa utawala bora tunaubadilisha kwa utaratibu wa sheria binafsi tunazojua watawala.

  Utawala bora usingefumbia macho mgombea ubunge wa CCM akimkata ngwara OCD sijui au OCS ofisini kwake akiwa kazini na kukaa kimya hadi leo wakati mgombea wa upinzani Shibuda akiswekwa ndani wakati hakujua nini kilichotokea. Utawala bora lini ukafumbia macho upindishaji wa sheria ili mradi kuchukua ofisi ya umeya? Huo ndio utawala bora unaofuata sheria? Hawa mawaziri waliopewa wizara za utawala bora, tawala za mikoa, sheria na kadhalika wamepewa nafasi hizo kama kirima au wajibu? Nini kinaendelea nchini sasa hivi katika mchakacho wa chaguzi za wenyeviti wa halmashauri na mameya?

  Kwa maana hiyo ukimya wa watawala na waandamizi wahusika katika idara zao kufumbia macho yanayotokea kama nilivyosema hapo juu inaweza tafsiriwa kama ni maelekezo toka juu. Tulijitoa kuwasaidia watani zetu wa HARAMBEE kana kwamba sie ndio tunaojua utawala bora na washeria, leo hayo yanatokea naona tuombe jumuiya ya kimataifa imtume Mwai Kibaki Rais wa wanaharambee aje lipa deni alilonalo kwa sisi kwenda kuwasuluhisha aje atusuruhishe, maana anaujuzi wao wamewezaje kuwa na utawala bora na washeria na wametulia. Sijui ninapoenda mataifa ya nje sasa watanionaje na watanielewaje? Jibu ninalo mwenyewe.

  Katika biblia nakumbuka historia ya Mfalme Sulemani wa Waisraeli alipotakiwa aombe kitu muhimu katika maisha na utawala wake. Kwa ujasiri wa moyo wate aliomba Mungu amjalie "Hekima." Aliomba kitu adimu hekima badala ya wengi wa watawala ambao hupeperukia kwenye utajiri na kupeteza mwelekeo sahihi wa maana ya utawala bora unaofuata sheria.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ubabe ndo njia pekee wanayoweza kutumia kunyamazisha wanaojaribu kubadilisha mambo!Utendaji kwao hauna umuhimu wowote...wanachojali ni kukomba vijisenti vyote vya Wadanganyika tu basi!
   
Loading...