Utausherekeaje uhuru wa Tanganyika huru?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,645
Reaction score
10,865
Hili swali linamuhusu Mtanganyika Mzalendo tu. Na Mtanganyika Mzalendo, kwa mujibu wa huu uzi, ni Mtanganyika yeyote anayeipenda nchi yake ya Tanganyika bila kujali anakoishi.

Ikiwa wewe ni Mtanganyika Mzalendo, utausherekeaje uhuru wa Tanganyika huru?

Uhuru upo karibu. Dalili zinaonesha kuwa muda wa Tanganyika kurejeshewa uhuru wake umekaribia. Utausherekeaje huo ushindi?

Kwangu mimi, hilo litakapofanyika, nitafanya yafuatayo:

Kwanza kabisa, nitafanya sala ya kumshukuru Mungu kwa kurejeshewa Tanganyika yetu. Ikiwezekana, nitatoa na Sadaka'.

Pili, siku hiyo kutaliwa mlo maalum nyumbani kwangu. Lazima kufanyike kasherehe kadogo kazuri ili familia, ikiwezekana, na majirani wachache, washerekee kwa vyakula na vinywaji vizuri. Hilo litafanyika hata kama nitakuwa safarini.

Hivyo ndivyo nitakvyosherekea siku Tanganyika itakaporejeshewa Uhuru wake. Wewe utasherekeaje?
 
Waunguja wanasema hawataki Muungano,hawataki kuwa koloni la Tanganyika.
Na Watanganyika wanasema nini? Hawataki Muungano,hawataki kuwa koloni la Unguja.
Sasa,hawa watu,hawawezi kuwa wote sahihi. Someone here has drunk too much wine .
 
Waunguja wanasema hawataki Muungano,hawataki kuwa koloni la Tanganyika.
Na Watanganyika wanasema nini? Hawataki Muungano,hawataki kuwa koloni la Unguja.
Sasa,hawa watu,hawawezi kuwa wote sahihi. Someone here has drunk too much wine .
And you know the one who is drunk!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…