Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika: Bevin Tipha Msowoya mpiga picha nguli wa wakati wa kupigania Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,900
30,235
MIAKA 60 YA UHURU: BEVIN TIPHA MSOWOYA MPIGA PICHA NGULI WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

Leo ni siku yangu ya furaha kubwa sana kupita kiasi.

Niko online na binti mmoja namjua kwa jina la Charming Girl kaniona akaniuliza kama namjua Bevin Tipha Msowoya?

Nikamwambia naam namjua Msowoya mpiga picha na nikamweleza mengi kuwa nimemjulia Kinondoni katika miaka ya 1960s mimi nikiwa mtoto mdogo nasoma shule ya msingi.

Miaka ile Kinondoni kulikuwa na jamii ndogo ya Wanyasa na nawakumbuka rafiki zangu tuliokuwa tunasoma pamoja, Kinsley Tenis na marehemu Bruno Msowoya.

Siku nyingine hawa Wanyasa wakicheza ngoma ya kwao wamevaa mashati meupe, tai, stocking nyeupe na viatu vyeusi.

Nakumbuka tulikuwa na mwalimu wetu Mnyasa akicheza ngoma hii na sisi wanafunzi tukipenda kwenda kumwangalia mwalimu wetu akicheza ngoma.

Kinsley na Bruno naamini walikuwa na ujamaa na Mzee Msowoya. Huyu bint akaniambia kuwa Msowoya ni babu mzaa mama yake.

Mshtuko mkubwa ulinipata.

Akili yangu imekwenda kwenye maktaba ya picha ya Msowoya.

Nikamwambia kuwa nina picha 11 alizopiga babu yake mwaka wa 1954/55 zilizobeba historia kubwa sana ya Julius Nyerere, TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Picha hizi zilinifikia kupitia watoto wa Ali Msham ambae alikuwa na ukaribu mkubwa sana na Mwalimu Nyerere na Mama Maria.

Kwanza na Mwalimu Nyerere alipokuwa anaishi Kariakoo nyumbani kwa Abdul Sykes kisha na Mama Maria walipohamia Magomeni Maduka Sita.

Hii ilikuwa mwaka wa 1955.

Nimemwomba huyu bint ruksa nitumie picha hii moja ya babu yake Bevin Tipha Msowoya aliyonipa ili watu wamtambue mzalendo huyu aliyetumia kipaji chake cha upigaji picha kutuhifadhia historia ya uhuru wa Tanganyika.

Bwana Msowoya mjukuu wake amenieleza kuwa alishuhudia kupandishwa kwa bendera ya Tanganyika huru na kuna video inamuonyesha akikimbia huku na huko Uwanja wa Taifa akipiga picha za sherehe za uhuru 9 Desemba, 1961.

Bado nipo katika mazungumzo na mjukuu wake na In Shaa Allah nitaleta hapa barzani kila kitu kuhusu Mzee Msowoya kwa faida ya historia ya Tanzania kila atakaponipatia.

Fatilia hapa...

Screenshot_20211124-061352_Facebook.jpg
 
Sawasawa kumbe wanyasa walihusika pakubwa katika harakati za uhuru wa Tanganyika
 
Back
Top Bottom