DOKEZO Utatuzi wa wizi wa TARURA kupitia kimulikwa ni mgumu, tutaendelea kuumizwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana JF,

Nimekumbwa na tatizo la kumulikwa na watu wa maegesho. Nilienda kulipia nikashangaa deni linaongezeka kucheck majumuisho nikakuta kuna sehemu ambazo nilipita lakini sikusimama wala kiegesha lakini nakuta nadaiwa fedha za maegesho.

Kuna sehemu nyingine natajiwa hata sipajui lakini nadaiwa. Huu wizi umebarikiwa na serikali kupitia vijana wenye roho mbaya ya kukomoa wenye magari.

Serikali haikuweka sehemu ya kulalamika ili tuonyeshwe kwa uwazi sehemu husika tulizopita au tuliegesha. Kila mtu huwa ana kumbukumbu ya matumizi yake ya gari, iweje TARURA watulazimishe kulipia tusichotumia?
 
Back
Top Bottom