Utata waibuka uuzaji migodi ya dhahabu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata waibuka uuzaji migodi ya dhahabu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Habari

  Mary Victoria


  Toleo la 259
  19 Sep 2012

  WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema atahakikisha kampuni ya China National Gold Group Corporation (CNGGC) ambayo iko mbioni kununua hisa zaidi ya asilimia 30 za kampuni ya African Barrick Gold (ABG) kwamba haichimbi madini nchini hadi hapo ABG itakapolipa madeni yote inayodaiwa na Serikali ya Tanzania, Raia Mwema limeelezwa.


  Msimamo huo wa Serikali umetokana na taarifa za hivi karibuni ambazo pia zilithibitishwa na Profesa Muhongo kwamba ABG imekuwa kwenye majadiliano ama tayari imeshajadiliana na kukubaliana na CNGGC juu ya kuuza hisa zake.

  Profesa Muhongo amesema wameanza kuchunguza taarifa hizo na kwamba atahakikisha kampuni hiyo ya China haichimbi madini nchini hadi kampuni ya ABG ihakikishe imelipa madeni yote inayodaiwa kutokana na shughuli zake za uchimbaji madini nchini.


  "Tutahakikisha kwamba kila kitu kinalipwa la sivyo atakayenunua hisa za kampuni ya ABG ndiye atakayelipa madeni yote kabla ya kuanza uchimbaji. Tunaendelela kufuatilia kila kitu kwa ukaribu sana, kwa kuwa wao wanatumia akili nyingi inatakiwa umakini kwelikweli,"alisema Profesa Muhongo na kuongeza:


  "Ikiwa hawatalipa na wataamua kuwadanganya Wachina, basi Wachina hao uchimbaji wao utakuwa mgumu na hivyo nitamueleza pia Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing kuhusu kampuni hiyo, ikiwa itanunua hisa za kampuni ya ABG iwe tayari kulipa gharama zote ambazo ABG imekwepa kuzilipa."


  Kauli hizo za Profesa Muhongo zinafuatia maoni kwamba Wizara yake inawachukua hatua gani kwa wamiliki wa kampuni za uchimbaji madini, gesi asilia na mafuta ambazo zimekuwa zikikwepa kulipa kodi kwa muda sasa na baadhi zimeamua kuuza hisa kwa kampuni nyingine ya kigeni kama ambavyo ABG inataka kufanya kwa sasa.


  Maoni hayo yanatokana na taarifa ya ABG kupitia barua pepe kuwa imekuwa kwenye majadiliano ya kuuza baadhi ya hisa zake kwa kampuni hiyo ya Kichina.


  Taarifa ya kuwa kuna majadiliano imethibitishwa pia na ofisi za ABG Dar es Salaam katika andiko lake kupitia kwa msemaji wake, Nector Foya, linalothibitisha kuwa kampuni hiyo iko katika hatua ya awali ya majadiliano na kampuni hiyo ya China.


  "Wakati huu hakuna uhakika kwamba majadiliano hayo yanaweza kufikia muafaka kutokana na kwamba bado ni mapema kwamba majadiliano yanaweza kukamilika iwapo CNGGC itachukua zaidi ya asilimia 30 za ABG, kulingana na soko la hisa la London (London Stock Exchange) ABG inathibitisha kuwa ina hisa paundi bilioni 4.1 katika soko la hisa.''


  Wakati ABG ikitoa ufafanuzi huo ripoti ya Mpango wa Uhamasishaji Uwazi kwenye Mapato ya madini, gesi asilia na mafuta (TEITI) iliyo chini ya Mwenyekiti Jaji Mark Bomani imeweka wazi kuwa kuna uwezekano kuwa ABG inaweza kuwa inadaiwa.


  Ofisa mmoja wa TEITI anasema: " Katika ripoti ya pili ya TEITI ya Julai 2009 mpaka Juni 2010, mapato yote ya Serikali yalikuwa bilioni 419 kutoka katika makampuni ya uchimbaji madini na gesi asilia na mafuta, katika mgawanyo huo ulipaji wa kodi kwa makampuni yote si mzuri, yanalipa asilimia saba tu, madai yao ni kwamba hayapati faida."


  Ofisa huyo anasema takwimu hizo ni kwa mujibu wa ripoti ya pili, " tu naposubiri kuandaa ripoti ya nne ya mwaka wa fedha 2012/ 2013 hatuna hakika ikiwa kampuni hiyo unayozungumzia ya ABG imelipa kodi ya mapato kwa mwaka wa fedha 2011/ 2012."


  ABG ina migodi kadhaa nchini katika maeneo ya Tulawaka, Biharamulo mkoani Kagera; Buzwagi na Bulyanhulu, Kahama, Shinyanga na North Mara, Tarime mkoani Mara


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hata kama ZITTO KABWE anamaamuzi au uwalakini wa Prof. Muhongo kwa ajili ya UHUSIANO wake wa kuwa Meneja Mkuu wa

  STAMICO iliyonunuliwa na VIBEPARI Mkapa - MRAMBA na Mfungwa Mwenzake MRAMBA bado ninaona angalau Prof. Muhongo

  anaweka vitu hewani wananchi kuelewa...
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  "Angalau" Ndiyo nini?
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  At Least...
   
 5. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mhongo anaongelea kodi ajue kwenye hiyo migodi kuna watanzania tupo tunafanya kazi haki zetu vipi zinakuwaje? Kuna sheria gani kama kampuni ikiuzwa mwenye ufahamu anijuze wafanyakazi wakitanzania hata wazungu tunaishi kwa wasiwasi hadi uzalishaji unashuka na ikizingatiwa na Nssf wamezuia mafao yetu yaani hii nchi sijui vp naona ndiyo maana usishangae waarabu kujitoa mhanga
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Niambie kwa lugha ya kwetu kisandawe, hizo lugha zilizoletwa kutughilibu dhahabu zetu zitoweke hainibariki!
   
 7. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  sina hakika what is our policy on foreign investments is well known from individual and nation, kumwelekeo as kila mtu na lwake hata ndani ya nyumba moja. nahisi better invest in Somalia rather TZ. Somalia inajulikana adui ni nani. Hapa waliambiwa CDM wakatoa msaada sasa wamegundua hata yule aliekuwa anamsingizia CDM kumbe nae anamla.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa hapo ndio unaleta UMASIKINI wa KIKABILA... Dhahabu NYINGI ZIKO MIKOA YALIYO kando kando ya ZIWA kwahiyo LUGHA Ingekuwa KISUKUMA

  Sio Kisandawe -- POLE SANA... SIJUI TENA HAKI IKO WAPI KWAKO!!!
   
 9. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu waziri ana shule kichwani mimi nilisoma Cv yake nikaishia njiani, jamaa ni kichwa mno hata mgao wa umeme nimeanza kuusahau, sasa ngoja awabane hao wakanada. Na nashauri waziri awafike karibu wafanyakazi wa Barrick nao wapate sitahiki zao kabla mzungu hajauza. Kuna suala lingine la mishahara wafanyakazi wengine wanahofia mchina awaze kushusha zile scale za Barrick make hawa jamaa wa Asia ni wagumu mno, waziri simama kidete kuwatetea wafanyakazi wa hawa.
   
 10. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Prof Muhongo endelea kupambana na hao wezi wa madini yetu.
   
Loading...