Utata wa picha za anga na kutoonekana kwa nyota

mwaminifuhalisi

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
329
412
Picha nyingi ambazo zimepigwa angani na satellite, nyota huwa hazionekani, lakini kwa mujibu wa wataalamu wa maswala ya anga hudai kwamba hapa duniani tunaweza kuona nyota chache sana kutokana na pollution, na zinaweza kuonekana vizuri sana maeneo kama vijijini ambapo pollution ni ndogo, lakini bado nyota zinazoonekana duniani ni chache.

Kitu ambacho kiliwasukuma wanasayansi wa NASA kuachana kutumia ground Telescope na kutumia telescope zinazonguka angani kama satellite mfano ni kepler telescope na Hubble Space Telescope ili kupata taarifa kwa undani kuhusu maswala ya anga, kwa maana kwenye anga hakuna atmosphere na hivyo nyota huonekana kwa urahisi sana.

NASA-Apollo8-Dec24-Earthrise.jpg

picha ya dunia inavyoonekana mwezini huku nyota zikiwa hazionekani.
sasa swali linalosumbua kichwa ni kwa nini picha nyingi ambazo zimepigwa angani na wanaanga ama telescope nyota huwa hazionekani?.
 
Hii picha ilipigwa na satellite inayozunguka mwezi, hapo jua lilikuwa kali sana mwezini hivyo mwanga ulikuwa mwingi. Kumbuka mwezini hakuna atmosphere wala mawingu. Kwa mwanga huo huwezi kuona nyota kirahisi. Ni kama hapa duniani, huwezi ona nyota mchana kirahisi.
 
lakini mkuu, wanasayansi wanasema nyota zinaonekana vizuri sana kwenye kwa sababu hakuna atmosphere na ndo maana zikatumwa space telescopes, sasa iweje unasema kwa sababu hakuna atmosphere ndio maana picha hazionyeshi nyota?, chukulia mfano wa hii picha
nostars-1200x796.jpg

hili ni jibu toka kwa mwanaanga
Of course we can see stars in space. We see stars more clearly from space than we do from Earth, which is why space telescopes are so useful
 
lakini mkuu, wanasayansi wanasema nyota zinaonekana vizuri sana kwenye kwa sababu hakuna atmosphere na ndo maana zikatumwa space telescopes, sasa iweje unasema kwa sababu hakuna atmosphere ndio maana picha hazionyeshi nyota?, chukulia mfano wa hii picha
View attachment 477251
hili ni jibu toka kwa mwanaanga

Hujanielewa mkuu, nimesema kwa kuwa hakuna atmosphere mwanga wa jua unakuwa mkali zaidi. Lakini usiku nyota huonekana vizuri zaidi kuliko duniani
 
Back
Top Bottom