Utata wa Oklahoma City Bombing 1995

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,704
Tarehe 19 mwezi wa 4 mwaka 1995, kulitokea tukio la kulipuliwa kwa jengo lililokuwa likimikiwa na serikali lijulikanalo kama Alfred. P. Murrah, lililokuwa katika jiji la Oklahoma, USA.
Takribani watu 168, 19 wakiwa ni watoto walifarika na mamia kujeruhiwa vibaya sana.
Ndani ya dakika 90, yani saa moja na nusu, polisi waliokuwa karibu na mpaka wa Kansas walisimamisha gari la kizamani aina ya Mercury lilikuwa halina na namba za usajili likiwa linaendesha na kijana ajulikanaye kama Timothy James McVeigh.
Baadae ilikuja kutolewa taarifa kuwa McVeigh ndiye mhusika mkuu katika kulipuliwa kwa jengo hilo akishirikiana na mwenzake ajulikanaye kama Terry Nicholas.
Kwa madai ya FBI, wanalisema McVeigh na mwenzake, walitenda kosa hilo kama kulipinga uvamizi wa polisi dhidi ya wafuasi wa dhehebu lijulikanalo kama Davian, ambapo askari walivamia ofisi za dhehebu hili zilizo Waco, Texas na kukatokea mapigano makubwa na kusababisha vifo vya watu 76.
Tukio hilo lilikuwa limetokea mwaka 1993, yani miaka miwili nyuma ya tukio la Oklahoma City Bombing.

NINI KILITOKEA SIKU YA TAREHE 19/04/1995 KWA MAELEZO KUTOKA FBI

Tarehe 19, mwezi wa 4 mwaka 1995, muda wa saa tatu na dakika mbili adubuhi, gari la kukodi likiwa limesheheni milipuko lilipaki mbele ya jengo la Alfred. P. Murrah.
Baada ya muda gari hilo lililipuka na kuharibu vibaya ukuta wa sehemu ya Kaskazinu ya jengo hilo kwa kuangusha ukuta.
Vikosi vya dharura nchi nzima vilipata taarifa na kukimbilia eneo la tukio kuokoa watu.
Siku hiyo hiyo askari wa doria wanamkakata Timothy Mcveigh kwa kosa la kuendesha gari bila namba ya usajili, pia kwa kukutwa amebeba bunduki bila kibari. Anapelekwa na kuwekwa ndani.
Tarehe 21 mwezi wa nne yani siku mbili baada ya tukio, kuna shahidi anayedai alimuona McVeigh akiacha hilo gari mbele ya jengo hivyo kwa maelezo yake wataalamu wanaweza kuchora taswira ya McVeigh.
Siku ambayo McVeigh ilikuwa aachiwe kutokana na kosa na kuendesha gari bila namba ya usajili na kuwa amebeba bunduki bila kibari, polisi wanagundua kumbe ndiye mtuhumiwa anayetafutwa hivyo wanamkabidhi kwa FBI.
Siku hiyo hiyo kijana ajilikanaye kama Terry Nicholas anajisalilisha mwenyewe na kudai kuwa alikuwa mwenza wa McVeigh katika kutekeleza shambulio hilo.
Tarehe 8 mwezi wa 8 mwaka 1995, mwanaume ajulikanaye kama Michael Frontier anawambia FBI kuwa alikuwa anajua mpango wa McVeigh kufanya shambulio hilo kwakuwa aliwahi kumwambia.
FBI wanamuomba awe kama shahidi wakati wa kesi, naye anakubari.
Kwa maelezo ya FBI wanadai mlipuko wa hilo gari ulitokana na Ammonium nitrate pamoja na nitromethane almaarufu kwa Fertilizer Bomb.
Baada ya wote kushitakiwa walikutwa na hatia ambapo McVeigh alihukumiwa kunyongwa huku Nicholas akihukumiwa kifungo cha maisha.
McVeigh alinyongwa kwa kuchomwa sindano ya somo mnamo tarehe 11 mwezi wa 6 mwaka 2011.

TIMOTHY JAMES MCVEIGH NI NANI?
Mcveigh alizaliwa tarehe 23, mwezi wa 4 mwaka 1963.
McVeigh alikuwa mtoto pekee wa kiume katika familia ya watoto wa tatu ya Bwana William McVeigh na Bi Mildred Noreen.
Wazazi wake ambaobwalikuwa na chimbuko la Irish, walitengana McVeigh akiwa na umri waiaka kumi hivyo McVeigh alibaki na baba yake na walihamua Pendleton, Newyork.
Kutokana na maelezo yake, anadai akkiwa shule alionewa sana kwakuwa analionekana mnyonge hivyo alijipa moyo kwa kuishu kwenye ulinwengu wa kufikirika ambapo alijiona yeye akiwa mtu mwenye nguvu akipambana na wote waliokuwa wakimuonea na kuonea watu wengine.
Wakati kesi yake ikiendelea mahakamani, McVeigh aliwahi kusema mbele ya mahakimu kuwa, serikali ya Marekani ndiyo inaoongoza kwa kuonea watu katika dunia hii. Hivyo alionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya serikali.
Pia historia ya maisha yake inaonyesha ya kwamba aliwahi kuwa na mpenzi mara moja tu na ambaye hawakuweza kudumu kwa kipindi kirefu.
Yeye mwenyewe McVeigh alidai ya kwamba hakuwa anajua jinsi ya kuongea na wanawake na kuwafanya wavutiwe naye ndiyo maana hakuwa anajihusisha na masuala ya mapenzi.
Rafiki zake wanadai alikuwa mtu mpole asiyezungumza sana na alikuwa ni mwenye aibu sana.
Akiwa sekondari, alitokea kupenda sana komputa na aliwahi shambulia mtandao wa serikali na kuvujisha taarifa za serikali, jambo hili lilimfanya awe mashuhuri na kubatizwa jina la Starpoint wa Central High School na watu walitegemea aje kuwa programa mwenye iwezo wa hali ya juu sana huko mbeleni lakini haikuwa hivyo kwa maana alikuwa akipata alama za chini sana katika masomo yake mpaka alipohitimu mwaka 1988.
Kutoka na ukaribu na babu yake, McVeigh alifunzwa matumizi ya bunduli aina mbalimbali jambo lililomfanya akapenda sana bundiki hadi akawa muda mwingine anaenda nazo shuleni kuwaonyesha wenzake.
Pia alikuwa na ndoto ya kuja kumiliki duka la kuuza bunduki aina mbalimbali.
Jambo hilo ndilo lilimfanya ajiunge na chuo cha jeshi cha Fort Bennings, kilochopo Georgia ambapo alihitimu mafunzo ya kijeshi mwaka 1988.
Akiwa jeshini McVeigh alitumia muda wake wa ziada kusoma kuhusu siraha za moto, mbinu za udunguaji na kutengeneza vilipuzi vya aina mbalimbali.
McVeigh alipelekwa kupigana vita ya Guba katika oparasheni iliyojulikana kama Desert Storm, katika vita hiyo McVeigh anadai kwamba siku ya kwanza kwake katika uwanja wa vita alimkata kichwa kijana wa Ki Iraq kwa kutumia mzinga na alifurahia sana jambo hilo.
Pia anadai alishtuka alipopewa amri ya kuwaua mateka waliojisalisha kwakuwa hakutegemea kama jeshi la Marekani linaweza fanya unyama kwa mateka hao.
Kutokana na mchango wake jeshini alipata medali mbalimbali kama zifuatazo
Bronze star medal
National Defense medal
Service Nedal
South Asian Serive Medal
Army Service Robon na
Kuwait Veteran Medal.

Aliporudi kutoka kwenye vita ya Guba, alidhamilia kujiunga na kikosi maalumu cha jeshi la Marekani. Alifanikiwa kujiunga na mafunzo katika kikosi hicho ila baada ya siku 21 toka mafunzo yaanze aliondolewa.

Mwaka 1991, McVeigh aliamua kuachana na jeshi kabisa na kufanya kazi mbalimbali hasa ulinzi.
Baadae aliacha kazi akaanza zunguka zunguka sehemu mbalimbali akiwatafuta rafiki zake aliokuwa nao jeshini.
Pia alikuwa akiandika barua mara kwa mara kwenye magazeti akilalamika juu ya kodi kubwa ambayo serikali inawatoza wananchi pamoja na uonevu wanaofanyiwa watu mbalimbali na serikali ya Marekani.
Akiwa na rafiki zake huko Decker Michigan aliwahi sikika akisema ya kwamba, kabla ya kuondoka jeshini aliwekewa kifaa ndani ya makalio yake ili waweze kumfuatilia kila anapokwenda.
Kutoka na kutokuwa na kazi, McVeigh pia hakuwa na makazi alikuwa hana sehemu ya kulala akawa mtu wa kucheza sana kamari jambo lililofanya we na madeni makubwa sana.

cbb52d3ca08a77780e83a7d86c7226c4.jpg

Jengo la Alfred. P. Murrah baada ya shambulizi
a2fcb1b53422b2707fa41b554b976f5e.jpg

Picha ya McVeigh
cb89fe922a56be91770bbce6f98db12c.jpg

Picha ya Terry Nicholas
5f5bff5b9f1515aae3685990cf52520b.jpg

Picha inayoonyesha michoro iliyochorwa kutokana na maelezo ya mashahidi.

Itaendelea sehemu ya pili kuonyesha utata kuwa kuna kitu serikali ilikuwa inajaribu kuficha juu ya hili tukio ambapo zimeibuka na dhaharia na ushahidi mbali mbali uliokusanywa na wataalamu na mashahidi kuonyesha kuwa si McVeigh pekee au hakushiriki kabisa katika tukio hili.
Madame B miss chagga
 
Duh Mkubwa, wakati unaianza hukujua kuwa watu wengi wataitaji mwendelezo wake mpaka upigiwe kelele?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nliacha kwa kuwa watu walianza weka link link wakasome as if nlienda ni kacopy na kupaste kumbe nimetazama nikasoma kwenye sources zaidi ya 3 ndiyo nikaandika nilichoandika kwa hiyo nilidhani labda watu watamalizia kwenye link walizowekewa maana wengine walianza hata nishambulia
 
Safi sana, sisi hatuna matukio yakufukua kama hayo?
Mfano mabomu ya kanisani Olasiti kule Arusha!
 
Safi sana, sisi hatuna matukio yakufukua kama hayo?
Mfano mabomu ya kanisani Olasiti kule Arusha!
Sisi kwanza hawaruhusu watu wasiyohusika kufanya uchunguzi eneo la tukio.
Hata kesi hawaruhusu watu kuzichungusa mfano kesi ya babu seya ingekuwa ishafanyiwa uchunguzi upya
 
Hii stori inaonekana mletaji ameiiba sehemu ikiwa imetafsiriwa sasa mwenyewe amestuka ndio maana imekwama kuendelea

Send via Quan dong fen from north Korea
 
Back
Top Bottom