Utata wa hesabu: Naibu waziri afya anadai tunapima kwa siku watu 500 na wanaohisiwa tu, na kati ya hao walio ambukizwa ni kati ya 70%-80%

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868

"Kuhusu vipimo vya ugonjwa wa Covid 19, niwathibitishie wabunge kwamba maabara yetu ya Taifa sasa hivi inafanya kazi saa 24 na tuna uwezo wa kupima sampuli mpaka 500 kwa siku, tumefanya tathmini ya maabara tisa ndani ya nchi yetu ambazo zina uwezo wa kufanya upimaji huu, upimaji huu huwezi kuuweka katika zahanati au kituo cha afya"-Dk. Ndugulile, Naibu Waziri wa Afya Tanzania.

Hoja:

Hata kama tunapima watu 100 kwa siku then tuseme 60% ni positive hawa si ni watu 60? Kwa siku?
 
Tanzania sa hivi wagonjwa wa corona kama dar najua wanachezea laki kadhaa. Wakisema wakae wanapima kweli namba watakayokutana nayo itatisha kila mtu kama wanaopimwa 70-80% ni wagonjwa hao wagonjwa wameutoa wapi?

Na watu hata hawajifungii hapo kila moja wao atakua kaondoka na watu kama watatu minimum jinsi bongo ambavyo hakuna social distancing. Yaani kama upo dar hujaugua una bahati kubwa tu.

Wana ukaribu na mataifa yenye test zinazoweza kutoa majibu ndani ya saa moja kama south korea wanaona aibu kuomba? Marekani yenyewe iliomba msaada wakatumiwa testkit laki kadhaa. Tanzania jiwe ashaamua liwalo na liwe hataki kujisumbua. Mwaka huu kura yangu bora nimpe mbwa kuliko jiwe.
 
Umeleta taarifa kishabiki..umepoteza utamu wa mjadala. Siwezi kuchangia.
 
Ukisikiliza hiyo clip,waziri anasema(kwa maneno yake) kuwa, katika sampuli 100 wanazochukua,70 % up to 80 % wanazikuta positive.

Kwa lugha nyingine,katika watu kumi wanaowapima,watu saba mpaka nane wana-test positive..
 
"Kuhusu vipimo vya ugonjwa wa Covid 19, niwathibitishie wabunge kwamba maabara yetu ya Taifa sasa hivi inafanya kazi saa 24 na tuna uwezo wa kupima sampuli mpaka 500 kwa siku, tumefanya tathmini ya maabara tisa ndani ya nchi yetu ambazo zina uwezo wa kufanya upimaji huu, upimaji huu huwezi kuuweka katika zahanati au kituo cha afya"-Dk. Ndugulile, Naibu Waziri wa Afya Tanzania.

Hoja:

Hata kama tunapima watu 100 kwa siku then tuseme 60% ni positive hawa si ni watu 60? Kwa siku?

Hata tukichukua hesabu za chini kabisa kwa mujibu ya Ndugulile, yaani (70/100)*500 = 350. Ndiyo kusema kwamba kwa kiwango cha chini kabisa kila siku wanaghundulika watu 350 wakiwa Covid_19 + nchini TZ. Bw. Ndugulile, anza kutafuta hoja nyingine ya kumfichia Siri bosi wako Waziri Mkuu.

Serikali yenu mmeshaanza kujenga mnara wa babeli. Mnapishana. Polepole mtaanza kukimbiana ofisi. Jambo hili limeshaanza kutoa tafsiri mbaya ya uwezo wa serikali kupambana na janga hili la Corona.
 
"Kuhusu vipimo vya ugonjwa wa Covid 19, niwathibitishie wabunge kwamba maabara yetu ya Taifa sasa hivi inafanya kazi saa 24 na tuna uwezo wa kupima sampuli mpaka 500 kwa siku, tumefanya tathmini ya maabara tisa ndani ya nchi yetu ambazo zina uwezo wa kufanya upimaji huu, upimaji huu huwezi kuuweka katika zahanati au kituo cha afya"-Dk. Ndugulile, Naibu Waziri wa Afya Tanzania.

Hoja:

Hata kama tunapima watu 100 kwa siku then tuseme 60% ni positive hawa si ni watu 60? Kwa siku?

Huu ndiyo mwendelezo wa habari yenyewe:

1. "Tumeamua kusema ukweli .." mwisho wa kumnukuu.
2. "Tunapima sampuli hadi 500 kwa siku ... Tunachofanya sisi ni targeted testing ... ambayo yield yake 70% - 80% positive". Mwisho wa kumnukuu.

Walisema waungwana: njia ya mwongo ni fupi.

Kwa hakika njia ya mwongo ni fupi.
 
Back
Top Bottom