Nilitaka kuacha kuchangia kwenye mchakato wa kujadili Katiba ya Watanzania kwa sababu nilipata hasira tangu mwanzo wa uandaaji wa kanuni za kuendesha Bunge lenyewe. Hata hivyo uwepo wa maoni ya viongozi wetu wa Imani umenitia moyo na sasa nipo nanyi kutoa maoni yangu. Leo mchango wangu ni wa maswali na maoni kidogo sana. Hivi mswada wa rasimu ya katiba ni wa nani? Ukisoma preamble tunaona kuwa mswada huu ni wa serikali. Sasa iweje serikali yenye mswada ndivyo iwe mstari wa mbele kupinga mswada huo? Hiki ni kiini macho kwangu.
Kama serikali ilipopokea mswada huu iliona unamapungufu iliunda Bunge la Katiba la nini? Kwa nini haiku disown rasimu hii badala ya kutupeleka kwenye aibu hii ya kutokusikilizana na kutukanana ovyo katika chombo hiki ambacho kina beba dhana ya kutukuka kwa kuangalia malengo mapana ya utungaji katiba. Iweje Rais wetu mpendwa aongoze juhudiza kujipinga mwenyewe? Nasema hivo kwa sababu tume ya jaji warioba ni yake na kwa niaba yake ni yetu sote. Ninini kimeikumba serikali yangu tukufu, nini shida hapa wapendwa wangu.Kwa nini turuhusu mazingaombwe katika nyumba ile, Watanzania hawataturuhusu kuendesha mazingaombwe haya kwa gharama zao historia itatusuta na kutuhukumu. Ningependa RAis wangu aniondoe katika hofu hii kuwa kupeleka mswada huu ulivyo ilikuwa ni kuanzisha vurugu katika nchi yetu yenye amani. Mwanasheria wa serikali unahoja ya kujibu kama amani ya Zanzibar itaondoka kwa vioja vilivyojitokeza katika Bunge la katiba. Mimi naamini katika kukosea wakati wa uandaaji wa katiba ya Zanzibar tulifanikiwa kama nchi kuwapa wananzibari tunu ya utulivu na amani. Sasa mnataka turudi kule kweli? Nani asiyeona na kuamini kuwa majadiliano, kujeli, matusi na ubaguzi ndani ya BMK kwa kiasi kikubwa yameamusha hasira na chuki ambazo SUK iliziondoa angalau kwa muda. Asanteni