Suip
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 1,338
- 803
Mwaka huu kama ilivyo miaka kati ya mwaka 2008-2016 kulikuwa na utoaji wa pembejeo za kilimo yenye ruzuku kwa wakulima. Wakulima walengwa huchangia kiasi cha fedha na kiasi kingine kuchangiwa na serikali.
Kulikuwa na vocha maalum yenye nembo ya NMB(National Microfinance Bank) na hiyo vocha hutolewa kwa kila aina ya pembejeo, yaani 1).Vocha ya Mbegu 2).Vocha ya Mbolea ya kupandia 3).Vocha ya mbolea ya kukuzia.
Sasa tofauti mwaka huu eti hakuna vocha na utaratibu ni kama nilivyoonyesha kwenye attachment hapo juu.
Mkulima jina lake linaandikwa na namba kitambulisho chake na kusaini baada kulipa sehemu anayochangia na zaidi wakulima wanalazimika kununua mbegu tu, na wanaacha mbolea kwani kwa mkulima mdogo kuchangia 118000/=sio rahisi kwa wengine hivyo hulipa 42000/= na kusaini.
Je wakala hawezi kufanya udanganyifu kwenye hiyo chati ya majina ya wakulima?
Je kwa maeneo waliotangulia kupata pembejeo mwaka huu utaratibu ulikuwaje?
Je mwaka huu hakuna zile vocha kwani mwaka jana mkulima akishindwa anachukua mbegu na kusaini vocha ya mbegu tu baada kulipa fedha za mbegu, anaacha zingine.
Naomba msaada kwa walio na ufahamu kwani naona wakala hataki kuwaelewesha wakulima na anawafokea kama watoto jambo linalotia shaka.
Na baada ya kuona hilo nimewashawishi wakulima waache kwanza mpaka tuulize huko wilayani na bado mawasiliano yanaendelea ila nataka kuishirikisha jf. kwa mjadala zaidi.