Black Walker
Senior Member
- Oct 8, 2018
- 107
- 238
Wakuu poleni na majukumu, hoja yangu ni moja tu! Kuna hii issue ya watumishi wa umma kutakiwa kufungua ankaunt maalumu kwa ajili ya taarifa zao za kiutumishi lakini pia likiwemo suala la uhamisho kufanyika mtandaoni.
Yaani nasikia hakutakuwa na ule utaratibu wa awali wa kuandika barua. Wasiwasi wangu ni kwamba naona kama hii njia haitafanyika kwa ufanisi na huenda inalenga kuondoa kasi ya watumishi kuhama. Kwa upande wa Tamisemi naona kabisa uwajibikaji wao utapungua.
Kwa mfano kama tu kwenye ule mfumo wa kawaida mtu anaandika barua ya kuomba nafasi kupitia kwa mkurugenzi wake barua inakaliwa ofisini zaidi ya miezi mitatu bila kupitishwa sasa kwa huu mfumo si ndo kabisa watu wataumia sana na wale ambao tuko mbali na wenza wetu tutasahau kabisa.
Mwisho kabisa naomba kuelimishwa kwa namna utakavyoratibiwa maana ni watumishi wengi hawajui namna unavyofanya kazi.