Utaratibu wa kivuko cha kigamboni ni mbovu

Jan 24, 2012
32
21
wapendwa
leo nimeshangazwa sana na wale wanaokatisha tiketi baada ya kuniambia inabidi nije na chenji ya sh 200. Nikamuuliza mhudu huyo swali Je ni nani anapaswa kuwa na chenji kati yangu mi na wewe? alichonijibu, pisha nihudumie wengine? Nikaamua kumfuata kiongozi wao,naye alinjibu hivi: tafadhali naomba usome tangazo lile pale, nilipoenda kusoma hilo tangazo nimechoka kabisa,tangazo linasisitiza watu waje na chenji lakini halijasema usipokuwa na chenji hupati huduma

Jamani sasa hii nchi tunakokwenda kumeshaanza kuonekana
 
Hiyo ndiyo customer care ya Magufuli,
Ila sisitiza tiketi unapewa na unapopita lazima attendant aichane na uone ameichana
maana wanatabia ya kuikunjakuja na kujidai wanaichana kumbe uongo, kisha wanairejesha ndani/kwenye kioski
kisha wanazinyoosha tena na kuwauzia abiria. Fedha inabaki kwenye mifuko yao, ndiyo maana
wabunge wa DSM walisisitiza wapewe wiki moja wasimamie mapato.
Pale supervision ni mbovu sana...
 
Back
Top Bottom