Ndugu wana jf inafahamika kwamba bima ya afya unalipia sio huduma ya bure kwani unakatwa kwenye mshahara wako .
Nimesikitika kunyimwa haki ya bima ya afya ya mke wangu wa ndoa kisa jina langu nililotumia ni la ubatizo ni tofauti na majina ninayotumia katika vyeti vyangu vya taaluma ,cha kuzaliwa na cha NIDA
Bima wanadai "deedpoll" ndo nipewe haki ya bima kwa mke wangu .na hii kuipata itanigharimu sio chini ya laki na nusu .
Naomba kuuliza hivi ni haki kufanya haya yote ili hali kuna nyaraka kibao za mke kama namba ya NIDA wanazo ,vyeti vya watoto ambavyo jina la mke wangu lipo ?
Na je kuepuka kutumia vibaya hizo pesa zangu kupata deedpoll naweza kwenda kanisani wakabadili jina kwenye vyeti vya ndoa ? Maana jina langu la vyeti ni LUKA ilaa vya taaluma ni Gabriel ,yote yapo kwenye bible kama kanisani wanavyotka jina la ubatizo liwe ,na kwa sie tuliobatizwa miaka ya nyuma ilikuwa lazima wakupe jina lao hata kama lako lipo katika bible .
Na je ni haki bima ya afya kunichagulia wategemezi? Wakati mm ndo mchangiaji na nakatwa pesa yangu?
Ahsanteni.
Sent from my TECNO CF7 using
JamiiForums mobile app