Utaratibu unaotaka mtumishi wa umma kubaki na walau moja ya tatu ya mshahara wake, haukufanyiwa utafiti wa kutosha na utaratibu huu umepitwa na wakati

Kwa mujibu wa sheria na kwa kuzingatia waraka wa serikali wa March 19,2009( waraka namba: C/CE 45/271/01/01/87), mtumishi wa umma hapaswi kukatwa zaidi ya theluthi mbili ya mshahara wake.Kwa maneno mengine, anatakiwa kubaki na walau moja ya tatu ya mshahara wake baada ya makato yote ya kisheria pamoja na makato ya kulipia madeni (mikopo) aliyonayo.

Sina mashaka na lengo na madhumuni ya serikali kuweka utaratibu huu kwanini ni wazi ulikuwa na nia njema ya kumlinda mtumishi walau abaki na chochote mwisho wa mwezi baada ya mshahara kutoka.

Hata hivyo, binafsi naona utaratibu huu haukfanyiwa utafiti wa kutosha kwani una mapungufu mengi kuliko faida na sababu zangu nitazitoa hapa chini.

1. Umekuwa wa jumla mno

Utaratibu huu umekuwa wa jumla mno bila kuzingatia ukweli kuwa kuna utofauti mkubwa sana wa viwango vya mishahara wanavyopata wafanyakazi, na hivyo hakuna logic ya kusema kila mtumishi abaki na walau moja ya tatu ya mshahara wake baada ya makato yote( mikopo na makato mengine ya kisheria kama PAYE,n.k).

Kwa mfano, mtumishi mwenye mshara wa let say shilingi 960,000 kwa mwezi, moja ya tatu anayotakiwa kubaki nayo ni shilingi 320,000 kwa mwezi huku mwenye mshahara wa shilingi 1500, 000 kwa mwezi anatakiwa kubaki na shilingi 500,000 kwa mwezi.

Hapo ndio najiuliza kama inaaminika mtumishi X anaaweza ku-survive na take home ya 320,000 kwa mwezi, kwanini mtumishi Y alazimike kubaki na take home ya walau shilingi 500,000 ili hali gharama za maisha ni zile zile?

Tena tukumbuke hawa wenye mishahara mikubwa ndio wenye marupurupu mengi kiasi kwamba baadhi yao marupurpu yao yanazidi take home wanazopata kutegemeana na mwezi husika kasafiri mara ngapi au amekuwa na vikao vingapi, n.k.

Vile vile, hapa nimetoa mfano wa watumishi ambao take home zao zinatofautiana kwa shilingi 180, 000 ila ukweli tofauti iliyopo ni kubwa mno kwani kuna watumishi ambao mishahara yao ni milioni kadhaa(mbili na kuendelea) huku wengine hata milioni moja hawafiki ila wote wanabanwa na sheria moja(kama kuna tofauti tuelezani).

Hoja yangu hapa ni kuwa, kwanini hawa watumishi wenye mishahara mikubwa wasiruhusiwe kukopa zaidi badala ya kuwabana sawa na wale wenye mishahara midogo?Logic ya kuwabana na sheria moja iko wapi?

Katika hili, napendeleza badala ya kulazimisha kila mtumishi abaki na take home ya walau moja ya tatu ya mshara wake,tubadili sheria na utaratibu mtumishi alazimike kubaki na walau take home ya mshahara wa kima cha chini.

2. Kuingilia uhuru wa mtu kutumia mshahara wake

Binafsi naona utaratibu huu pia unaingilia uhuru wa mtu kutumia mshahara wake na zaidi unaweza kuwa ni mwanzo wa sheria zingine za aina hii huko mbeleni (unaweka precedence mbaya).

Kazi nifanyaje mimi alafu matumizi ya mshahara wangu unipangie huku shida, dharura na mahitaji yangi sio tu havikuhusu, bali huwezi kunisaidia kuzizatua.

3. Utaratibu huu utazamwe upya kuruhusu watu wakope mikopo ya muda mfupi
Kama nilivyosema mwanzoni,utaratibu huu umekuwa ni wa jumla mno bila kujali tofauti kubwa ya mishahara iliyopo na hivyo kuwabana hata wanaostahili.

Kwa mfano, mtumishi anaetakiwa kubaki na take home ya walau shilingi 500,000 au zaid kwanini asirihusiwe kutumia shilingi 100,000 au 200,000 kukopa mkopo wa muda mfupi na muda wa kati(kwa mfano miezi 6 mpaka 24) atataue matatizo yake mfano kumalizia ujenzi wa nyumba yake,n.k?

3. Serikali yenyewe kutuhumiwa kukiuka hii sheria
Nakumbuka kumekuwa na tuhuma kuwa makato ya Bodi ya Mikopo yanayofanywa na serikali, hayazingatii hii sheria bali wanaka tu hata kama makato yatazid theluthi mbili ya mshahara wa mtumishi.

Sasa tujiulize, kama madai haya yana ukweli, serikali inapata wapi uhalali wa kuwabana watumishi kwa kuwawekea ukomo wa kukopa katika mishahara yao ili hali yenyewe inatuhumiwa kufanya kinyume chake?

4.Sheria/utaratibu huu kwa sasa umebaki kuwa wa kinadharia tu

Ukweli ni kwamba, kutokana na kuongezeka kwa ugumu wa maisha na kuongezeka kwa vijitaasisi/taasisi za mikopo mitaani,hivi sasa watumishi wana mikopo mingi tu isiyoonekana katika salary slip zao na kufanya wanachokipokea mwisho wa mwezi kuwa ni chini ya moja ya tatu ya mishahara yao hivyo ni bora kuwapa uhuru wa kukopa watakavyo.

5.Serikali kutoongeza mishahara kwa miaka mitano sasa

Kitendo cha serikali kutoongeza mishahara ya wafanyakazi kwa miaka mitano sasa huku tukielelekea mwaka wa sita, kunaondoa dhana nzima ya serikali kutaka mtumishi wake anapata mshahara unaoweza kumsaidia kumudu gharama za maisha na badala yake unawafanya/ unawalazimisha watumishi kutafuta fedha kwa njia za ziada ikiwemo kuchukua mikopo mitaani.

6.Mikopo ya dharura kupitia financial institutions inayotolewa bila kujali hiyo moja ya tatu

Wakati sheria ya moja ya tatu inatumika kudhibiti makato haya,hali ni tofauti kwa baadhi ya taasisi za kifedha ambazo hutoa mikopo ya dharura ya hadi miezi 6 bila kujali hiyo moja ya tatu ambapo watumishi hukopa na kupeleka wenyewe marejesho kila mwezi huku baadh ya taasisi hizo zikiwa na riba kubwa tofauti na mabenki.

Kwa maana hiyo, sheria hii ya moja ya tatu inafanya kazi kwa baadhi ya taasisi huku taasisi zingine zikiwa na mwanya wa kukwepa huu utaratibu kwani mtumishi anapeleka mwenye kile anachodaiwa lila mwezi na tafsiri ya hali hii ni kuwa sheria hii inatumika zaidi katika mabenki kuliko katika taasisi nyingine za kifedha, hivyo kufanya hii sheria au huu utaratibu kuwepo kinadharia tu katika kuhakikisha mtumishi anabaki na walau moja ya tatu ya mshahara wake pale anapokuwa ana mkopo wa mwezi mmoja, miezi mitatu mpaka sita katika taasisi hizi ambazo hutoa mikopo midogo midogo na ya muda mfupi.

Kwahiyo, huu ni ushahidi mwingine kuwa sheria hii japo ipo, ila lengo limefeli na hivyo ni bora ikfanyiwa marekebisho ili kuruhusu watumishi kukopa mikopo ya muda mfupi katika mabenk hata kama moja ya tatu ya mshahara inayotakiwa kubaki itakuwa imegota.

7.Sio watumishi wote wanategemea mishahara

Wako watumishi wenye biashara zinazowaingizia kipato nje ya mshahara, hivyo mtumishi ataependa kutumia mshahara wake kukopa, aruhusiwe mradi tu atoe uthibitisho wa biashara katika benki anayoyaka kukopa kwa kutumia mshahara wake ikitokea mtumishi anataka kukopa kama mfanyanyakazi na si mfanyabiashara.

9.Serikali inajinyama/inajikosesha mapato

Ni wazi kuwa kadri mabenki na taasisi nyingine za kifedha zinapoongeza utoaji wa mikopo, ndivyo faida wanayopata kutokana na biashara hii inavyoongezeka na hivyo kulipa kodi nyingi zaidi serikalini na kwahiyo kuchangia katika kuiongezea mapato serikali.

10.Hoja kwamba watumishi watapunguza uwajibikaji/ufanisi na kujihusisha na ubadhirifu au ufisadi haina mashiko

Tunaelezwa kuwa moja ya sababu ya seeikali kuweka utaratibu huu ni kuhakikisha mtumishi habaki na zero take home au take home ndogo sana kwa hoja kwamba mtumishi wa aina hiyo anaweza kupunguza uwajibikaji na hata kujihusisha na njia haramu za kupata fedha akiwa kazini (wizi,ufisadi na ubadhirifu).

Hoja hii sidhani kama ina mashiko kwani mtumishi huyu anajua athari za vitendo hivyo ni pamoja na kufukuzwa kazi au kusimamoshwa kazi kitu kitachomfanya ashindwe kulipa mkopo wake na ukizingatia ukweli kuwa Bima ya mkopo haihusiana na mtumishi kufukuzwa kazi bali kifo au kupata ulemavu utakaomfanya ashindwe kuendelea kuwa kazini.

Isitoshe, si wafanyakazi wote wako katika nafasi za kufanya wizi au ufisadi wawapo kazini kwani wengi wako katika nafasi ambazo ama ni vigumu au haziwapi kabisa nafasi ya kuiba hela ya serikali au kujihusisha na rushwa.

Vile vile kama kweli hii ndio concern/hofu ya serikali, mbona haiboreshi masilahi ya wafanyakazi kwa mfano hii ya awamu ya tano iliyogoma kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa muda wa miaka zaidi ya mitano sasa?

Kwa maneno mengine, mishahara duni haiondoi morali ya kazi na kuchangia wizi na ufisadi sehemu za kazi kama hii ndio hoja ya serikali katika kutetea hiyo moja ya tatu ya mshahara wa mtumishi wa umma?

11.Utaratubu huu wa moja ya tatu unatumika pia katika sekta binafsi?

Kama utaratibu huu hautumiki katika sekta binafsi, basi hii ni sababu nyingine kuwa utaratibu huu haufai kuendelea kutumika kwa watumishi wa serikali unless serikali itoke sababu zs msingi na za kutushawishi kuwa utaratibu huu unapaswa kuendelea.

12.Nchi zote duniani zina utaratibu kama huu?

Tujiulize pia serikali zote duniani zina utaratibu kama huu ,na hata zile zenye utaratibu huu(kama zipo) utaratibu wao ni kama wetu au wao umeboreshwa zaidi?

Hivyo, kwa kuzingatia sababu hizo na zingine ambazo sikuzitaja au zinazoweza tolewa na wataopenda kuchangia mada hii, natalie wito kwa serikali kuwa wakati umefika wa sheria na utaratibu huu kufutwa au kutazama upya ili uendane na wakati na pia kuwapa nafasi zaidi watumishi kukopa kulingana na mishahara yao badala ya watumishi wote kubanwa na sheria moja ili hali kuna tofauti kubwa sana ya mishahara serikalini.

Kwa upande wa wapinzani, panaopo Tume Huru ya Uchaguzi, nawashauri mwaka 2025 katika Ilani yenu mje na ahadi ya kupitia upya utaratibu huu kwa lengo la kuufanyia mabadiliko mkilienga kuwapa watumishi uhuru zaid wa kupata mikopo.
Hii ni Akili ya bata kabisakwa sababu madhara ya mikopo kwa watumishi ni kuwa mafisadi na walarushwa pale wanapokuwa na mikopo mingi hivyo hiyo sheria ingeweka Nusu ½ ya mshahara siyo ⅔ yaani makato na mikopo isizidi nusu ya mshahara ,tofauti na mleta mada anavyo taka ......mfano mapolisi wanao katwa ⅔ ya makato kutokana na mikopo kazi yao kubwa ni rushwa ,ufisadi,kusumbua raia ili wapate pesa nje ya kutegemea mishahara.
 
Kwa mujibu wa sheria na kwa kuzingatia waraka wa serikali wa March 19,2009( waraka namba: C/CE 45/271/01/01/87), mtumishi wa umma hapaswi kukatwa zaidi ya theluthi mbili ya mshahara wake.Kwa maneno mengine, anatakiwa kubaki na walau moja ya tatu ya mshahara wake baada ya makato yote ya kisheria pamoja na makato ya kulipia madeni (mikopo) aliyonayo.

Sina mashaka na lengo na madhumuni ya serikali kuweka utaratibu huu kwanini ni wazi ulikuwa na nia njema ya kumlinda mtumishi walau abaki na chochote mwisho wa mwezi baada ya mshahara kutoka.

Hata hivyo, binafsi naona utaratibu huu haukfanyiwa utafiti wa kutosha kwani una mapungufu mengi kuliko faida na sababu zangu nitazitoa hapa chini.

1. Umekuwa wa jumla mno

Utaratibu huu umekuwa wa jumla mno bila kuzingatia ukweli kuwa kuna utofauti mkubwa sana wa viwango vya mishahara wanavyopata wafanyakazi, na hivyo hakuna logic ya kusema kila mtumishi abaki na walau moja ya tatu ya mshahara wake baada ya makato yote( mikopo na makato mengine ya kisheria kama PAYE,n.k).

Kwa mfano, mtumishi mwenye mshara wa let say shilingi 960,000 kwa mwezi, moja ya tatu anayotakiwa kubaki nayo ni shilingi 320,000 kwa mwezi huku mwenye mshahara wa shilingi 1500, 000 kwa mwezi anatakiwa kubaki na shilingi 500,000 kwa mwezi.

Hapo ndio najiuliza kama inaaminika mtumishi X anaaweza ku-survive na take home ya 320,000 kwa mwezi, kwanini mtumishi Y alazimike kubaki na take home ya walau shilingi 500,000 ili hali gharama za maisha ni zile zile?

Tena tukumbuke hawa wenye mishahara mikubwa ndio wenye marupurupu mengi kiasi kwamba baadhi yao marupurpu yao yanazidi take home wanazopata kutegemeana na mwezi husika kasafiri mara ngapi au amekuwa na vikao vingapi, n.k.

Vile vile, hapa nimetoa mfano wa watumishi ambao take home zao zinatofautiana kwa shilingi 180, 000 ila ukweli tofauti iliyopo ni kubwa mno kwani kuna watumishi ambao mishahara yao ni milioni kadhaa(mbili na kuendelea) huku wengine hata milioni moja hawafiki ila wote wanabanwa na sheria moja(kama kuna tofauti tuelezani).

Hoja yangu hapa ni kuwa, kwanini hawa watumishi wenye mishahara mikubwa wasiruhusiwe kukopa zaidi badala ya kuwabana sawa na wale wenye mishahara midogo?Logic ya kuwabana na sheria moja iko wapi?

Katika hili, napendeleza badala ya kulazimisha kila mtumishi abaki na take home ya walau moja ya tatu ya mshara wake,tubadili sheria na utaratibu mtumishi alazimike kubaki na walau take home ya mshahara wa kima cha chini.

2. Kuingilia uhuru wa mtu kutumia mshahara wake

Binafsi naona utaratibu huu pia unaingilia uhuru wa mtu kutumia mshahara wake na zaidi unaweza kuwa ni mwanzo wa sheria zingine za aina hii huko mbeleni (unaweka precedence mbaya).

Kazi nifanyaje mimi alafu matumizi ya mshahara wangu unipangie huku shida, dharura na mahitaji yangi sio tu havikuhusu, bali huwezi kunisaidia kuzizatua.

3. Utaratibu huu utazamwe upya kuruhusu watu wakope mikopo ya muda mfupi
Kama nilivyosema mwanzoni,utaratibu huu umekuwa ni wa jumla mno bila kujali tofauti kubwa ya mishahara iliyopo na hivyo kuwabana hata wanaostahili.

Kwa mfano, mtumishi anaetakiwa kubaki na take home ya walau shilingi 500,000 au zaid kwanini asirihusiwe kutumia shilingi 100,000 au 200,000 kukopa mkopo wa muda mfupi na muda wa kati(kwa mfano miezi 6 mpaka 24) atataue matatizo yake mfano kumalizia ujenzi wa nyumba yake,n.k?

3. Serikali yenyewe kutuhumiwa kukiuka hii sheria
Nakumbuka kumekuwa na tuhuma kuwa makato ya Bodi ya Mikopo yanayofanywa na serikali, hayazingatii hii sheria bali wanaka tu hata kama makato yatazid theluthi mbili ya mshahara wa mtumishi.

Sasa tujiulize, kama madai haya yana ukweli, serikali inapata wapi uhalali wa kuwabana watumishi kwa kuwawekea ukomo wa kukopa katika mishahara yao ili hali yenyewe inatuhumiwa kufanya kinyume chake?

4.Sheria/utaratibu huu kwa sasa umebaki kuwa wa kinadharia tu

Ukweli ni kwamba, kutokana na kuongezeka kwa ugumu wa maisha na kuongezeka kwa vijitaasisi/taasisi za mikopo mitaani,hivi sasa watumishi wana mikopo mingi tu isiyoonekana katika salary slip zao na kufanya wanachokipokea mwisho wa mwezi kuwa ni chini ya moja ya tatu ya mishahara yao hivyo ni bora kuwapa uhuru wa kukopa watakavyo.

5.Serikali kutoongeza mishahara kwa miaka mitano sasa

Kitendo cha serikali kutoongeza mishahara ya wafanyakazi kwa miaka mitano sasa huku tukielelekea mwaka wa sita, kunaondoa dhana nzima ya serikali kutaka mtumishi wake anapata mshahara unaoweza kumsaidia kumudu gharama za maisha na badala yake unawafanya/ unawalazimisha watumishi kutafuta fedha kwa njia za ziada ikiwemo kuchukua mikopo mitaani.

6.Mikopo ya dharura kupitia financial institutions inayotolewa bila kujali hiyo moja ya tatu

Wakati sheria ya moja ya tatu inatumika kudhibiti makato haya,hali ni tofauti kwa baadhi ya taasisi za kifedha ambazo hutoa mikopo ya dharura ya hadi miezi 6 bila kujali hiyo moja ya tatu ambapo watumishi hukopa na kupeleka wenyewe marejesho kila mwezi huku baadh ya taasisi hizo zikiwa na riba kubwa tofauti na mabenki.

Kwa maana hiyo, sheria hii ya moja ya tatu inafanya kazi kwa baadhi ya taasisi huku taasisi zingine zikiwa na mwanya wa kukwepa huu utaratibu kwani mtumishi anapeleka mwenye kile anachodaiwa lila mwezi na tafsiri ya hali hii ni kuwa sheria hii inatumika zaidi katika mabenki kuliko katika taasisi nyingine za kifedha, hivyo kufanya hii sheria au huu utaratibu kuwepo kinadharia tu katika kuhakikisha mtumishi anabaki na walau moja ya tatu ya mshahara wake pale anapokuwa ana mkopo wa mwezi mmoja, miezi mitatu mpaka sita katika taasisi hizi ambazo hutoa mikopo midogo midogo na ya muda mfupi.

Kwahiyo, huu ni ushahidi mwingine kuwa sheria hii japo ipo, ila lengo limefeli na hivyo ni bora ikfanyiwa marekebisho ili kuruhusu watumishi kukopa mikopo ya muda mfupi katika mabenk hata kama moja ya tatu ya mshahara inayotakiwa kubaki itakuwa imegota.

7.Sio watumishi wote wanategemea mishahara

Wako watumishi wenye biashara zinazowaingizia kipato nje ya mshahara, hivyo mtumishi ataependa kutumia mshahara wake kukopa, aruhusiwe mradi tu atoe uthibitisho wa biashara katika benki anayoyaka kukopa kwa kutumia mshahara wake ikitokea mtumishi anataka kukopa kama mfanyanyakazi na si mfanyabiashara.

9.Serikali inajinyama/inajikosesha mapato

Ni wazi kuwa kadri mabenki na taasisi nyingine za kifedha zinapoongeza utoaji wa mikopo, ndivyo faida wanayopata kutokana na biashara hii inavyoongezeka na hivyo kulipa kodi nyingi zaidi serikalini na kwahiyo kuchangia katika kuiongezea mapato serikali.

10.Hoja kwamba watumishi watapunguza uwajibikaji/ufanisi na kujihusisha na ubadhirifu au ufisadi haina mashiko

Tunaelezwa kuwa moja ya sababu ya seeikali kuweka utaratibu huu ni kuhakikisha mtumishi habaki na zero take home au take home ndogo sana kwa hoja kwamba mtumishi wa aina hiyo anaweza kupunguza uwajibikaji na hata kujihusisha na njia haramu za kupata fedha akiwa kazini (wizi,ufisadi na ubadhirifu).

Hoja hii sidhani kama ina mashiko kwani mtumishi huyu anajua athari za vitendo hivyo ni pamoja na kufukuzwa kazi au kusimamoshwa kazi kitu kitachomfanya ashindwe kulipa mkopo wake na ukizingatia ukweli kuwa Bima ya mkopo haihusiana na mtumishi kufukuzwa kazi bali kifo au kupata ulemavu utakaomfanya ashindwe kuendelea kuwa kazini.

Isitoshe, si wafanyakazi wote wako katika nafasi za kufanya wizi au ufisadi wawapo kazini kwani wengi wako katika nafasi ambazo ama ni vigumu au haziwapi kabisa nafasi ya kuiba hela ya serikali au kujihusisha na rushwa.

Vile vile kama kweli hii ndio concern/hofu ya serikali, mbona haiboreshi masilahi ya wafanyakazi kwa mfano hii ya awamu ya tano iliyogoma kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa muda wa miaka zaidi ya mitano sasa?

Kwa maneno mengine, mishahara duni haiondoi morali ya kazi na kuchangia wizi na ufisadi sehemu za kazi kama hii ndio hoja ya serikali katika kutetea hiyo moja ya tatu ya mshahara wa mtumishi wa umma?

11.Utaratubu huu wa moja ya tatu unatumika pia katika sekta binafsi?

Kama utaratibu huu hautumiki katika sekta binafsi, basi hii ni sababu nyingine kuwa utaratibu huu haufai kuendelea kutumika kwa watumishi wa serikali unless serikali itoke sababu zs msingi na za kutushawishi kuwa utaratibu huu unapaswa kuendelea.

12.Nchi zote duniani zina utaratibu kama huu?

Tujiulize pia serikali zote duniani zina utaratibu kama huu ,na hata zile zenye utaratibu huu(kama zipo) utaratibu wao ni kama wetu au wao umeboreshwa zaidi?

Hivyo, kwa kuzingatia sababu hizo na zingine ambazo sikuzitaja au zinazoweza tolewa na wataopenda kuchangia mada hii, natalie IGwito kwa serikali kuwa wakati umefika wa sheria na utaratibu huu kufutwa au kutazama upya ili uendane na wakati na pia kuwapa nafasi zaidi watumishi kukopa kulingana na mishahara yao badala ya watumishi wote kubanwa na sheria moja ili hali kuna tofauti kubwa sana ya mishahara serikalini.

Kwa upande wa wapinzani, panaopo Tume Huru ya Uchaguzi, nawashauri mwaka 2025 katika Ilani yenu mje na ahadi ya kupitia upya utaratibu huu kwa lengo la kuufanyia mabadiliko mkilienga kuwapa watumishi uhuru zaid wa kupata mikopo.
CC: mwigulu MCHEMBA
 
1/3 ni nzuri Sana tuliza kichwa, uliza watumishi hasa walimu watakupa experience zao kabla na baada ya huo utaratibu maisha yalikuwaje. Mwaka 2009 yupo mtu aliacha kazi kwasababu ya kubakiwa na mshahara wa elf 30 kwa mwezi, akaona ni kupoteza muda
 
Najua lengo lingine lilikuwa ni kuhakikisha mtumishi hajihusishi na ubadhiru pale atapokuwa na mshahara zero au kupokea mshahara mdogo sana mwisho wa mwezi.Je, unadhani hii sababu ni ya msingi?

Na kwa maelezo yako, unaamini mtu atakuwa hafiki kazini kwasababu mshahara wote ameukopea?Sheria na taratibu za kazi hazijui mpaka ahatarijshe Akira yake kiasi hicho?

Alafu ukifukuzwa kazi huo mkopo utaulipaje?
Itakuwa si mtumishi wa umma, na haujafanya utafiti wa kutosha kabla ya kuandika.
 
1/3 ni nzuri Sana tuliza kichwa, uliza watumishi hasa walimu watakupa experience zao kabla na baada ya huo utaratibu maisha yalikuwaje. Mwaka 2009 yupo mtu aliacha kazi kwasababu ya kubakiwa na mshahara wa elf 30 kwa mwezi, akaona ni kupoteza muda
Hatarii sana na alizokopaa zote kalaaa
 
Back
Top Bottom