Utaratibu mbovu wa upakiaji magari wa kampuni ya Kamanga ferry - Mwanza

Ilulu

Senior Member
Mar 22, 2008
161
31
Kama mtumiaji wa Kivuko cha Kamanga Ferry, kivuko kinachotoa hudumakati ya jiji la Mwanza na upande wa Sengerema katika ziwa Victoria. Napendakutoa dukuduku zangu juu ya utaratibu mbovu na ambao si wa kiusalama unaotumiwana mmiliki au wafanyakazi wa kampuni hii katika upakiaji wa magari kivukoni.

Magari yanatakiwa kuingia katikakivuko kinyume nyume kwa lugha nyingine kwa "reverse". Si madereva wote nimahodari sana inapofikia suala la kuendesha gari kinyume nyume. Kibaya zaidi,hakuna utaratibu nzuri wa kuyaruhusu magari kuingia katika kivuko na mara zote sualala kuingiza gari kivukoni ni suala la nani mjanjazaidi, nani hodari wa kuendesha gari kinyumenyume, na utayari wa kugombea nafasi ya kuingiza gari. Gari ya kwanza kufika nakuelekezwa na wafanyakazi wa kivuko wapi iegeshe haina uhakika wa kupakiwakatika kivuko isipokuwa tu kama dereva ni mjanja na yuko tayari kugombea na magarimengine mara kivuko kikifika. Hapa nina maanisha kuwa wa kwanza kupanga folenihana nafasi kabisa ya kuwa wa kwanza kupakia gari yake kivukoni kwani mara Pantoni ikifika ni suala la kugombea kupakia na si kwamba kuna utaratibu rasmiwa kuongoza kupakia magari kwa kadri yalivyopangwa au kuingia eneo la kivuko.Kutokana na kushindwa kuwa nautaratibu wa kuongoza magari kuingia kwenye kivuko na hasa ukizingatia magariyanaingia kinyume nyume, ajali ndogo ndogo ni jambo la kawaida wakati wakupakia magari.
Muda wa zoezi la kupakia magari linatumia muda mrefu kwaniwakati mwingine katika kugombea magari ujikuta yamefunga njia na kila derevaakibaki na msimamo wa kutoa ondoa gari lake kwani anafahamu wazi akitoa nafasibasi uhakika kwake ni mdogo.

Upande wangu, sioni kama tabia yammiliki au wafanyakazi kushindwa kuwa na utaratibu nzuri ni jambo la kufumbiamacho kwani lina madhara mtambuka, sisi wateja tunaharibu magari yetutunapolazimishwa kugombea kuingia kivukoni (tunagongana na gharama zinarudikwetu), kukosekana kwa lugha za staha katika mazingira hayo ya kugombea kuingiakivukoni na la msingi zaidi ni kuwa kuna hatari ya magari kutumbukia ziwanikatika hali hii ya kugombea kivuko.

Kwa nini wasiige taratibuzinazotumiwa na kivuko cha serikali cha Busisi/Kigongo katika kuruhusu magarikuingia kivukoni? Utaratibu unaomhakikishia mteja wa mwanzo kuwa pia ni kwanzakuingiza gari yake katika kivuko mara tu inapotolewa ruhusa ya kupakia gari kivukoni.

Ni ushauri wangu kwa Mmiliki wakivuko hiki kujaribu kwa haraka inavyowezekana kutegeneza utaratibu nzuri,rafiki na salama kwa watumiaji wa huduma ya kivuko hiki. Unaweza kuigautaratibu wa wenzako au kutengeneza wa kwako ili mradi uwe unaohakikisha hudumabora, rafiki na salama kwa mteja.

Kwa hali ilivyo sasa huduma bora,rafiki na salama
HAVIPO katika kampunihii. Kilichopo ni bora huduma!


Mlio karibu na Mmiliki auWafanyakazi wa KAMANGA FERRY naomba mnisaidie kufikisha ujumbe huu.


Ilulu

GEITA
 
Back
Top Bottom