nkundaruwa
Member
- Dec 3, 2011
- 28
- 2
Ndugu wanaJf, kwa muda mrefu nimekuwa nikisoma mada mbalimbali, lkn kuna lililonikwaza hadi nikaingia mazima.
Kama wiki mbili hivi zilizopita, Chama cha Mapinduzi kilifanya mikutano yake Dodoma. Baadhi ya Wajumbe wakaingiwa hofu ya kuvuliwa gamba hadi wakakusanya kundi la Vijana wa UVCCM; wakawalipia malazi na posho nyingine kadhaa ili waweze kuwasaidia kuweka shinikizo pale ambapo upepo utakuwa mbaya kwao.
Hofu inanipata kwamba, kama utaratibu hu wa kukusanya vijana hautadhibitiwa, itakapofika 2015, wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea wa Urais kupitia CCM, makundi mbalimbali yanaweza kuja Dodoma na Makundi ya Vijana kushinikiza fulani apite, fulani asiguswe.
Je Great thinkers, huko si ndiko kuchochea machafuko? Makundi haya ya Vijana si yanaweza kugeukana na Tz kikanuka?
Tutafakari.