Utapeli vipimo vya U.T.I na typhoids

MUSHEKY

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
2,812
Reaction score
2,768
Serikali kupitia waziri wake anayehusika na masula ya afya Dr ndugulile imewafumbua macho watanzania tanzania wengi wanaokwenda kwenye mahospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya U.T.I na homa za matumbo (typhod)

Inaelezwa kitaalam kwamba vipimo vya magonjwa haya huchukua muda wa masaa mawili (2) hadi sabini na mbili (72) ili kupata majibu yaliyo sahihi na sio vinginevyo

Taarifa hii imekuja kuwafumbua macho wananchi ambao kwa kiasi kikubwa tumekua "tunapigwa" kwa kupatiwa majibu ya maradhi haya sugu na hatari kwa muda usiozidi hata nusu saa!


Hali hii ikiachwa iendelee hivyo itapelekea watu wasio na maradhi kutumia dawa wakidhani wana maradhi (medicalization)

Au itawezakufanya watu walio na maradhi haya kutokupewa dawa zozote kwani huenda kwa muda huo mfupi maradhi hayataweza kudhihirika

Kwa maoni yangu serikali itupie macho pia mahospitali ya binafsi ambayo mengi yao si waaminifu kwani wengi hujisahau na kujikita zaidi kwenye biashara na si kutoa huduma

Imekua ni kawaida kila ukienda baadhi ya mahospitali haya ya binafsi ni lazima ukutwe na ugonjwa flani hasa U.T.I na malaria ili waweze kuuza na kumaliza stock zao za dawa walizojaza kwenye pharmacy zao

Pengine watakuambia macho yako yameharibika kabisa ili wakuuzie miwani kwa 150000/- , huu ni upigaji

Chanzo: gazeti la mtanzania
tar 19/5/2019
 
Utapeli wa typhoid ulianza yangu enzi za Mwinyi licha ya malalamiko ya watu kuuziwa dawa wasizozihitaji hakuna hatuna yoyote iliyochukuliwa, na hili litapita tu.
 
KWANINI WAKINYWA DAWA WANAPONA Kwa vipimo hivyohivyo? Muulizeni waziri swali hili!
maana AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO!!

Wakati mwingine si kweli kwamba tunakuwa wagonjwa, yawezekana ni uchovu pengine kupumzika tu au kunywa maji mengi ingetosha kuwa tiba. Lakini kwa sbb umeenda hospital hawawez kukuachq ukaenda bila kukupiga pesa ndio hapo watakubambikia magonjwa ambayo huna na kukupa dawa ambazo kiukweli haikuwa tiba yako. Pia na sisi wabongo huwa hatumwamini daktari tukiambiwa hakuna tatizo badala yake tutaendelea kuhangaika kwny mahospital mengine na ndio maana daktar anaona ni bora akudanganye unaumwa akupige mpunga( though ethically is not right)
 
Hivi kuna dawa ya malaria ya Sindano ambapo dozi yake ni Sindano tatu kuwa gharama ya 26000 kwa Kila Sindano jumla elfu 78000.Kuna dozi ya namna hiyo au ni kupigwa.Maana mgonjwa kaambiwa asitumie.dawa nyingine zaidi ya Sindano
 
Hivi kuna dawa ya malaria ya Sindano ambapo dozi yake ni Sindano tatu kuwa gharama ya 26000 kwa Kila Sindano jumla elfu 78000.Kuna dozi ya namna hiyo au ni kupigwa.Maana mgonjwa kaambiwa asitumie.dawa nyingine zaidi ya Sindano
ipo name nishawai tumia but bei sifahamu
 
Kw kweli serikali uiangalie sn hii sent a binafsi.ni kz ngumu sn kwenda kupimia na naambiwa huna ugonjwa.lkn pia dawa zina uzwa bei ya juu kweli kweli.prednisolen kuitwa the 100 kw tembe moja ni wizi mkubwa kbs.
 
Juzi juzi nilikuwa najisikia vibaya nikaenda kutibiwa hospitali moja ya Private Dodoma.Kufika pale nikafanyiwa vipimo nikaambiwa nina UTI.

Nikapewa mzigo wa madawa niliyanywa kama siku mbili nikaachana nayo.Kwa sababu kiukweli sikuwa na dalili zile kubwa kubwa za UTI.Nikamuonyesha majibu Kuna mshkaji mmoja anasoma medical lab alichoniambia duh! Acha niishie hapa
 
Kwakweli hospitali nyingi za watu binafsi na vituo vya Afya wamekuwa wafanyabiashara wa dawa na vipimo vyao.

Ni Wapigaji mno

Wizara ya afya iliangalie hili.
 

Idiot Embicile, majina huumba.... nakazia Idiot Embicile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…