Utapeli na dhuluma Himo wilaya ya Moshi

WatesiWETU

Senior Member
Jan 2, 2022
106
245
Wizara ya Ardhi, Takukuru, na Usalama wa taifa Fuatilieni Utapeli Unaofanywa Mkoa wa Kilimanjaro: Watu wengi wameshalizwa mamilion na ni mchongo wa watu wa Manispaa, viongozi wa wilaya na wakishirikiana na chama cha Ushirika cha mchongo hapo Himo(Lokolova).

Niende moja kwamoja kwenye issue yenyewe, Ni hivi katika wilaya ya Moshi, Kata ya Himo kuna maeneo ya Lotima na Riata, watu wame nyang'anywa na Ushirika ili hali yalikuwa ni ya watu binafsi wakilima tangu miaka ya 1970, ila huu ushirika unaojiita LOKOLOVA umejingiza kwenye mashamba haya mwaka 2001 ambayo ni ya watu binasfi kisha unaanza kuwalazimisha wayalipie ilihali yalikuwa chini ya watu binafsi na kulikuwa na mgogoro waki sheria kati ya wachaga na wapare kila upande ukiyagombania

Ikumbukwe miaka ya nyuma sana kabla ya uhuru wa Tanganyika kuliibuka vita za wapare na wachaga wakigombania maeneo na wachaga wakashinda na kuyamiliki mpaka hivi leo, ambapo miaka ya 2000 wapare walianza tena kuleta fujo za kuyataka na hivyo kupelekea kesi na kulikuwa na zuio la kimahaka(Court Injection) kuhusu kulima au kuyatumia mpaka hapo mgogoro utakapomalizika, cha ajabu hichi chama cha ghafla kikajitokeza kujidai kinawasaidia wamiliki kupambania haki zao hivyo kuwaandikiasha watu kama wanachama ili wafuatilie hiyo kesi.. lakini ghafla malengo yakabadilishwa na wahuni wakaanza kuwalipisha watu hela za kuwakatia viwanja, mara leo wanatoza hela za plot na kuwauzia watu mara ghafla kuwalipisha hela ya bicon,

Ajabu unaambiwa plot zitagaiwa kwa 60x60 unalipishwa hela kati ya laki6 kwa waliokuwa wanamiliki awali na kwa wale waliojitokeza kama wateja wapya eti wanalipishwa milioni na nusu

Waliojiandikisha wapo karibia watu 1500, eneno unalolipishwa hulijui, wanachama wameshatoa karibia milion na kila siku wanabuni jambo kuwaita na kuwachomoa hela, na hapo ile court Injection iliyowekwa mahakamani bado haijaamuliwa

Hili suala limekuwa ni mradi wa watu binafsi kwa kivuli cha ushirika, wanawadanganya wananchi kuwa ardhi ipo chini ya Ushirika.. wakati mashamba hayo ni mali ya wananchi chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ushirika haumiliki ardhi, ardhi ni mali ya Serekali na kama kuna miradi ya maendeleo basi kuna fidia kwa watu waliokuwa wanayamiliki maeneo hayo ili waachie

Sasa kinachoshangaza ulikuwa na miliki ekari 4 unanyang'anywa na ushirika unapewa plot ndogo ya squaremeter 600. na hiyo plot unilipia laki 6 na hapo hujui utakatiwa eneo gani maana hajaoneshwa eneo ila unalipishwa hela ya plot na Hela ya Bikon ili hali hujui utapewa wapi na kama hutapapenda hajulikani.

Ni ajabu sana hichi chama cha kilivyowahadaa wananchi na mpaka sasa wanawadanganya kuwa eti Ushirika ndio unapima na kuwagawia hadi watu ambao hawakuwa wanamiliki mashamba awali wameingizwa ilimradi wanalipia plot ya ardhi, Yaani chama kimetoka kwenye kuwasaidi wananchi kwenda kumiliki na kuwauzia wananchi ardhi yao.

Wananchi wengi hawana uwelewa ila baadhi wamekuwa wakilalamika na kufuatilia kwa muda wa miaka 10 mpaka sasa.

Takukuru na usalama wa taifa mfuatilie hii hujuma ya eneo la Lotima na Riata, hapo Himo, wilaya ya Moshi Vijijini. Hicho chama huenda kimesajiliwa kwa kazi nyingine ila kinachofanywa ni kazi nyingine na hadi account ya bank ipo wananchi wanalipa na kubaki na reciept miaka nenda rudi hakuna kuoneshwa au kugawiwa hizo plot wala mashamba.
 
Kilimanjaro ardhi ni ndogo sana,niko mkoa fulani huku kusini kuna eneo nimenunua ekari 4 kwa sh milioni moja ndani ya manispaa
 
Kilimanjaro ni mkoa wa pili kwa udogo baada ya dar es salaam

Ardhi pia kule ni scarce coz watu wa kule wanajielewa sana
 
Da Lotima nimekuliq hapo tulilima sana miaka ya 90 unavuna hadi gunia mia kwa jembe la mkono. Lotima Primary ndio nilianzia darasa la kwanza hadi la nne. Nitaenda kufuatilia hii
 
Da Lotima nimekuliq hapo tulilima sana miaka ya 90 unavuna hadi gunia mia kwa jembe la mkono. Lotima Primary ndio nilianzia darasa la kwanza hadi la nne. Nitaenda kufuatilia hii
Yaan ukipata majibu uje ahapa utoe mrejesho.. maana watu wanalia sana nimekuta malalamiko ya watu kutozwa hela miaka zadi ya kumi hawapewi viwnja zaidi ya kila siku mikutano na michango isiyo kwisha.
 
Back
Top Bottom