Utapeli mwingine Zain | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utapeli mwingine Zain

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by fiksiman, Jun 2, 2009.

 1. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Makampuni ni miongoni mwa biashara inayotengeneza faida kubwa na haramu kupindukia huku zikihusisha wizi wa moja kwa moja kutokana na huduma zinazotolewa kwa lazima au bila wateja kujua kuwa wanalipia. Pia promosheni mbalimbali zimekuwa kichocheo kikubwa cha kuwaibia wateja hasa wale wapenda njia ya mkato kuelekea utajiri. Sitaki kuzitaja huduma hizo kwani si agenda iliyonipelekea kuweka thread hii.

  Hivi karibuni kampuni ya simu za mkononi Zain imeanzisha huduma nyingine ya kitapeli kwa mtazamo wangu ili kuendeleza libeneke la wizi wa kimachomacho kwa wateja ambao wengi ni ignorant na namna makato yanavyofanywa. Huduma hiyo ambayo imepachikwa jina la Zap ambayo humuwezesha mteja kufanya manunuzi kupitia akaunti yake aliyoweka kwenye mtandao huo. Huduma kama kununua Luku, kujua balance yako kutoka akaunti yako ya benki na pamoja na kuhamisha pesa kutoka kwenye benki kwenda Zap ni mambo ambayo niliyaona mazuri na nikavaa mkenge wa kujiunga.

  Utapeli unaanzia hapa: Kwanza kwa kila huduma utakayotumia utakatwa pesa si chini ya 150 na kuendelea kulingana na aina ya huduma. Pia lazima simu yako iwe na credit iliuweze kutumia huduma hiyo, Huduma ya kuhamisha salio kutoka kwenye akaunti yako ya benk haifanyi kazi japo watakuta kila unapotumia. Kibaya zaidi walidai huduma zote zitafanywa na mawakala wao ambao hadi sasa hawajaanza kufanya kazi hivyo utalazimika kuzngumka mji mzima kutafuta wakala wa kuwekea pesa au kuchukua. Yote tisa kubwa ni kitendo cha kuwakata wateja hata kama hakuna huduma kwangu nahisi ni utapeli wa hali ya juu.

  Kama unataarifa zaidi tafadhali nijlishe ili watanzania wengine wasiuvae mkenge wa kutapeliwa kama wanavyofanya Zain na bila shaka kampuni zingine ziko njiani kuanzisha huduma hii isyo na maana.
   
 2. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,361
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Pole sana Kaka,
  Tatizo lako unaonekana kukata tamaa bila hata kujua unachokiongea kwanza amini hapa Duniani hakuna huduma ya bure hata ile tu ya Kiroho na Maombezi unatakiwa kulipa ( sadaka ) kama ambavyo unaambiwa na kulipa ! Nachukia sana watu wavivu ambao hafanyi tafiti lakini ndio wa kwanza kulalama !

  Sasa sikia mimi nina jamaa yangu anafanya kazi huko huko zain makao makuu Dar hata huku mkoani tunapata mambo ya Zap fresh tu itakuwa huko jikoni.......chukua namba hiyo 0786 670 371/ 2 wakusaidia wewe na wenzako ambao hawataki kufanya tafiti na kubaki kulalama tu....waulizie kile kitu kuanzia mawakala mpaka na namna ya kufanya hizo issues zingine !

  Pole sana na Karibu sana, Tabora !
   
 3. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45

  Hiyo si kazi yangu kuuliza walipo mawakala. Kama mmefanikiwa huko kwenu kila kheri lakini huku mjini tuna ATM kila mahali hivyo muda wa kufuatilia walipo mawakala bora niutumie kwenye kutafuta ATM. Ukisema huko kwenu mambo safi sitashangaa afteral mtalinganisha na huduma gani muhimu za kipesa zaidi ya hizo za ujanja ujanja. Kumbuka huku tunachoice ndo maana hatuibiwi kirahisi kama nyinyi....wasalimie wanyamwezi.
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
Loading...