Utapeli mpya, taasisi zinazohusika msaada tafadhali

Utapeli mpya, taasisi zinazohusika msaada tafadhali

Baba wa mbingu

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
496
Reaction score
1,184
  • Wana jamii juzi jumapili tarehe 28-09-2025, kuna dogo aliniambia kapata kazi ya kuwa tingo(tanboy) wa magari makubwa ya masafa marefu. Hivyo basi kuna mahali amekwama kiasi kidogo cha pesa nimsaidie ili akanunue ovaroli la rangi ya karoti lenye mistari ya reflector na kiasi alichopelea ni Tsh.25000/= kwani ovaroli linauzwa Tsh 45000/= .
  • Mimi nlimuuliza maswali machache,
  • Je? kazi uliipataje na ni kampuni gani?
  • YEYE: Ni rafiki yangu aliniunganisha na huyo dereva ila kampuni bado sijaijua.
  • MIMI: Overall nani amekwambia ununue na bei umejuaje kama ni hiyo au zaidi ya hapo
  • YEYE: Ni huyo dereva na nimempa laki kuna vitu kasema anaviweka sawa kama vibali na mambo mengine huko ofisini ili nianze kazi kesho tunaenda Dodoma, bado tu hilo overall
  • MIMI: aah! kumbe umeshaonana nae na umempa pesa yote hiyo vip usipopata kazi? na mshahara amekwambia bei gani?
  • YEYE: Mshahara kasema ni 3500k ila kula na kulala ni juu ya boss.
  • Mimi nikamwambia usimpe pesa tena adi uingie kazini kama kweli anania ya kukusaidia overoll haliwez kukunyima kazi na ujue ni kampuni gani usijetelekezwa njiani, ila hiyo pesa ntakupa asubuhi kabla hamjaondoka.
  • ASUBUHI AKANITAFUTA MIDA YA SAA 2 ASUBUHI AKISEMA BADO HAJAONANA NA JAMAA ILA KAMTUMIA MESEJI KUWA KAMPELEKA BOSI UWANJA WA NDEGE KISONGO SO YEYE AJIANDAE AKAMTUMIA NAMBA YA SIMU DOGO ALIPIE OVEROLL, Hapa nikaona huyu mdogo anatapeliwa kabisa so mapema sana nikashuka kwa mrombo soko la mahindi mizani pale kwani ndo ilikuwa sehemu yao ya makutano, baada ya kufika na nkamwambia janja usitume pesa mwambie aje na overoll pesa unayo uumpe ili muondoke. aseee kuanzia sa 2 asubuhi jamaa sijui alisanuka tumemuwekea mtego ili tumnase maana hakutokea kabisa alikuwa akimtishia tu Dogo mara me naonoka staki lawama ukikosa kazi, mara nimekopa ili kulipia overoll lAKO na pesa hutumi, mwisho kabsa akamblock dogo mpaka sasa.
 
🎵🎵🎵Kekundu, kekundu….
Hao ni matapeli kuwapata sio rahisi
 
Jobless tunapata shida sana, hata kidogo tulichonacho wanakichukua pia
ni hatari na janja anapiga vibarua vya ujenzi yaani ni mwendo wa zege, kupandisha tofali na kuchimba misingi yaania kalaani sana icho kitendo
 
Huu utapeli ni wa kitambo aisee bado upo hadi leo?
 
Back
Top Bottom