Tanzanian kid
Member
- Apr 1, 2025
- 98
- 143
Utapeli mitandaoni kupitia phishing link na jinsi unavyoweza kujilinda.
Siku hizi karibu kila kitu kiko mtandaoni kutoka kwa mitandao ya kijamii, benki, hadi mawasiliano ya kila siku. Lakini pamoja na hayo, kuna watu wanaotumia mtandao kwa ajili ya udanganyifu. Moja ya njia wanazotumia sana ni kutuma phishing link.
Phishing Link ni Nini?
Ni link ya bandia iliyotengenezwa na matapeli ili kudanganya watu wafungue na kuingiza taarifa zao binafsi kama vile:
●Neno la siri (password)
●Taarifa za akaunti ya benki au simu
●Namba ya kadi ya malipo
Mara nyingi link hizi hupeleka kwenye tovuti inayofanana sana na ya kweli, kama vile Facebook, Gmail au benki yako, lakini si halisi.
Jinsi ya Kutambua Phishing Link
1. Link ina mwandiko wa ajabu au makosa ya herufi
Mfano: badala ya facebook.com unaweza kuona faceb00k-login.net
2. Ujumbe unakutisha au kukulazimisha kuchukua hatua haraka
Kama vile: “Akaunti yako itafungwa leo, bonyeza hapa kuthibitisha”
3. Link inakupeleka sehemu ya kuingiza taarifa zako
Ikiwa link inafunguka na kukuambia uweke jina lako la kutumia au nenosiri, chunga sana.
4. Inatoka kwenye namba au email isiyojulikana
Wanaweza kujifanya benki au kampuni fulani, lakini kwa kutuma kutoka namba ya kawaida.
Jinsi ya Kujilinda
Usibofye link yoyote bila kuwa na uhakika nayo
Hata kama umetumiwa na rafiki, thibitisha kwanza.ikiwezekana mpigie simu kumuuliza, je ni sahihi au laa?
Weka usalama wa hatua mbili kwenye akaunti zako (two-step verification)
Hii inafanya isiwe rahisi kwa mtu kuingia kwenye akaunti yako.
Tumia programu au app ambazo zina uwezo wa kukukinga na tovuti feki
Simu nyingi za kisasa zina uwezo huu tayari.
Toa elimu kwa wengine
Watu wengi huathirika kwa sababu hawajui hatari hizi.