Utapeli K.N.C.U / Coffee Tree in - Moshi

Bayebe

Senior Member
Jan 31, 2014
152
198
Nilikuwa Safari ya Kikazi Mjini Moshi Tarehe 29-31, Dec, 2015. Muonekano wa Hotel na kuwa Centre ya mji vilinivutia, lakini kilicho ndani ya Hotel ni Wizi Unaoendana na Huduma Mbovu Kupindukia.

Chumba 30,000 /=, hakuna maji ndani ya vyumba , hakuna Television , Ceiling Fan Hazifanyi Kazi, Switch Socket Hazifanyi Kazi,

Niliongea na Baadhi ya Wahudumu na nikapitia vyumba vyote hali ni hiyo hiyo na kunieleza Uongozi umeshaelezwa lakini hawataki kubadilika.

Serikali / Ofisa Biashara Mjini Moshi Chukua Hatua Kutembelea Hotel Hiyo Kabla Jipu halijatumbuliwa.

Malalamiko ni mengi Mno..
 
Acha uongo
Ukweli ni upi sasa? Naeleza nilichokiona nimelala pale nimeyashuhudia hayo , Maji unapewa ndoo ukakinge Ghorofa ya chini , Ninyi ndo niloambiwa mnanufaika na Pesa chafu inayokusanywa hapo..
 
Ni kweli kabisa nimewahi kulala hapo, hii hotel iendane na wakati
Thanks Kwa Ushuhuda , Lengo ni kurekebisha Hotel ipo Eneo zuri sana ni rahisi kwenda Popote Moshi Mjini , Asbuhi na jioni Muonekano wa Mlima Kilimanjaro ni Safi Kabisa , Ila Huduma ni Wizi Mtupu
 
Hii ni dunia ya biashara huria,,,,ungeenda tu kwingine kwenye facilities hizo,mbona zipo nyingine nyingi tu!
 
Biashara Huria Haina Maana ya kuwa Holela, Imagine kila sehemu pangekuwa Hovyo kwa kigezo cha Huria Ungeishi vipi ? Tumia akili kufikiri
 
Atakuwa anatumia makalio kufikiria,kumbuka moshi ni mji wa kitalii c unaropoka hovyo mtoa mada kaangalia mbali ww lofa
 
Yasemwayo ni kweli kabisa!hotel inahitaji marekebisho makubwa sana.Kwa eneo iliyopo ingeweza kutengeneza faida nzuri sana
 
Hii Hotel nashangaa kwanini matajiri wa Moshi hakuna anayetaka kuichukua atie pesa yake pale...

Ina view nzuri sana ya Mount Kilimanjaro na mji mzima wa Moshi hasa pale Round About ya CRDB/NMB mpaka kule TTCL...

Marekebisho ni kwenye vyumba vya kulala tu... Chakula chao kiko poa sana alafu ni bei nzuri... Kila nikifika Moshi siachi kwenda hii Hotel, mpaka yule mzee aliyekuwa anaendesha ile lift miaka ya 2007-10 alikuwaga rafiki yangu sana..
 
Thanks Steph curry kwa nyongeza , Huwezi Panda Lift hadi awepo Controller Mfanyakazi wa humo , Button zake wanajua wao kuzi handle, Zaidi ya saa 3 usiku Controller anaondoka , na huduma ya Elevator/lift kwisha , kwa wale wapiga beer hapo Makumba bay mtapanda kwa kubebwa
 
T
Hii Hotel nashangaa kwanini matajiri wa Moshi hakuna anayetaka kuichukua atie pesa yake pale...

Ina view nzuri sana ya Mount Kilimanjaro na mji mzima wa Moshi hasa pale Round About ya CRDB/NMB mpaka kule TTCL...

Marekebisho ni kwenye vyumba vya kulala tu... Chakula chao kiko poa sana alafu ni bei nzuri... Kila nikifika Moshi siachi kwenda hii Hotel, mpaka yule mzee aliyekuwa anaendesha ile lift miaka ya 2007-10 alikuwaga rafiki yangu sana..
Thanks Steph, Hupandi Lift bila Kuwepo Controller wao , Button Zimechoka na wanajua namna wana vyozihandle, Controller ambao ni wahudumu mabinti wa humo wakiondoka Mteja imekula kwako , hasa kwa wale wapiga Vyombo /maji hapo Makumba bay mtapanda ngazi kwa kubebwa
 
Nilikuwa Safari ya Kikazi Mjini Moshi Tarehe 29-31, Dec, 2015. Muonekano wa Hotel na kuwa Centre ya mji vilinivutia, lakini kilicho ndani ya Hotel ni Wizi Unaoendana na Huduma Mbovu Kupindukia.

Chumba 30,000 /=, hakuna maji ndani ya vyumba , hakuna Television , Ceiling Fan Hazifanyi Kazi, Switch Socket Hazifanyi Kazi,

Niliongea na Baadhi ya Wahudumu na nikapitia vyumba vyote hali ni hiyo hiyo na kunieleza Uongozi umeshaelezwa lakini hawataki kubadilika.

Serikali / Ofisa Biashara Mjini Moshi Chukua Hatua Kutembelea Hotel Hiyo Kabla Jipu halijatumbuliwa.

Malalamiko ni mengi Mno..
Hivi ile ni hotel ya serikal? Manake ni chafu kweli yani inanuka? Watumbua majipu itabidi walitumbue tu.
 
T

Thanks Steph, Hupandi Lift bila Kuwepo Controller wao , Button Zimechoka na wanajua namna wana vyozihandle, Controller ambao ni wahudumu mabinti wa humo wakiondoka Mteja imekula kwako , hasa kwa wale wapiga Vyombo /maji hapo Makumba bay mtapanda ngazi kwa kubebwa
Tatizo ile Lift ni zile za zamani... Ni ngumu ku'operate ndio maana akawekwa mtu pale.... Tatizo hii KNCU ya sikuhizi imekosa viongozi wazuri, hakuna uwekezaji wowote wanaoufanya sikuhizi, makato ya wanachama sijui yanaendaga wapi... Zamani makato ya wanachama ndio yalileta maendeleo kule Uchaggani kama kujenga Barabara, madaraja, shule na hospitali hata kusomesha watoto ndani na nje ya nchi...

KNCU iliuliwa kabisa kisiasa kwa kuogopwa kwamba itaipiku serikali kwa kupeleka maendeleo.. Kama KNCU ingeachiwa nguvu zake na Mwl Nyerere (yeye ndiye alifanya fitna) ungekuta sasahivi hata Mji wa Moshi uko mara 10 mbele ya ulivyo sasa...
 
Hivi ile ni hotel ya serikal? Manake ni chafu kweli yani inanuka? Watumbua majipu itabidi walitumbue tu.
Lile jengo lilijengwa na KNCU (Chama cha Ushirika cha wakulima wa Kahawa)... Lina Office, maduka na hiyo Hotel...

Sijajua kama serikali walilitaifisha au bado linamilikiwa na KNCU, na kama bado linamilikiwa na KNCU sijui kwanini wameusahau huu mradi wao... Lile jengo linahitaji renovation kubwa tu ile lionekane la kisasa.. Sasahivi kuna majengo mengi makubwa ya kisasa yanajengwa pale Moshi.. Wakifanya utani hata hao wenye ofisi hapo na maduka watawakimbia... Waliupdate lile jengo na pia waweke parking ya kutosha na yenye usalama..
 
Waziri wa kilimo Mh. Mwigulu Jana tar. 6.01.2016 kavunja Bodi ya chama cha Ushirika Iringa ,kwa kuwatapeli wananchi , Issues za mikopo na ufujaji mali za umma
 
Acha uongo
Mtoa mada kanena ukweli mtupu..kuna siku niliingia Moshi saa saba usiku kwa vile kncu ipo karibu nikaona nijipumzishe tu ili asbh niendelee na safari..yaani nilijuta mbali ya anayosema mtoa mada lakini hata umeme mule ndani ya lile "gofu" ni wa mgao kwa vyumba.
 
NI kweli mtupu acheni ubishi wenu! pale kuna mijizi tu inakula fedha za chama na kuuza mali za chama kama za mama zao.
 
Hii Hotel nashangaa kwanini matajiri wa Moshi hakuna anayetaka kuichukua atie pesa yake pale...

Ina view nzuri sana ya Mount Kilimanjaro na mji mzima wa Moshi hasa pale Round About ya CRDB/NMB mpaka kule TTCL...

Marekebisho ni kwenye vyumba vya kulala tu... Chakula chao kiko poa sana alafu ni bei nzuri... Kila nikifika Moshi siachi kwenda hii Hotel, mpaka yule mzee aliyekuwa anaendesha ile lift miaka ya 2007-10 alikuwaga rafiki yangu sana..

Pale round about hakuna NMB mkuu, naamini ulitarajia kuandika NBC
 
Back
Top Bottom