New Nytemare
JF-Expert Member
- Dec 15, 2011
- 3,400
- 2,572
Kuna utapeli wasikuizi ni hatari.. Kama wiki mbili zilizopita katika gazeti la Mwananchi la tarehe 2 novemba niliona tangazo la chuo cha afya cha Eckernforde Tanga University kwa wito kwa wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa ngazi ya Diploma na cheti wakatoa na maelekezo jinsi ya kupata form katika internet na jinsi ya kuituma ila kabla uwe umeingiza pesa katika account yao ya CRDB...Kumbe wakati huo wametoa tangazo tayari chuo kilishakuwa kimepokea form na kimesha fanya selection na mwezi huu wa novemba waliochaguliwa ndo wanaripoti na mwisho na tarehe 15 novemba kuripoti,mie nina mdogo wangu ambaye baada ya kuona tangazo na vigezo wanavotaka anavo nikaona bora tu apply sasa majuzi katika kutaka kutuma form kwanjia ya fax nikaona ni vema kuwajulisha uongozi kwa njia ya simu kwamba natuma form kwa fax maana namba zao zilikuwepo kwenye tangazo ktk gazeti nikakutana na majibu haya "usijisumbue kutuma form kwani selection zilishatolewa kabla ya Novemba na kuripoti mwisho ni tarehe 15 yani kesho kutwa"
sasa najiuliza walitoa tangazo hili novemba 2 ili watulie pesa zetu 20,000/= na je wangapi wameliwa kama mimi..
tahadhari kwa wote
sasa najiuliza walitoa tangazo hili novemba 2 ili watulie pesa zetu 20,000/= na je wangapi wameliwa kama mimi..
tahadhari kwa wote