Muota Ndoto
Member
- Dec 4, 2007
- 89
- 128
Mpenda starehe za dunia hii hatimaye amelazimika kuiaga. Kama kawaida anafika lango kuu la mbinguni huku akiwa hajui hatma yake. Langoni kuna mlinzi na kama kawaida anapekua hati za kusafiria za Mpenda starehe.
Baada ya muda mfupi anamweleza: "Kuna makazi ya aina mbili, Peponi na Ahera. Utapewa muda wa siku mbili kukagua makazi yote mawili halafu utachagua. Baada ya uchaguzi hautaruhusiwa tena kubadili. Sasa sema utaanzia wapi".
Mpenda starehe akachagua kuanzia Ahera. Basi Mlinzi akiwa na mavazi yake meupe akamwongoza hadi lango la ahera. Akapokelewa kwa bashasha na mwangalizi wa ahera. Ni mtanashati na mwenye bashasha kuu. Akamtembeza Mpenda starehe maeneo yote ya ahera.
Kuna maeneo ya kucheza dansi za kila aina, zikiwepo za waenda uchi, kuna vinywaji vya kila aina, miziki ile aliyoipenda akiwa duniani, wadada wazuri wa kila aina, hoteli nzuri na kila aina ya starehe ambazo nyingine hajawahi kuziona. Vyote alipewa bila bure.
Kesho yake akaamka na ni siku ya kwenda kuangalia peponi nako kukoje. Akajikongoja kutokana na uchovu wa jana yake hadi lango la ahera ambapo alimkuta yule mlinzi wa mbinguni aliyemwongoza hadi lango la Peponi. Kufika, akapokelewa na mtunza peponi- pia amependeza na mavazi yake meupe.
Kama kawaida akamtembeza maeneo mbalimbali. Kuna utulivu, watu wanaimba nyimbo za slow na kusali, kuna kila aina ya vyakula na vinywaji ingawa sio sawa na ahera. Hakuna watembea uchi wala wadada poa. Kimsingi, Mpenda starehe aliboreka.
Akalala na kesho yake akapokelewa tena na Mlinzi wa lango la mbinguni. Akamwuuliza alikoamua kuishi. Haraka haraka Mpenda starehe akachagua ahera. Basi Mlinzi wa mbinguni akamwambia "haya njia ya ahera hiyo hapo na siruhusiwi kukusindikiza."
Kufika lango la ahera akakuta mambo yamebadilika. Mlinzi ni tofauti, ana mapembe, anatisha sana. Akamkaribisha. Mpenda stareke kwa mshtuko akasema: "nafikiri nimekosea njia, hapa hapakuwa hivi juzi nilipokuja".
Kwa kicheko cha dharau mtunza ahera akamwambia: "Jana tulikuwa kwenye KAMPENI. Unayoona ndio hali halisi ya ahera". Akamvuta akaingia nae gizani, motoni, na kila aina ya shida...