Utamu wa Penzi Changa

Utamu wa Penzi Changa

happiness win

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Posts
2,461
Reaction score
1,394
Penzi changa, (nikimaanisha mahusianao mapya) ni tamu sana. Kila mmoja anamfurahia mwenziwe na anaweza akajikuta anashindwa kujizuia hata kuelezea mambo yake ya ndani kabisa bila kujua hatari inayoweza kutokea hapo baadaye hasa kama hawa wawili watashindwana na kuachana au wataamua kuoana.

Katika kipindi hiki cha Penzi Changa jaribu kuwa mtulivu, acha uropokaji, acha kujieleza hadi kupitiliza, jifunze kuwa mdadisi ili kumfahamu mwenza wako vizuri raha ya penzi changa usikufanyie upofu utakaoujutia baadaye. Wengi katika mahusiano/ndoa hujuta kutokana na upofu wao katika kipindi cha penzi changa. Hebu tufundishane na kuonyeshana faida na hasara hata kwa mifano kulingana na topic yetu hii. KARIBUNI.
 
anza wewe mwenyewe kwanza, mie kama napenda napenda tu huwa sibadiliki badiliki bhana...
 
kama mtu ni katili ni katili tu and in real sense haina maana kukaaa na mtu nusu nusu eti unamweleza hiki mara kile usimwambie! Kuwa huru na nafsi yako maana kama atakutenda hata ukiyaficha kiasi gani when time comes in atakutenda tu!!!!
 
hahahah, bila kuropoka ropoka utamjuaje sasa? endeleeni kuropoka. halafu msijibanie bana huo wakati mlionao mnaweza msiupate tena! raha ya penzi changa ziacheni tu ziflow zenyewe. lol
 
Rahaaaa, sanaaa. Na sio kweli Kama utaweza kujizuwiaa Kama unapenda kweli, Kama unapenda jiachieee ufurahiye penzi usijidhulumu wala usimdhulumu mwenzio ambizaneni, mtajuaje nn kila mmojawapo anapendaa?
 
umeona eeeh! yaani huo ndio wakti mzuri haswaaa maana hujui huko mbele ya safari kama vitachacha.
 
Hakuna kitu kizuri kama penzi changa furaha kutoka moyoni haina haja ya kujificha kwani tunafahamiana nijifiche ila iweje sasa,
 
^^
Ni kama safari ya jua..asubuhi tamu mchana chungu jioni tamu tena (ila kwa wateule)
^^
 
Mapenzi yanakua taratibu yaani mwendo wa kinyonga....Sidhani kama ni muhimu kujieleza saaaana au kujisemea mengi saaana mwanzoni kwani mambo mengine yanajiseti kadri muda uendavyo. Unaweza kuropoka sana ukampeperusha ndege kwani bado hujajenga msingi imara....Ni muhimu kujenga msingi imara wa penzi ndipo uwe wazi zaidi kwa mpenzi. Waswahili wanasema MAPENZI UPOFU kama wako, wako hata aje mwenye kizizi na kama sio wako hata utumie kikombe cha babu utaishia kunawa kula huli.
 
nakuunga mikono na miguu yote,,,,,,,umemaliza kila kitu sio mwanzo wa penzi unahaditthia hadi babu yako alivyo mshirikina,mama yako anavyogawa uroda,ulivyo kicheche na blah blah nyingi zitampeperusha ndege automatically labda kama utajiachia kutoa yale mazuri mazuri ooooh
 
KWANI waweza kuishi na mwenzio hata miaka 10 lakini penzi likawa changa tu....
 
hbr ndo hyo wanaojianika mapema dawa yao ndogo!huo uchanga wa penz ndo wawatia wazm!hamkumbuk penz lilopta llkuaje?kwa upande wng,umexomeka
 
kwa kweli nadhani hapa duniani hakuna raha kama ile,ni kama unapaa, ni kama dunia iko kiganjani,ni hisia ambayo usingependa ifike ukomo...bahati mbaya sana huisha without even knowing.....nadhani hii ndio hutufanya baadhi yetu tuanze kuisaka tena regardless of our current relatoonship status,nadhani hisia hii ndio hutufanya tuwasaliti wenza wetu...ni hatari sana.
 
nakuunga mikono na miguu yote,,,,,,,umemaliza kila kitu sio mwanzo wa penzi unahaditthia hadi babu yako alivyo mshirikina,mama yako anavyogawa uroda,ulivyo kicheche na blah blah nyingi zitampeperusha ndege automatically labda kama utajiachia kutoa yale mazuri mazuri ooooh

Nashukuru kwa kunielewa...ndio hasaa maana yangu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom