Utamu wa katiba mpya, Wakenya tujifunze na yanayotendeka Zimbabwe

Km vile magu alivyo na uhakika wa 2020 tena hahahaha
 
Mfumo wa democrasia Africa,haukuwa muafaka sana,tulipaswa tawaliwa kiimla na tawala za kimila mfano wafalme,watemi nk,tungekuwa mbali sana.So katiba na democracy bila dhamira ya dhati haina tija.
 

Hehehe unaona unafiki wako ule, kuniwekea maneno ambayo sikusema ilmradi ushinde tu, huwezi kujadili mada bila kupindisha, kwako wewe ni ushindani tu uibuke mshindi, mara nyingi huwa inabidi unaachiwa uwanja.

Huyo game over huwa simjibu, kama wengine wengi humu, nimezoea kumwona akitoa bandiko fupi fupi za kubeza tu, sijaona siku anaamua kujadili, na pia sikumjibu kisa eti amepongezwa maana wanaompongeza ndio nyie wale wale. Pia huku hatupo kushindana, ila kuelezana na kujadili, ukianza ushindani unaachwa ujadili mwenyewe.

Narudia tena, na kama hutaelewa basi shauri yako, Game over ndiye alikua wa kwanza kusema katiba yetu haitufai na kwamba inawafaa watu wa Ulaya na RSA kisa sisi hatuchagui kwa kudadavua, nikamjibu ni jambo la kawaida hata kwa hao mabwana zetu aliowatolea mfano wa kama waliostaarabika, wengi wao huchagua kwa kutozingatia vigezo vyenye tija.
Hivyo hiyo sio sababu tosha ya kutufanya tutelekeze katiba nzuri hii inayotufaa na kututoa kimaisha.

La kuandika insha, nakumbuka kuna mara sio haba nimejibu insha zako, lakini huwa napuuza ukiandika andika tu ilmradi uone umeandika na umekua wa mwisho kusema wakati ukiishia kupindisha pindisha kinafiki na kiushindani, aya yako ya kwanza imetosha kujua unakoelekea na kuachwa utiririke mwenyewe.
 
Hivi kwanini unadhani kuna tofauti kubwa ya usalama, amani na umoja wa kitaifa kati ya Kenya na Tanzania?, huku Tanzania tangu kipindi cha Nyerere tumekuwa tukitofautiana bila kupigana, muhimu ni kusikiliza upande wa pili na kutoa maoni yako, hata kama hamkubaliani lakini tunasikilizana, Kenya ni tofauti sana, mtu yeyote anayetoa mawazo tofauti na yako anakuwa ni adui na anastahili kifo, kitendo alichofanyiwa Lisu kimestua nchi nzima huku kwetu, hadi huko kwenu kimesikika, lakini ninyi mnauana kila siku na kwenu bado ni sawa tu

Kitendo cha kukiri kwamba ulipanga kutomjibu gameover na wengine humu kwasababu tu unahisi wanayoandika hayakupendezi, ni muendelezo wa utamaduni wakenya kushindwa kuvumiliana na kukubali kukosolewa, leo hii Kenya inageuka kuwa kituko duniani, lakini bado umeshikilia katiba isiyokuwa na msaada wowote zaidi ya kuisifia kwamba ni nzuri, gameover alisema ukweli, hata Kenya ipewe katiba nzuri kiasi gani, kama akili zenu zitabaki kuwa primitive kiasi hiki, hakuna lolote litakalobadilika, ni sawa na kuwapa katiba nzuri wale wanyama kule Serengeti na ukategemea wanyama watabadilika
 
nice discussion...nimependa sana jinsi Game Over alivyojibu..nimefurahi pia jinsi MK254 alivofatilia.....naona ustaarabu wa hali ya juu...na pia kila alichokisema Game Over ni ukweli mtupu ingawa mchungu kumeza....yaani waafrika hatuna ustaarabu kabisa! yaani siasa zinafanywa miaka nenda miaka rudi ingali mtu hata hana chakula, karo au kazi...tumefika kiwango mtu haogopi hata kumtupia askari aliyejiami na bunduki mawe?? are you fuckin kidding me?? and you do this just because of a politician....its very sad.....mtu anafurahi sana kuamka mapema kwenda kufanya mchezo wa paka na panya na polisi huku wakirusha mawe na kupambana na vitoa machozi...mzungu hawezi kufanya upuuzi huu...Mbona? wazungu wamekomaa kiuchumi, kielimu na kisiasa...inabidi kwanza afrika tukomae kiuchumi na kielimu... tukishafanya hivo tutaona matunda ya katiba kama hii ila tukiwa na 40 percent unemployment na high illiteracy, bila shaka katiba hii nzuri hakuna mahali itakapotufikisha...fikiria nchi kama Tanzania, hii ni nchi ambayo haina uhuru au demokrasia tulio nao wakenya ila wanasonga sana kimaendeleo...inabidi wakati mwingine tumwachie tu raisi afanye atakachotaka ilimuradi tu aiendeleze nchi kisha tutakuja kupambana na demokrasia baadae...hivi sasa tunatia aibu sana jinsi Uhuruto na Odinga walivyokataa kuzungumza na kumaliza uhasama huu...kila mmoja ameipa masilahi yake kipaumbele...ingekuwa marekani au Ujerumani, aliyeshindwa katika uchaguzi angekuwa alishampongeza raisi mteule na kuendelea na maisha...ila hapa jamaa anataka afanye kila kitu ili Uhuru asipate urais tena kwa kususia maandamano kila kunapokucha, kususia bidhaa za kampuni flan na kupaa angani kwenda nchi za ng'ambo kuwashtaki Uhuruto...for what reason really? how does that help Kenya and Kenyans get wealthier or put food on their table? tourists and investors are keeping away...Game over you are right...we dont need democracy now...what we need is to enrich ourselves first then democracy will fall in place automatically....asante kwa majibu ya kistaarabu watanzania wenzangu..
 
Mada hii inagusa bara letu zima, hivyo sio rahisi mtu kuongea kishabiki maana haya mambo yapo kila nchi hapa africa.

Hata hivyo, mimi siku zote huwa siongei kishabiki, hasa ule ushabiki wa vyama vya siasa maana sipendi siasa! Ni vile tu tunajikuta tuna mitazamo tofauti kwenye mada za hapa hasa zile zinazogusa nchi zetu hizi mbili.

Kurudi kwenye mada, nikubaliane tu na wewe kuhusu upya wa hiyo katiba yenu! Moja ya maeneo ambayo huwa nawapongeza ni kwenye katiba. mlijitahidi sana hadi kuipata! Kwa hili hongereni sana!

Kikubwa tu ni kwa viongozi kuitii katiba hiyo, maana kwetu sisi wenye nywele ngumu hii nayo ni changamoto nyingine hasa pale ambapo mtu anaona katiba haiko upande wake.
 
Muambie huyo MK254 kwamba ni muhimu aanze kukubaliana na ukweli, na aachane na uzalendo usiokuwa na faida eti kwa sababu tu anashindana na Tanzania, tulipompongeza gameover kwasababu ya mchango wake mzuri, ambao kwakweli kwa mtu yeyote makini kamwe hawezi kuupinga kwa sababu yeyote ile, lakusikitisha na kushandaza MK254 akatukebehi wote tuliompongeza gameover akatuita watu wa CCM, je na wewe uliyesifia mchango wa gameover pia ni CCM?, sasa kama Kenya wananchi wenu waliowengi akili zao ni kama hizi za MK254, Kenya itakuwaje baada ya miaka kumi ijayo?, kiukweli kwa sasa hivi, hasa chini ya Magufuli, Kenya na nchi zingine za EAC zinabidi zijifunze mambo mengi sana toka Tanzania kama zinataka kupiga hatua za maendeleo, juzi Museven alikiri kwamba ataanza kuiga mambo anayofanya Magufuli, kwa hali ya Kenya ilivyo sasa hivi kiuchumi, kijamii na kisiasa, haipaswi kuendeleza ushindani usiokuwa na faida.
 

Asante, kwa kweli mimi hapa nimeshuhudia aina tofauti za uongozi Kenya, niliishi enzi ambazo hatukua na demokrasia, yaani kipindi kile kutaja jina la rais uliruhusiwa tu wakati unamsifia, hata kwenye klabu cha walevi pamoja na ulevi wote ilikua huwezi kutaja chochote cha kuhusu serikali, au rais.

Wakuu wa wilaya, machifu, viongozi wa mitaa na hata mapolisi walikua wanatunyanyasa, yaani nakumbuka kwetu kijijini ilikua kawaida kufikishiwa ujumbe kwako nyumbani eti chifu anashida nawe, ukamwone mara moja, na ukifika kwake anakuamrisha utoe kitita fulani cha hela maana serikali imekua ikifuata mienendo yako na wana taarifa kukuhusu na hurusiwi kuhoji ni taarifa zipi hizo maana serikali haihojiwi.

Rais akitangazwa kuja mjini kwetu, lazima tutoke wote mashuleni tukamlaki pembeni mwa barabara, maduka yote yalikua yanafungwa, biashara zinasimama, uchumi wa nchi ulikua umekwama, uzalishaji na ukuaji wa uchumi vilikua vitu vya kigeni kwetu. Ikulu ilikua inapiga simu na kuamrisha makampuni yachangie mamilioni ya hela, kamata kamata za mapolisi zilikua mambo ya kawaida, walikua wanazunguka kitaa na kukusananya vijana bila makosa yoyote, tunaswekwa kwenye kaladinga za polisi kiholela.

Haiwezekani hata kidogo nikawaza kurudi huko hata siku moja, tumepiga hatua, tumesonga, tupo mbali sana kila nikiangalia nyuma naona umbali wa tulikotoka, naweza nikaandika mengi sana ya tuliyopitia enzi hizo. Nilikua mmoja wa waliopokea vibano vya polisi ili tufikie hapa tulipo.

Nakiri hatujafika, safari bado mbali, hatua za kukamilisha bado ni nyingi lakini taratibu tunasonga, changamoto zipo, kuna viongozi ambao waliishi kwa mazoea ya zamani bado wanapitia hali ngumu ya kuzoea huu mfumo mpya. Damu bado inamwagika, mabomu ya machozi bado yanarindima mjini, makelele na mikimbio kila siku, lakini tutafika na nina uhakika watoto wetu ipo siku wataishi kwa raha sana, lakini kwa sasa tutapambana hadi kieleweke maana nimeona matunda ya katiba nzuri, niemonja hayo matunda na kama walivyosema wataalam wa maisha mchovya asali hachovi mara moja.
 
Sasa hapo unaanza kueleweka, wewe ulikotoka umeteseka sana, kwasababu mlikuwa chini ya uongozi katili wa Jommo Kenyatta na mzee Moi, sasa hii katiba mpya kwako wewe ni sawa na kipofu kuona punda, kwake kila kitu hakiwezi kuzidi punda kwa ukubwa

Sisi huku kwetu ni kinyume chake, tulilelewa kwa kudekezwa na mwalimu Nyerere, hakuna hata mtu mmoja aliyeguswa na polisi au kunyanyaswa na kiongozi yeyote wa serikali, tuliishi maisha ya umoja, amani na kupendana, maisha ya ujamaa yalijali sana uhuru na haki za binadamu, kwahiyo kama tunakuambia kwamba bado katiba mliyopata haijaleta matokea chanya, tunalinganisha na tulivyokuwa huko nyuma chini ya Nyerere, tunajua nini maana ya kuwa huru, hatulinganishi na kipindi hiki cha Magufuli ambaye ameanza kukandamiza uhuru, japo katiba ni ileile ya Nyerere, muhimu sio katiba pekee, muhimu zaidi ni utashi wa watu, hasa viongozi kuitekeleza katiba kwa vitendo, kama alivyofanya Nyerere
 
Hueleweki ndugu. Huwezi kutenganisha siasa, uchumi na maendeleo. Hii dhana kuwa tuache siasa tufanye maendeleo ni dhana ya kidikteta inayolenga kuwafungia milango wapinzani wasihoji maamuzi ya kipuuzi ya watawala.
 
Hueleweki ndugu. Huwezi kutenganisha siasa, uchumi na maendeleo. Hii dhana kuwa tuache siasa tufanye maendeleo ni dhana ya kidikteta inayolenga kuwafungia milango wapinzani wasihoji maamuzi ya kipuuzi ya watawala.

Ni wachache watakuelewa, ninachojua ni kwamba bila makelele ya upinzani na vyombo vya habari hapa kwetu Kenya tungekua tumeliwa na kuuzwa mazima mazima. Wanahoji na kuzingua kila siku hadi serikali inakaa mkao wa kuogopa ogopa.

Watu wengi hawaelewi kwamba Waafrika wa leo sio wale wa zamani waliokua wanazugushwa zungushwa bila kuhoji chochote. Hata Watanzania wa leo ni tofauti sana na walioishi kwenye hiyo nchi enzi zile, hata CCM iliponea chupu chupu kwenye uchaguzi uliopita, Magufuli aliishia kujinadi kwamba ni yeye anasaka kura na sio CCM, ukiangalia asilimia walioshinda nayo ndio kidogo kuwahi kutokea. Watanzania wa leo wanahoji balaa, uwafunge jela au hata kuwapiga risasi bado wanahoji.

Masuala kama ndege ya Tanzania iliyokamatwa hayangejadiliwa yanavyojadiliwa leo, nilicheka sana juzi kutazama video dada Kawawa anajibu maswali hadi jazba inamuingia na kuwaacha wanahabari.

Ndio taswira Afrika yote, vizazi vya Waafrika wa sasa ni tofauti sana, sio wale waliokua wananyanyaswa enzi zile. Na viongozi wa sasa wasiotambua hilo wanajikuta katika hali aliyojikuta Mugabe juzi. Ameishia kushangaa na kutokuelewa nini kimemtendekea, hicho kilichomkuta kilisukwa lini, na wapi na nani na kivipi hadi hakuna aliyemtonya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…