DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 302
Kijana yangu mmoja ambaye sasa ni mwalimu wa chuo fulani maarufu kaja akaniambia kaka haya maisha sio kabisa, labda amerogwa. Akasema alikuwa anachat whatsapp na marafiki zake aliomaliza nao degree miaka 8 iliyopita, mmoja wa hao marafiki alikuwa anawajulisha wenzake kuwa ameomba kazi mahali na anategemea kufanya interview siku kadhaa baadae kwahiyo alikuwa anaomba baraka zao, sasa katika maongezi ikaonekana mshahara anaoenda kudai huko si chini ya milioni 8, huko alipo kwa sasa anapokea milioni 5, wengine wakasema hiyo hela ya kawaida sana.
Sasa yeye tangu amalize degree alibahatika kubaki kama tutorial assistant(TA) kwenye chuo hicho baada ya kuonekana amefaulu kwa kiwango cha first class, tangu abaki hapo amekuwa akisota na kusoma kila siku ili apande ngazi mbali mbali ili aufikie uprofessor. Kwenye udadisi wake amegundua Full Professor mshahara wake wa juu kabisa kwa sasa hauzidi millioni 5. Na ili yeye afike ngazi hiyo inabidi asote kwelikweli mpaka nywele zibadilike rangi ndio apate hiyo hela ambayo wenzake aliomaliza nao wanaofanya kazi sehemu zingine wanapata zaidi ya kiasi hicho kwa sasa pamoja na allowance zingine za kutosha.
Huko nyuma alishawishika kwamba ukiwa mwalimu wa chuo kuna mambo mengi utafanya au kushirikishwa kama projects mbalimbali au consultancy mbalimbali kitu ambacho anasema sio vile ilivyo kama vile watu wengi wanavyofikiria. Hata wenzake ambao wamemtangulia hawana maendeleo ya maana, ni kama watu waliokata tamaa.
Zamani kuna wazee tulikuwa tunawaona ambao ni walimu wa vyuo mambo yao yalikuwa ni mazuri sana. Kwahiyo yeye alikuwa na ndoto za kufanya vizuri sana darasani ili awe kama wao, lakini anaona imekuwa kinyume chake.
Sasa anaona kuwa mwalimu wa chuo atasota sana kuileta familia yake maendeleo. Mfano wenzake wamepeleka watoto wao kwenye shule nzuri za private wanapata elimu nzuri yeye uwezo huo hana kabisa hata ndoto hazipo. Sasa yeye bahati yake miaka hiyo aliweza kuungaunga akafanya vizuri, watoto wake atawasaidia vipi kufika huko kwa kipato anachopata!.
Sasa ni kwamba kijana ana bahati mbaya au ndio maisha ya walimu wa vyuo yalivyo miaka hii?