Utamfahamu vipi mke mwema?

Utamfahamu vipi mke mwema?

Ngoja nikae chonjo nipate sifa za mke mwema, nimuibukie humu humu ninayemzimikia kila siku
Soma Mithali 31: 10-30

10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
 
Mke mwema ni huyo uliyenaye,huwezi ukampata mwingine yeyote.
 
kumekuwa na mkangayiko mkubwa sana juu ya kumtafuta ama kumpata mke mwema je! utamtambuaje!?

Hii ni mada nzuri sana hasa kwa sisi wa kizazi hiki. Natumaini aliyeuliza na wanachangia wana maana halisi ya kutaka kuelewa na si mizaha mizaha kama ilivyozoeleka humu mpaka JF inadharaulika.

Well, ni kweli Jibu la msingi linapatikana katika mithali 31:10 na kuendelea. Lakini nadhani kinachokosekana ni TAFSIRI, yaani UFAFANUZI wa hiyo mistari.

Na ninaomba niseme tafsiri si moja. Ya kwangu iko hivi:-

Tuanze na mwanamke aliye tayari kwenye ndoa ambaye ni mke mwema.

Kwa kifupi kabisa mwanamke huyo ni yule ambaye mara baada ya kuolewa, agenda zake binafsi zote zinakufa. Yaani hobby zake, na chochote kinakufa. Badala yake anafuata na kudumisha hobby za mume wake. Hashindani na mumewe kwa kauli, majibishano, ugomvi, nk. Yeye ni mtu wa Ndiyo = 95% na HAPANA 5% NA hata namna anavyokataa anatumia hekima sana asimdhalilishe mumewe.

anamsaidia mumewe mambo mbali mbali na furaha yake ni kuona mumewe anafanikiwa, mumewe anang'aa, mumewe anasifika kwa majirani, na katika jamii. Hajiwekei mali za kificho i.e. viwanja, maduka, nyumba, n.k. Kila alichonancho ni cha mumewe, na kila cha mumewe ni chake.

Anatambua madhaifu ya mumewe na anamsitiri mumewe katika hayo. si mbea, wala hatangazi habari za mumewe kwa majirani wala marafiki zake. Haijalishi mumewe ana mapungufu gani lakini yeye atasema mazuri tu juu ya mumewe.

Ajenda zake ni mbili tu: kumtumikia mumewe na watoto. Halalamiki juu ya mumewe kutokufanya kama yeye maana anajua wajibu wa mumewe ni 95% kumtumia Mungu +jamii na 5% iliyobaki ni kwa mke na watoto. Hivyo hawezi kutafuta usawa na mumewe. anaelewa kuna tofauti. Mume ni kiongozi, yeye ni mfuasi. Mume ni mbeba maono, yeye ni mtekelezaji.

huyo ni mke aliye katika ndoa.

Sasa kazi kwenu kung'amua binti asiyeolewa mwenye sifa hizo.
 
Wanawake wa hivo kwa kizazi hiki wanatafutwa kwa kurunzi
 
Wanawake wa hivo kwa kizazi hiki wanatafutwa kwa kurunzi

Amini usiamini wapo mkuu. Ila lazima utulie kuwapata. Hawajitangazi. sikatai kuwapata ni kazi kweli kweli maana kama neno linavyosema. thamani yao inapita vito vyote vya thamani unavyovijua wewe.

Ila "clue" mojawapo, mdadisi binti habari za wazazi wake. Kama mama yake ana hizi sifa, basi kuna uwezekano mkubwa wa yeye pia kuwa na hizi sifa.
 
Nmekupata boss
 
nukuuu ya "Martin Luther"
oa/owa m2 ambaye unadhani huwezi ishi bila ya yy, na sio m2 unadhani unaweza kuishi naye
 
Tafuta uzi wangu nmeuliza .. "Nani mke mwema kwako ?".

Then itakupa mwanga....n.b kutoka kwangu
 
Mkuu umeuliza swali zuri sana

Ngoja Leo nifunguke

Mke mwema ni yule unayeendana naye swali unaendanaje naye

Kwa kawaida mwanamke anatakiwa akamilishe yaliyopungua kwako

Maana yake wewe unajielewa upungufu wako kuumbuka mke ana k..ma na mwanaume ana mb....l.

Hivi vikiingiliana vinatengeneza ukamilifu moja SHIMO moja kimetokeza mbele

Hata kitabia tunapaswa tuwe interlock mfano mpole amuoe mkali wataendana ila wakali kwa wakali wakioana ugomvi ukitokea hapakaliki

Wapole nao wakioana nakuambia watoto watakaozaliwa watakuwa mazuzu

Huo ni mfano tu mkuu sasa ni kuangalia sifa zipi zimepungua endapo ukimpata mtu mtamechi na maisha yataenda mbele

Kumbuka no one is perfect kwa hiyo yajadili mapungufu yakekama utayaweza.

Kila LA kheri mkuu
 
Back
Top Bottom