Utambuzi Binafsi silaha ya Kwanza

Utambuzi Binafsi silaha ya Kwanza

Joined
Jul 26, 2015
Posts
49
Reaction score
30
Habari Wakuu,

Nakumbuka enzi hizo za utafutaji wa ajira kama tulivyo wengi humu jukwaani.

Kiukweli haikuwa rahisi kupata kazi,Sehemu nyingine ambazo nilibahatika kupata walau kujishkiza Maslahi yalikuwa duni kuliko maelezo.

Kuna sehemu nilikuwa katika matazamio kwa muda wa miezi mitatu,Pasi na kupewa shilingi kumi,Ila nilipambana kwa kutegemea hisani za maswahiba ofisin hapo.

Jambo nalomshukuru Mungu ni kwamba,Mara tu baada ya kukubali kuteseka kwa miezi hyo mitatu!

Ilikuwa rahisi kupata kazi kutokana na sehemu hiyo.Kwani kupitia marafiki tuliokuwa pamoja walipopata mchongo wa kazi hawakusita kunistua.

Kwa sasa nilipo naweza sema,Changamoto na mateso niliyopitia Leo yamekuwa silaha.

Kwani nina uzoefu wa kutosha katika kazi nifanyayo sasa.
Japo kipindi kile sikulipwa na nilidharaulika mtaani kwa kupendeza halafu mizinga ikawa mingi kwa Masela na wadau.

Cha muhimu ni kujitambua binafsi,Kwani maneno ni mengi kwa familia na hta marafiki wanaotuzunguka.

Kama utapata kazi yeyote ya halali,Itumie kujiimarisha kwa kuhakikisha walau Unaongeza ujuzi juu ya kile ulichonacho.

Kozi ndogo ndogo kama za lugha,Computer na hata udereva si za kudharau kabisa.

Mwisho ni kumtegemea Muumba kwa mujibu wa Imani ya kila mmoja.


Siku zote atafutae Hachoki.

Naamini kwa kuandika,lipo utakalopata

Kalamu na Karatasi

(Chanzo cha Maarifa)
 
Mkuu silaha binafsi ya kwanza ni ipi?
Naomba kueleweshwa Tafadhali!..
 
Back
Top Bottom