Utamaduni wa kuvishana pete

Mwakani mwanzoni Mungu akituweka hai naomba mnikumbushe nihitaji msaada wa mwongozo wenu katika hili suala la pete na engagement kwa ujumla wake tafadhali.
 
NaUnGa mKoNo hOjA....[emoji30][emoji30][emoji30]
Hata mimi naunga haja kubwa mkono...

Yaani wavalishane pete au minyororo watajua wenyewe... ila tu huu ukuda wa mwanaume kumpigia goti mwanamke kwangu mimi sioni tofauti yake na ushoga.

Hii mitamthilia itatuharibia vijana wetu wallah. Wameanza kuiga hii ya kupigiana magoti soon wataiga ya kubanjuana wao kwa wao.

Ndio, nimeandika mimi babu yao ODM original
 
zote mbwembwe tu umvalishe pete au usimvalishe kama sio muaminifu sio kikubwa uaminifu na uvumilivu nyingine mbwembwe tu nimewha shuhudia binti kavalishwa pete jion then usiku kaenda kumegwa na ex boy wake hii dunia tunapenda sana kuiga
 
Mwakani mwanzoni Mungu akituweka hai naomba mnikumbushe nihitaji msaada wa mwongozo wenu katika hili suala la pete na engagement kwa ujumla wake tafadhali.

Basi sawaaaa..... usijali
 
Kwa utaratibu wa Kikristo haswa waliookoka. Ukipata mchumba unamwambia Mchungaji wako.. Mchungaji anakupa baraka zake ndo unapeleka barua ya posa. Barua inajibiwa, unapeleka Mahali, Siku ya mahali ni mahali tu.

Ukimaliza hapo unarudi kwa mchungaji na hapo sasa ndo utatangaza uchumba kanisani kwako na kanisani kwa mwanamke. Siku ya kutangaza uchumba ndo siku ya kuvisha pete. Baada ya hapo mnabandikwa kanisani kote(Tangazo) kwamba nyie ni wachumba. Kwasasa nipo hapo na mimi huko mbele sijui ila ndoa yangu ni mwakani.

Sasa kwenye style ya kuvisha pete ni nyie tu maamuzi yenu. Mimi binafsi nilipiga goti wakati navisha pete. Niligoogle sana na kuuliza sana kwama je kupiga goti ni sana nikaona ni sawa tu maana goti lenyewe moja tu.. ni ishara ya unyenyekevu. Afu nimejichanga kwenye kibubu miaka 2 nimemnunulia mchumba wangu pete nzuri ya Gold k yenye Tanzanite stone amefurahi sana.

Nkaona wanapendaga kunyenyekewa basi nkajishusha nkapiga goti moja nkamvisha pete yake nzuri kabisa alifurahi sana sana. Kama kupiga goti ni ubwege basi mzee baba nlipiga ili tu afurahi.
 
Mimi sielewi tu, mtu unamvalisha pete mwanamke kwa misingi ipi haswa wakati unajuwa kabisa atakusaliti ama utamsiliti yeye.
 
Utamaduni wetu toja enzi, ukivutiwa na msichana kwanza unawashirikisha wazazi, badae unaenda kujitambulisha kwao binti, binti akikukubalia unatoa posa, unachukua binti unaingia kwake anakuwa mkeo....
habari kwisha
Haya mambo ya kuvishana Pete na kunyonyana mate a.k.a kubadilishana uchafu/bakteria ni tamaduni chafu zilizoingizwa na wazungu kwenye hizi dini za kimamboleo.
 
Mwakani mwanzoni Mungu akituweka hai naomba mnikumbushe nihitaji msaada wa mwongozo wenu katika hili suala la pete na engagement kwa ujumla wake tafadhali.
Usijali kuhusu hilo mkuu, tuko pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…