Utamaduni wa kuvishana pete

storyteller

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2014
Posts
1,544
Reaction score
1,874
Nawasalimu wote MMU

Huwa najiuliza huu utamaduni wa kuvalishana pete hapa kwetu Tanzania.

Je, mwanaume anatakiwa amvalishe pete mwanamke siku ya kuomba uchumba, au siku akishakubalika nyumbani kwa mwanamke?

Kwa uelewa wangu, naamini makubaliano kati ya mwanamke na mwanaume yanatakiwa kufanyika na kuvalishana pete kunaweza kuwa kwa namna yoyote (siri ama mbele ya kadamnsasi).

Sasa naomba kueleweshwa, kwa wale wazoefu walio katika ndoa, ama walioingia katika ndoa na kutoka. Utaratibu uliopo(ambao wengi wanaufanya) ni kuvalishana pete siku ya kupeleka mahari(ama wakishapeleka mahari wanapanga siku ya kuvalishana pete), je uko sahihi, ama wanatakiwa kuvalishana kwanza ndipo mahari ipelekwe?

Na pili, suala la mwanaume kupiga goti wakati wa kuvalishana pete, je ni utaratibu sahihi hasa kwa mila na desturi za kiafrika, tujadiliane.

wasalaam.
 
Naona pete ivalishwe siku ya kupeleka mahari au kama mtaandaa siku ingine fresh kikubwa mahari ya watu ushatoa hapo unajihakikishia naam ni mchumba wangu napaswa kuweka uthibitisho kidoleni.


Kupiga goti kwa mwanaume ni ishara ya kuomba na wala sio utumwa na pia sio lazima ni wewe tu upendavyo.

Ni lazima uombe tena kwa unyenyekevu sababu unapoomba kuna kukataliwa pia, imagine umeandaa surprise watu kama wote mwisho wa siku bibie anasema " I'm not ready".... tumeshajionea sio mageni.
 
Inapendeza kuvalishwa siku ya kutoa Mahari lakini inategemea na mapendekezo ya wahusika wenyewe.
 
Ni lazima uombe tena kwa unyenyekevu sababu unapoomba kuna kukataliwa pia, imagine umeandaa surprise watu kama wote mwisho wa siku bibie anasema " I'm not ready".... tumeshajionea sio mageni.
Hayupo mwanamke wa karne hii wa kukataa kuchumbiwa sababu hajapigiwa goti. Si sahihi kumpigia goti mwanamke, kumbuka wewe (mwanaume) ni mamlaka kamili toka kuumbwa kwa ulimwengu.
 
Pete huvishwa mbele ya kadamnasi ili kuanza kujiwekea kinga ili kuzuia wanyakuzi dhidi ya yule uliyemchagua ktk wengi. Pia si lazima mhusika avishwe baada ya kutoa mahari. Na mwanaume kumpigia goti mwanamke wakat wa kumvika pete ni ishara ya heshima kuwa umemfanya awe km dunia jinsi ilivyo beba kila kitu ukionacho hapa ardhini, hivyo ni heshima ya hali ya juu sana.
 

Kwa utaratibu wa mila na desturi, kuna kabila linapiga goti kwa mwanamke???
 

Mkuu kwani ukiamua kumpeleka mchumba wako beach kisha ukamvika hiyo pete kimya kimya, hapo utakuwa hujajihakikisha kwamba ni wako. na utakosa kinga?
 
Hayupo mwanamke wa karne hii wa kukataa kuchumbiwa sababu hajapigiwa goti. Si sahihi kumpigia goti mwanamke, kumbuka wewe (mwanaume) ni mamlaka kamili toka kuumbwa kwa ulimwengu.

Wenyewe huwa hawataki kusikia kwamba "imeandikwa" wanadai tukisema hivyo ni mfumo kandamizi.... binafsi naamini kumpigia mwanamke goti ni kujifedhehesha.
 
MI NADHANI NI SAWA MKUU MAADAMU MHUSIKA AMEONA NI SAWA KWA UPANDE WAKE
Afu vitu vingine sio lazima kujiuliza saaaaaana ni vitu personal

Unaposema vitu persona ina maana hujali kama unakosea ama lah...... mfano, kupiga punyeto ni kitu personal, lakini kujitapa mbele ya wanaume wenzako unapiga puchu ni kujifedhehesha. kuna vitu huwa ni minor sana lakini tunahitaji japo kujifunza toka kwa wengine ili tufanye maamuzi ya busara... au unasemaje.
 
Mkuu kwani ukiamua kumpeleka mchumba wako beach kisha ukamvika hiyo pete kimya kimya, hapo utakuwa hujajihakikisha kwamba ni wako. na utakosa kinga?
Mkuu, kumvisha mbele ya umati hata km atatamani kufanya mambo yake km usaliti hatokuwa huru kwa kuwa uliwaambia kadamnasi kuwa yeye ni wako, tofaut na kumvika pind ukiwa peke yako
 
Ni katabia tu kachafu tumeiga kwa wazungu. Utampigiaje magoti mwanamke? Zipo namna nyingi za kuonesha upendo lkn hiyo hapana. Mamlaka uliyopewa na Mungu unaiinamisha mbele za msaidizi wako, halafu kesho akikukaripia unakimbilia hapa kuanzisha mada ukiomba ushauri ambao hata hivyo hautaufuata maana tayari unatawaliwa na mkeo.

Haya mambo mengine spiritually yana madhara lkn kuiga kunatuponza.
 
Wengi huwa wanafanya engagement party baada ya mahari kutolewa au wengine huvalishwa siku hiyo hiyo ya kutoa mahari kuhusu kupiga goti ni mapenzi tu ya mwanaume hasa umkute gentleman mwenye mahaba kama yote anakutreat adi unajihisi duchess...
 
Ningekua Mimi ndo nimepigiwa goti,,hadi tendo la ndoa angenipigia goti,,daadeki


Yani kila anachoomba apige goti. Mana kumbe kuomba ni mpaka upige goti😱😱😱
 
Hayupo mwanamke wa karne hii wa kukataa kuchumbiwa sababu hajapigiwa goti. Si sahihi kumpigia goti mwanamke, kumbuka wewe (mwanaume) ni mamlaka kamili toka kuumbwa kwa ulimwengu.

kwanza sijasema mwanamke atakataa/amekataa kuvishwa pete kisa HAJAPIGIWA GOTI, nimesema kupiga goti sio lazima lakini ni ishara ya KUOMBA kwa unyenyekevu, the whole process kuanzia barua, mahari mpaka ndoa ni mwanaume anaomba, ndio maana huwaendea wazazi kwa heshima na unyenyekevu (hapo nimekujibu uliposema mwanaume kapewa mamlaka tangu kuumbwa kwa ulimwengu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…