Utamaduni wa kusoma/kujisomea

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
UTAMADUNI WA KUSOMA/KUJISOMEA

Siku chache zilizopita nilikuwa na kasafari ka kwenda mkoani morogoro kwenye basi nililopanda mimi mwenyewe ndio nilikuwa na gazeti la kusoma nakumbuka nilikuwa nasoma gazeti la mwanahalisi , kwenye basi hakukuwa na mtu aliyeshika kitabu cha kusoma wala gazeti wala jarida lolote sembuse yule ambaye anasikiliza radio za nyumbani kusikiliza yanayojiri .

Nyakazi za asubuhi zile wakati wa mchaka mchaka wa makazini na mashuleni ingia kwenye daladala uone wanafunzi ukiona ameshika kitu cha kusoma basi ujue ana mtihani baadaye ana kariri cha kwenda kujibu kwenye mtihani huo kama hakuna mtihani utafikiri hata sio mwanafunzi hata shuleni anachelewa kwa dakika chache .

Ukipita vyuoni napo ndio utashangaa zaidi ukienda kwenye internet café angalia history ya search ujue wanafunzi walikuwa wana search nini au kuangalia aina ya tovuti walizokuwa wanatembelea utashangaa na kustaajabu mfano wa UDSM samahani kwa sasa hakuna huduma ya internet café kwa miezi 2 sasa ila ni asilimia chini ya 10 ya wanafunzi wanaotembelea tovuti hiyo kwa siku kwa ajili ya kazi za kila siku hapo vyuoni .

Ukitembelea stationary zao kuangalia kwa mfano kinachoandikwa utashangaa mfano watu 20 wameandika jibu moja kwenye swali waliloulizwa si inaonekana kwenye print out pale tofauti ni majina ya wanafunzi tu ingawa hii zaidi inatokea kwenye taarifa za field

Hii ni tofauti sana na Nairobi au mombasa ambapo huwa naenda mara kwa mara kule watu wanapenda kusoma kuanzia wanafunzi mpaka wafanyakazi pamoja wadau wengine wa masuala ya nchi yao .

Hata unapoingia kwa mfano kwenye forum za nchi jirani utaona na kuamini watu wengi wanapenda kusoma na kuandika tofauti ya nyumbani kwetu kwa mbali kidogo nimeona hili kwa sababu nimetunga riwaya kadhaa zimesomwa sana na watu wa huko mpaka sasa hivi naendelea kuandaa fupi fupi .

Naona zifanyike jitihada za dhati kabisa kuamsha utamaduni wa kusoma kwa watanzania wote hii ni pamoja na wadau wa kuandika na utunzi kukaa pamoja kufanya utafiti na kujua kitu hichi kifanywaje ili hali iwe nzuri .

Mfano kwa mimi nimegundua wengi wanapenda vitu vifupi fupi ila ukimwandikia mwanamke wa kikuyu kitu kifupi ataomba uendelezee kuandika mpaka umalizie yote uliyotaka kusema .
 
And all the magic is in the books and reading! What a sad story!!!
 
IF TOU WANT TO HIDE ANYTHING FROM AFRICAN, PUT IT IN THE BOOK,
habari ndo hiyo, we have to change
 
Nafikiri kwanza inabidi waandishi wa vitabu wawepo, na kufanyika marketing kubwa ili ku-change population behaviour zao...waandishi wengi wamekata tamaa kwasababu kazi zao hazuuziki..cheap habari inauzika zaidi
Tatizo ni kubwa zaidi kwa wafanyakazi wa serikali kusoma report tu issue ndio maana wana underperfom sana..of course we have long way to go ku-build hiyo culture...
Nyumbani watoto ni Ze-comedy and the like hakuna vitabu vya maana vinavyochangamsha fikra na akili za watoto....na hakuna anayetilia umuhimu...
 
Ulikuwa unasoma mwanahalisi.....basi lazima waswahili
waku azime na wao wasome....
Dawa yao ni kushika gazeti la daily news tu....
Utasoma peke yako kwenye basi.....
 
Back
Top Bottom