Utamaduni wa kurejesha mahari marufuku Uganda

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,888
Mahakama ya juu zaidi nchini Uganda imesema kuwa utamaduni wa kurejesha mahari baadaya talaka katika ndoa za kitamaduni unakiuka katiba na utamaduni huo unapaswa kupigwa marufuku.


Uamuzi huo wa majaji saba katika mahakama hiyo umetolewa baada ya wanaharakati wa haki za wanawake kuwasilisha kesi mahakamani wakisiema kuwa utamaduni huo unawanyima wanawake haki zao.


Jaji mkuu wa Uganda Bart Magunda Katureebe amesema kuwa ikiwa utamaduni huo utaruhusiwa kuendelea itakuwa na maana kuwa wanawake ni kama bidhaa zinazouzwa sokoni.
150806084509_uganda_ngombe_304x171_bbc_nocredit.jpg

Ngombe hutumiwa sana kulipa mahari Uganda


Lakini idadi kubwa ya majaji hao walikubaliana na uamuzi kwamba utamaduni wa utoaji mahari unapaswa kuendelea na kwamba haukiuki katiba.


Hata hivyo mmoja wa majaji hao alisema kuwa utamaduni huo unawadhalilisha wanawake na kwamba mahakama inapaswa kulifanya swala la ulipaji mahari kuwa chaguo na wala sio sharti.


Chanzo: BBC
 
majaji viazi hawa,eti kudai mahari kunawafanya wawe bidhaa,kwanini wasikatae kwanza mahari?inawezekana hapo kuna conflict of interest yaan majaj wana watoto wa kike,lakin wangeacha mila zibak km zlvyo
 
Back
Top Bottom