Utamaduni hazina - ukihamia Bukoba utakutana na hii hapa


Sema Alpum mkuu, siyo Album.
 

Mkuu umenifurahisha hapo kwenye Moses reels. Faiza Foxy au Ally Kombo hawezi kujua hii kitu.
 
style ya unywaji pombe ndiyo utamaduni unaoelezewa kibuyu na mrija. Kama mavazi zote ni nguo kihifadhi mwili ila tofauti ni mishono na materials za nguo, wengine ngozi, vitambaa nk.
Kumbe kunywa pombe nayo ni utamaduni
 


Kukiwa na mende ndani ya kibuyu utamwonaje kama si kummeza pamoja na pombe na kushtukia tu mikwaruzo anapopita shingoni?

kwa wale wazee waliobobea na watumiaji wazuri mrija husukwa kwa vitu maalum kwa chini ili kuchuja uchafu wowote kama "enkanja" na vinginevyo visivutwe wakati wa kunywa, na hicho kitu kiachosukwa huitwa ENCHENCHO.
 


Wazee wa Kihaya wakipata pombe aina ya Olubisi ikiwa katika Ekilele (Kibuyu) huku wakifyonza kwa kutumia Olusheke (Mrija - straw).​

Basi hasikwambie mtu hiyo kilele huwa inatunzwa kama mboni ya jicho. Kwa mfano huyo mzee aliyekaa upande wa kulia hiyo kilele yake ukimuuliza anaweza akwambie anayo miaka 25 iliyopita. Basi nikiwa secondary nilipewa na baba nitangulie nayo nyumbani wakati naenda nikateleza nikaanguka kikavunjika! Nilipigwa kuliko dr Ulimboka alivyopigiwa na msangi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…