Utalii wa ndani

Utalii wa ndani

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
38,082
Reaction score
57,737
Wikiendi hii natamani nikatembelee kijiji chochote chenye mandhari mazuri ya kiujamaa. Lengo ni kupumzisha akili na mwili kwa kuona vitu vya asili asili.

Kama kwenye hicho kijiji kutakuwa na pombe za kienyeji na ni salama kwa watumiaji itakuwa vizuri sana. Muhimu ni kufurahi kwa kula vitu vya asili, vinywaji vya asili pamoja na kuburudika kwa kuona mazingira ya asili.

Itapendeza kama nyumba za wageni zitakuwa zime ezekwa kwa nyasi, na vitanda vikiwa vya miti au vyenye badala ya godoro.

Kwa hiyo wakuu, nipeni majina au wekeni picha za hivyo vijiji vyenye hizo sifa niende nikale maisha, hii ni sehemu ya utalii wa ndani.​
 
Back
Top Bottom