Utalii Wa Ndani Kwa Bei Nafuu

FOEL

Senior Member
Jan 19, 2012
141
34
Wakuu nimeanzisha thread hii ili watu tujulishane ni kwa kiasi gani tunaweza kutembelea vivutio vyetu vya ndani vya utalii kwa bei nafuu au bei affordable, kwa mfano kama sehemu watu wanaweza ku drive badala ya kupanda ndege au badala ya watu kulala ndani ya vivutio basi walale kwenye hoteli zilizo nje ya vivutio kwa kuwa huwa zinakuwa za bei ya chini kidogo na hakuna gharama za park fee.

Hapa nataka tupeane options na ikiwezekana na gharama zake japo kwa makadilio tu, na ikiwezekana, travel agent wa kuwaona, mabasi gani ya kupanda na hotel gani za kufikia.

Hii iwe kama USHAURI WA SAFARI ZA NDANI

Hapa tuzungumzie maeneo kama;-

1. Zanzibar
2. Pemba
3. Mafia
4. Bagamoyo
5. Tanga
6. Mikumi
7. Serengeti
8. Selous
9. Manyara
10. Ngorongoro

E.t.c
 
Unataka ushauri wa kuanzisha bishara ya utalii wa ndani au wewe mteja unaulizia package za bei nafuu?
 
Unataka ushauri wa kuanzisha bishara ya utalii wa ndani au wewe mteja unaulizia package za bei nafuu?

Nimegundua watu wengi tunashindwa kutembelea vivutio vyetu vya ndani kwa kuwa na uelewa mdogo, wa ni vipi tutavifikia vivutio hivyo na gharama zake.

Sasa hapa nimeanzisha hii thread kwa sababu hiyo, ili walio na uelewa wa gharama na jinsi ya kufikia vivutio vya utalii watujulishe na sisi wengine.

Ni hayo tu.
 
Safi sana hii, ngoja tusubiri wataalamu wa utalii wa ndani, lakini hapa ungejumuisha na cultural tourism.
 
Nilipata kwenda Mafia last year na ilikuwa kama ifuatavyo:-

1. Kama inavyojulikana hiki ni kisiwa na hakuna boat inayokwenda kula zaidi ya ndege, kama uko dar garama ya ndege ni dollar 140 return ticket.
2. Vyumba vya bei poa ni dollar 35 na vizuri, na hotel, lodges, beach resorts nyingi ziko south of Mafia, Utete.
3. Vitu vya kufanya kule zaidi ya kuogelea kwenye beach za Kanga zilizo north ya Mafia, unaweza kwenda fishing, kufanya diving na snorkeling.
4. Hakuna migahawa mingi kwa hiyo mara zote chakula utakula hotelini kwako, na fee ya Marine Park kwa kuwa takribani nusu ya Mafia ni Marine Park ni sh 2,000 tu kwa sisi wabongo, wageni 20 USD.

Its a beautiful place, kuko kimya and virgin.

Nitakupeni bagamoyo na Znz muda kidogo.
 
Bagamoyo: Kama unatokea Dar unaweza kwenda ukavinjari kwenye vivutio vya kitalii na kurudi Dar. Nauli ni shilingi 1500/= kwa kichwa. Kama utapenda kulala vyumba vizuri vinaanzia 30,0000/=. Utatembelea maeneo ya kihistoria na beaches kama vile Kaole, Caravan Serai, Ngome Kongwe, Mji Mkongwe, Makumbusho ya Kanisa Katolic n.k. Karibu sana.
 
Mkuu asante kwa info, na je hakuna vivutio vingine vya baharini, kama diving na snorkeling na kuogelea na je gharama zake zikoje kama vitu hivi vipo huko Bagamoyo
 
Nilienda mikumi ilikua mwezi wa kumi mwaka jana nilikuwa na gari ndogo saloon lakini niliweza kwenda nayo mpaka ndani ya mbuga na kujionea wanyama na vivutio vingine kama sunset mida ya jioni kiingilio ni elfu 15 kama sikosei kwa gari na abilia wake, na baada ya hapo nilenda kulala mji mdogo wa mikumi ambapo pia kuna snake park. gharama ya kulala mji mdogo wa mikumi ni Tsh elfu 25 VETA hotel na kesho yake nikaludi dar. it was good
 
mkuu FAKE ID

nina eneo katika mpaka wa hifadhi ya taifa mikumi ipatayo eka nne, inakufaa kuwekeza campsites au Resorts kwa ajili ya idea yako hii, it is up for sale or Joint Venture

contact me for more info
 
Nimegundua watu wengi tunashindwa kutembelea vivutio vyetu vya ndani kwa kuwa na uelewa mdogo, wa ni vipi tutavifikia vivutio hivyo na gharama zake.

Sasa hapa nimeanzisha hii thread kwa sababu hiyo, ili walio na uelewa wa gharama na jinsi ya kufikia vivutio vya utalii watujulishe na sisi wengine.

Ni hayo tu.

Mkuu nakubaliana na idea yako. Pamoja kupata bei na kujua wapi pa kwenda kutalii, naamini hii ni fruksa nzuri ya kibiashara ya kupeleka watanzania kutalii. Kama uko kwenye hii fani tunaweza kutengeneza network ya wafanya bishara ya utalii na tubalishane idea mbili tatu.
 
Mkuu asante sana kwa mchango wako,

Hapa tunajaribu kupata ufahamu wa sehemu za vivutio vya kwenda, jinsi ya kwenda na gharama zake kwa unafuu.

Nadhani ni wakati mufaka kwa utalii wa ndani kuwa experienced na watu wengi zaidi.

Kwa hiyo kama unaufahamu tujulishe mkuu.
 
Huu uzi ni wa muda mrefu lkn kama ulidorora hivi.
Humu hakuna watu walioko kwenye makampuni ya kusafirisha watalii watujuze gharama za kukodi magari na mambo mengineyo?
 
Back
Top Bottom