Utalii wa Ndani (domestic tourism) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utalii wa Ndani (domestic tourism)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PauliMasao, Sep 9, 2008.

 1. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wana JF, haya ni makala katika gazeti laTanzania Daima la Septemba 9, 2008 kuhusu Utalii wa ndani na chanzo cha mapato nchini na Amana Nyembo


  HIFADHI za Taifa (TANAPA) ni Shirika la Umma lililokabidhiwa dhamana ya kusimamia na kulinda maeneo yaliyotengwa na serikali kama hifadhi ya taifa kwa manufaa ya kikazi kilichopo na kijacho.

  Mpaka sasa kuna hifadhi 15 zenye wanyama, milima na ndege wa aina mbalimbali wanaopatikana huko, hali inayofanya kuleta kivutio kikubwa kwa watalii.

  Kutokana na hifadhi hizo, uchumi wa nchi hukua kutokana na fedha zinazopatikana katika hifadhi zilizopo nchini, lakini licha ya kuongeza kipato, pia hutoa burudani kwa watalii wanaotembelea hifadhi hizo.

  Baadhi ya Watanzania wana tabia iliyozoeleka kuwa wageni kutoka nje ya nchi, ndio wanaopaswa kutembelea hifadhi za wanyama na kuangalia kumbukumbu mbalimbali.

  Hivi karibuni Daktari Mkuu wa wanyamapori kutoka Hifadhi za Taifa (TANAPA), Titus Mlengeya, alipokuwa akizungumza na Tanzania Daima hivi karibuni, anaeleza kwamba Watanzania hawana uelewa wa vitu na faida inayopatikana endapo watatembelea hifadhi ya taifa.

  Mlengeya, anasema mfumo huo wa Watanzania kutotembelea hifadhi za wanyama ulijijenga tangu awali, serikali ilipotenga maeneo ya maalumu ya hifadhi kwani haikuwashirikisha wananchi.

  Anasema, wananchi wabadilike na wawe na nia ya kutembelea hifadhi mbalimbali za wanyamapori, kwani licha ya kuburudika na kupata mafunzo lakini pia utalii ni chanzo cha mapato katika kuongeza uchumi wa nchi.

  Akielezea zaidi, anasema kuna umuhimu wa wananchi kuwa watalii katika nchi yao ili waweze kujua tabia mbalimbali za wanyamapori ambao wengine tabia zao hufanana na zile za kibinadamu.

  “Unajua watu hawajui tabia za wanyama kwa sababu hawatembelei hifadhi, wanyama kama sokwe, huweka matanga, ikitokea katika familia kuna mmoja amefariki…sasa kitu kama hicho Watanzania wengi hawajui,” anasema.

  Mlengeya, anasema changamoto iliyopo kwa Watanzania lazima wawe wadau muhimu wa utalii, kwani wanapotembelea sehemu hizo hujifunza tabia mbalimbali za wanyama na kujua aina na tofauti zake.

  “Jamii iachane na tabia ya kupita na basi maeneo ya Hifadhi ya Mikumi pindi wanaposafiri halafu ikitokea wameona wanyama kama simba njiani, wao hufikiri wameshafanya utalii, wakati utalii hauendi hivyo,” anasema.

  Anasema pesa inayopatikana baada ya watalii kutembelea hifadhi huwa inachangia katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wanaozunguka eneo la TANAPA.

  “Katika kipindi cha mwaka jana TANAPA ilichangia kiasi cha sh bilioni nne kwa wananchi na kila mwaka TANAPA hutenga bajeti ya asilimia saba katika michango ya jamii,” anasema.

  Moja ya hifadhi za taifa kati ya hizo 15 ni Hifadhi ya Ruaha, ambayo inapatika mkoani Iringa, yenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,300 na ni maarufu kwa wanyama aina ya kudu wakubwa na wadogo ambao hupatika huko.

  Ustawi wa Hifadhi ya Ruaha hutegemea kwa kiasi kikubwa Mto wa Ruaha, ambao ndiyo tegemeo kubwa kwa maji.

  Kuna aina mbalimbali za samaki, viboko, mamba na swala pala, ambao hunywa maji katika mto huo na hufanyiwa mawindo ya kudumu na wanyama wakali kama simba, chui, mbweha, fisi na mbwa mwitu.

  Sifa ya hifadhi hii ni kuwa na aina ya mimea karibu yote inayopatikana katika nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika.

  Lakini pia ina magofu yanayosadikiwa kuwa ni maskani ya watu wa kale katika Kijiji cha Isimila, ambacho kipo kilometa 120 kutoka Iringa.

  Magofu hayo ni miongoni mwa maeneo muhimu yenye historia ya kale barani Afrika.


  Amana,
  Watanzania hatuna utamaduni wa kupumzika au kwenda likizo kwa mapumziko, sababu kubwa ikiwa ni umasikini. Mnaposema eti Watanzania wawe ni wadau muhimu wa watalii mnashangaza kweli kweli. Hebu nielezeni mimi Mtanzania, mfanyikazi, mshahara wangu ni Shilingi Laki Mbili kwa mwezi, sina gari, na ninataka kuenda Lake Manyara, Serengeti National Park pamoja na familia yangu kutalii angalau kama siku tatu, hivi ni kiasi gani cha pesa natakiwa niwe nazo? Wote tunajua hoteli za kitalii ambazo ziko porini ni ghali sana, wewe na mimi itakuwa ni ndoto kwetu kukaa huko kwa vile bei ya chumba kimoja katika hoteli hizo ambazo karibu zote zinamilikiwa na watu wa nje ni kati ya Shilingi 200,000/- mpaka 500,000/- kwa chumba kwa siku. Bei hii tena ni ya chini, nasikia bei ya kukaa katika Camps au lodge za mahema (permanent tented lodges and camps) ni kati ya Shilingi 400,000/- na shilingi 2,500,000/- kwa siku kwa mtu moja. Ni Mtanzania yupi atakaeweza kukaa katika hoteli hizo, labda mafisadi! Wewe na mimi tunajuwa kwamba hapo awali mahoteli kama Lake Manyara Hotel, Ngorongoro Wildlife Lodge, Seronera Wildlife Lodge, Lobo Wildlife Lodge, Mafia Lodge zilikuwa zinaendeshwa na kumilikwa na Watanzania. Hoteli hizo zilikuwa ni za gharama nafuu sana kulinganisha na hoteli zingine za kigeni zilizokuwa kwenye hifadhi za taifa. Tangu hoteli hizo ziwe mikononi mwa mhindi mmoja ambae baada ya kuzinunua hoteli hizo miaka kadhaa iliopita (kama ni kweli alilipa pesa zote hizo) alipandisha bei ya kukaa kwenye hoteli hizo kwa zaidi ya asilima mia mbili bila kufanya matengenezo yeyote yale. Mahoteli hayo yalikuwa ni mategemeo makubwa sana kwa Watanzania kwa vile bei zake zilikuwa ni nafuu sana. Leo hii mnazungumzia Watanzania tuanze kutembelea mbuga zetu, jamani tutakaa wapi? kwenye makambi au nyumba za mabati za TANAPA?! Usafiri nao, si mmnajua gharama ya kukodisha gari na pesa zinazotozwa na Ngorongoro Conservation Area Authority kuingia ndani ya Crater? Unahitaji zaidi ya shilingi laki mbili kwa gari moja kuingia ndani ya Crater. Siyo wengi wanaoweza kumudu gharama hizi. Au mnatuambia sisi walalala hoi tukodishe mabasi ndipo gharama zitakuwa nafuu. Kumbukeni Watanzania tumeshafungua macho, tunataka pia kusafiri kwa raha zote kama hao watalii wa nje na tutahitaji kukaa kwenye magari ambayo yamejengwa kwa safari, yaani dirisha moja, kiti kimoja. Ushauri: Hizo hoteli nilizozitaja hapo juu ni urithi wetu, zirudishwe kwa Watanzania. TANAPA, tengenezeni barabara katika hifadhi, hasa kutoka Ngorongoro hadi Naabi gate, zinatisha, ukisafiri siku moja kwenye barabara hiyo hutataka kurudi kamwe Serengeti. TANAPA inapata pesa nyingi za kigeni, lakini utashangaa kuona hali za miundo mbinu zake. Acheni kupeleka wafanyakazi wa TANAPA wengi namna hiyo kwenye Maonyesho Ya Kitalii huko nchi za nje. Inasikitisha kusikia eti mhasibu au mkurugenzi wa bodi anakwenda kuhudhira maonyesho ili kuvutia watalii waje Tanzania kwa wingi! Hawa wanajua nini? Acheni ufisadi, ofisa mmoja anatosha kuiwakilisha TANAPA. Vile vile Ngorongoro mue na aibu, kazi kubebana kwenye maonyesho hayo ili mlipwe pesa (per diam). Hizo pesa sio zenu ni za Watanzia wote.
  paulimasao
   
 2. t

  tinkibiruka mhaya JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2016
  Joined: Jul 28, 2016
  Messages: 511
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 80
  Kwa sasa imeshafika shilingi ngapi kwa mtanzania kuweza kulipia gharama za kwenda ngorongoro
   
Loading...