Utakuwaje na wasiwasi kama wewe siyo mwingi!?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,039
Posted Date::12/1/2007
Siku ya Ukimwi: Rais Kikwete akiri kupatwa hofu baada ya kupima
* Asema hata Waziri wa Afya alikuwa na wasiwasi
* Aonya wanaoambukiza ukimwi kwa makusudi
* Mwakyusa ataka waliokimbia majibu wayachukue

Na Waandishi Wetu
Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete amesema alipatwa na hofu kubwa wakati anasubiri majibu baada ya kupima kama ana virusi vya ukimwi au la wakati akizindua kampeni ya upimaji wa hiari Julai 14 mwaka huu.

“Baada ya kupima na kuingia kwenye banda kusubiri majibu, nikawa najiuliza ikionekana nina virusi vya ukimwi itakuwaje?" alisema Kikwete.

“Hata Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa ambaye nilikuwa naye kwenye banda hilo akawa na wasiwasi sasa itakuwaje Rais akiwa na virusi vya Ukimwi, lakini nashukuru niko salama,” alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete ambaye alikuwa akihutubia jana katika kilele cha siku ya Ukimwi duniani kwenye†uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mkoani hapa alisema suala la kupima si tatizo, tatizo ni majibu kwani ni†jambo linalotia hofu.

Hofu kubwa inahusiana na kule kufikiria itakuwaje iwapo utapata matokeo yasiyokuwa mazuri.†Inahitaji moyo wa ujasiri kuamua kuwa tayari kupokea matokeo yoyote.†

“Lakini ni muhimu sana kupima na kujua hali ya afya yako, kwa sababu kama utakuwa una virusi utashauriwa jinsi ya kuishi na unaweza ukaishi miaka mingi zaidi, lakini kama huna utakuwa makini zaidi katika kuhakikisha huambukizwi,” alisema.

“Tulijiwekea lengo la kuwafikia watu milioni 4.1 ifikapo Novemba 30, 2007.† Taarifa ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, inaonyesha kuwa hadi Novemba 20, watu wapatao 2,508,382 walikuwa wamejitokeza kupima. Kiasi hicho ni zaidi ya asilimia 60 ya lengo,” alisema Kikwete.

Ingawa Rais alipongeza mafanikio hayo lakini baadhi ya wapimaji virusi wanalalamikia†malipo duni na yasiyokwenda na wakati, jambo ambalo Kikwete alilizungumzia suala hilo la kuahidi kupatikana kwa ufumbuzi.

“Naambiwa matatizo yahusuyo malipo ya posho kwa wapimaji yamechangia kupunguza kasi na ufanisi wa zoezi hili, lakini hizi ni changamoto tunazozifanyia kazi,” alisema.

Alisema awamu hiyo ya kwanza ya zoezi la upimaji hadi Novemba mwaka huu,†imekuwa ya mafanikio. Awamu ya pili inaanzia Novemba mpaka Julai 14, 2008, na baada ya hapo†serikali itaangalia matokeo na kufanya tathmini ya hali ya maambukizi ilivyo.

“Kapimeni ndugu zangu.†Matokeo ya kupima ni siri ya yule anayepima. Kwa maana hiyo hakuna sababu ya kuogopa kupima.

“Lakini kubwa zaidi ni kwamba wale watakaobainika kuwa wameambukizwa virusi vya Ukimwi watapata fursa ya kuhudumiwa ipasavyo na serikali.† Uwezo tunao toeni hofu kabisa. Pili, ninawaomba waliokwishapima wawe waangalifu.† Walio salama wasipate na wasio salama wasiambukize wenzao makusudi,” alionya.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete aliwataka waandishi wa habari kujitokeza na kupima afya zao kwa hiari ili kubaini kama wameambukizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU) au la.

Alisema waandishi wa habari nao wanapaswa kujitokeza na kupima afya zao kama kichocheo ya kampeni yake ya kupima ukimwi kwa hiari, aliyoizindua kwa yeye na mkewe, Salma, kupima Julai 14, mwaka huu.

“Kuna mwandishi mmoja aliniandikia ujumbe mfupi na kuniambia anaunga mkono kampeni yangu na kwamba alipima na kugundulika ameathirika, sasa ombi langu kwenu mkapime afya zenu,” alisema Rais Kikwete.

Pia Rais Kikwete alivipongeza vyombo vya habari kwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupima afya zao na alivitaka viendelee kuripoti habari zinazohusu kampeni hiyo.

“Vyombo vya habari vimekuwa vikijitahidi kuwahamasisha watu wajitokeze kupima kwa hiari, hivyo ombi langu, muendelee kuripoti kwani mahitaji bado ni makubwa,” alisema Rais Kikwete.

Vile vile Rais Kikwete alisema mwisho wa baadhi ya watu wanaowaambikiza wenzao ugonjwa huo kwa makusudi, umefika na kwamba sheria ya ukimwi inaandaliwa kwa lengo la kuwathibiti watu hao.

“Kuna magazeti yamekuwa yakiandika kuna kigogo ana fedha zake anaambukiza wanawake ukimwi, watu kama hawa tutawachukulia hatua kali ikiwemo kuweka mtego na hata ikilazimika kumpima ili†kujua ukweli, hatutaki kabisa tabia hii.”

Alionya kuwa tabia hii ya kuambukiza wengine ili mfe wote ni†chafu na inapaswa kuachwa mara moja, kwani dawa ya watu wenye tabia hiyo iko jikoni inamcheka.

Kuna sheria inaandaliwa juu ya wenye tabia kama hizo. Kikwete alisema “Nafurahi kuwaarifu kuwa tumekamilisha muswada wa Sheria ya Ukimwi. Muswaada huo umesomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Bunge kilichopita cha mwezi Novemba, 2007.

“Muswada huo unatarajiwa kusomwa tena, kujadiliwa na kupitishwa kuwa sheria katika Mkutano wa Bunge cha mwezi wa Februari, 2008. Sheria hiyo inalenga kulinda haki za wananchi na kusimamia upatikanaji wa huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.

“Chini ya sheria hii pia, hatua muafaka zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote atakayebainika kuambukiza watu wengine virusi vya Ukimwi kwa makusudi. Sheria itatoa jibu kwa malalamiko yaliyokuwepo dhidi ya watu hao,” alisema.

“ Kama ambavyo sote tunafahamu kumwambukiza mtu ukimwi kwa makusudi ni kitendo cha ukatili na unyama wa hali ya juu. Ni kitendo kisichokubalika kamwe ambacho lazima tutafute njia endelevu ya kupambana na uovu huo ili kuwalinda wananchi wasiokuwa na hatia,” alisisitiza Kikwete.

Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Professa David Mwakyusa, aliwataka watu waliopima VVU na kukimbia majibu waende kuyachukua.

Alisema katika kampeni hiyo, wanawake wamejitokeza zaidi kuliko wanaume na hivyo aliwataka wanaume wajitokeze zaidi ili kufikia malengo yaliyowekwa.

Alisema katika kampeni hiyo, Mkoa wa Lindi umeongoza kwa asilimia 115 na kufuatiwa na Kilimanjaro asilimia 99.6 ya watu waliojitokeza kupima.

Waziri huyo alisema Mkoa unaoongoza kwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo ni Iringa, Mbeya na Mwanza wakati mikoa yenye maambukizi kidogo ni Kigoma, Manyara na Kilimanjaro.

Alisema serikali imejiandaa vya kutosha katika kumpatia kila mwananchi mwenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi huduma† zote muhimu.† Huduma hizo ni pamoja na dawa za kupunguza makali ya ukimwi (ARVs).

Hadi sasa watu zaidi ya 220,000 wameorodheshwa kupata huduma ya dawa hizi na tayari watu 121,000 wanapata dawa hizo nchini kote.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Balozi wa Marekani nchini, Mark Green alizitaka jamii za kimataifa na wafadhili mbalimbali kuwa kitu kimoja katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Balozi Green pia aliwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kusaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo na kwamba ataendelea kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kupambana na VVU.

“Nimeona kwa vitendo juhudi za Rais Kikwete za kupambana na Ukimwi. Na Kikwete na mama Kikwete wamekuwa mfano katika kampeni ya kupima ukimwi kwa hiari,” alisema Balozi Green.

Naye Michael Uledi anaripoti kutoka Dodoma kuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Dodoma, Peter Mwamasika amesema kuwa matumizi ya kondomu hayawezi kuwa suluhisho kwa ajili ya kuzua maambukizo ya ukimwi kwa kuwa si moja ya tamaduni za kiafrika.

Askofu Mwamasika alisema kuwa pamoja na kutopenda kuingia katika migogoro na wanasiasa ambao wamekuwa wakihubiri sana juu ya matumizi ya kondomu lakini anadhani kuwa watu wengi wanapokuwa katika harakati za kutumia kondomu wamejikuta wazikivua, hivyo kuwataka viongozi wa dini

kuhakikisha wanahubiri upendo na uaminifu katika ndoa ili kuhakikisha Ukimwi unadhibitiwa.

Alisema kuwa pia ni muhimu kwa wasichana na wavulana kutambua kuwa kupata matiti na kuota ndevu si kigezo cha kuanza kujiingiza katika uzinzi na badala yake wajitunze hadi watakapooa ama kuolewa.

Alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anadhibiti shughuli zote za burudani ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika ongezeko la maambukizo ya ukimwi.

“Naomba rais awe serious kuzuia wanawake kucheza nusu uchi na kuonyesha mapaja na matiti yao…wakataze picha za kucheza nusu uchi, hata hapa mkoani Dodoma kuna maeneo yanayoshawishi watu kucheza wakiwa katika hali hiyo,” alisema Askofu Mwamasika.

Katika maadhimisho hayo mtoto mdogo mwenye umri wa mwezi mmoja aliyezaliwa na mama ambaye anaishi na virusi vya UKIMWI na ambaye amethibitika kuwa hana ugonjwa huo baada ya mzazi wake kufuata masharti aliyopewa kabla na baada ya kujifungua alikuwa kivutio kwa mamia ya watu waliokusanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu.

Wakati huo huo, Paulina David anaripoti kutoka Mwanza kuwa watu 14,848 kati ya 195,370 waliojitokeza kupima virusi vya ukimwi kwenye kampeni ya kitaifa ya kupima mkoani humo wamekutwa na virusi vya ukimwi.

Akizungumza mkoani hapa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk James Alex Msekela alisema kuwa hadi juzi watu hao sawa na asilimia 7.6 wamekutwa na virusi vya ukimwi.

Alisema kuwa watu hao wamejitokeza katika wilaya zote za mkoa wa Mwanza na kwamba takwimu za watu waliojitokeza kwa ajili ya kupima virusi vya ugonjwa huo ni sawa na asilimia 55 ya watu 368,000 waliokuwa wanatarajiwa kupimwa mkoani hapa.

Naye mke wa Rais Kikwete, Mama Salma, alisema kuwa Mkoa wa Mwanza uko juu kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi ukiwa katika nafasi sita kitaifa, hivyo akawataka wananchi kupiga vita maambukizo mapya na kujitokeza kupima.
 
Lazima wasiwasi umpate, anazijua nyendo zake, je majibu yangetoka Positive angetangaza?
 
Back
Top Bottom