UTAKAPO KUFA YATASEMWA MANENO GANI?!

UTAKAPO KUFA YATASEMWA MANENO GANI?!

bartaizo

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
236
Reaction score
91
Utakapokufa Yatasemwa Maneno Gani?
[emoji117] “Na kama vile watu wanavyo wekewa kufa mara moja, na baada ya kufa ni hukumu” Waebrania9:27[emoji117]Utakapokufa waumini wenzio watasema maneno gani juu yako? Je, watasema uliwapenda? Waebrania 13:1. Je, watasema ulikuwa mwaminifu katika mahudhurio? Waebrania 10:25. Je, watasema ulikuwa mkarimu na mnyenyekevu? Waef. 4:32. Je, watasema ulikuwa na roho ya kusamehe? Mathayo 6:14-15; 18:22. Je, Watasema ulimpenda jirani yako? Marko 12:32. Je, watasema kila wakati uliwasalimia kwa tabasamu? Waebrania 3:13. Je, watasema ulikuwa mpole na mnyenyekevu? Mithali 16:19. Waumini wenzio watasemaje utakapokufa? Siku ya msiba wako wa kuhudumu ibada, mhubiri atasema nini kuhusiana na wewe ? Je, atasema kila walipohitaji mtu kufundisha darasa, kupiga simu, kuwasaidia vijana, kutembelea wajane ulikuwa wa kwanza kunyoosha mkono wa kusaidia? Mathayo 23:11. Je, atasema kwamba kwa kadri ya uongozi wa kanisa, ulikuwa thabiti na wala hukuwahi kuleta matatizo au mashaka? 1 Wakorintho 15:58. Je, atasema imani yako ilikuwa madhubuti, upendo wako kwa Bwana ulikuwa katika kweli na kwamba kweli ulikuwa mwanafunzi wa neno? 1 Yohana 2:5. Je, atasema uliitamani nchi, mji aliouandaa Mungu? Waebrania 11:16. Hivi, kweli kwa ujasiri ataweza kusema kuwa mwili huu tunaulaza humu kaburini utafufuliwa hivi punde na kukutana na Bwana na watakatifu hewani na kuwa na Bwana milele? 1 Wathesalonike 4:17. Atasemaje? Mungu atasemaje siku ile? Siku ya Bwana itakapowadia, nawe utasimama mbele ya kiti cha enzi cha [emoji271]Kristo ili kutoa hesabu ya mambo uliyoyatenda katika siku za uhai wako ikiwa yalikuwa mema au mabaya, 2 Wakorintho 5:10, Bwana atasemaje? Je, atasema, “vema mtumwa mwema na mwaminifu…ingia katika furaha ya Bwana wako? Mathayo 25:21. Je, atasema “nitakupa taji ya uzima? Ufunuo 2:10. Je, atakuhakikishia nafasi katika enzi yake? Ufunuo 2:21. i Jamani, najua kadri tukuavyo ndivyo tunavyoelekea kwenye umauti. Lakini, utakapokuwa tayari umo katika umauti ungependa wale waliokufahamu na kukupenda hapa duniani wasemeje ? Unataka Bwana asemeje siku hiyo? Endapo unataka haya maneno mazuri naya uaminifu yaje yasemwe juu yako nyakati hizo, na tuyakumbuke maneno ya Paulo katika 1 Wathesalonike. 3:12 “Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu. Apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wote.”
[emoji534][emoji271][emoji271][emoji271][emoji271][emoji519]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom