Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Niliwahi kulizungumza swala hili kule Facebook mwaka 2014, Leo naomba kulirudia tena. Ukisoma biblia vizuri utajua mengi kuhusu haya, ikumbukwe kuwa Biblia imekaa kiutawala zaidi.
DETENTION au VIZUIZINI ni ile hali ya kugeuzwa kuwa MTU usiyejitambua na kukufanya usifikie hatma yako.
Utajuaje uko vizuizini sasa:-
1. Unaweza kuwekewa mapingamizi katika majukumu yako ya msingi ili usifanikiwe katika utawala. Mfano unapelekwa Exile nje ya Nchi yako au unabaki kwenye nchi yako ila unawekwa exile kwenye kijiji chenu uliko zaliwa au kulia au kwenye asili yako na huruhusiwi kutoka nje ya eneo hilo au MKOA huo. Lengo hilo ni woga au wivu wa kiuongozi ambapo unaweza kuwa mhusika una karama ya uongozi kuliko watawala wote au Viongozi Fulani na wakawa na hofu na wewe kuwa Siku moja utakuwa kiongozi Fulani hivyo watakusingizia chochote ili wakuweke kizuizini kama njia ya kukuzima. n.k
2. Kutengwa na wenzio, hapa mhusika unapotaka kufanya ushirikiano na wenzako wao wanakupuuza lakini wanajua fika au una karama au kipaji na wanafanya hivyo ili watumie akili yako vizuri. Hapa ukifika kwenye kundi la watu, utashangaa watu wanaondoka mmoja mmoja na unabaki peke yako au na watu kadhaa, unaweza kufikiri wako busy kumbe wamekuweka vizuizini, kila unapotaka kujumuika na wenzio unashangaa wamejitenga, unaweza kufikiri umelaaniwa kumbe ni mbinu tu ya kukufedhehesha.
3. Zuio la Wateja: unaweza kuwa ni mfanyabiashara hapa kinachofanyika kila mteja anapofika ofisini kwako au dukani akitoka tu kuna watu wameshaandaliwa kila mteja akija anapewa somo la kutokuja tena kwako. Unashangaa Wateja wanakata gafla unabadilisha eneo lakini tena hali inaendelea vilevile, kama hujui unaweza kwenda kutafta dawa kwa waganga kumbe wenzio wanakuchezea tu. Mpaka ukastuke umemalizwa na kuharibiwa mambo mengi sana.
4. Propaganda na Uongo: hiki ni kizuizi ambapo watu wanakuwa wamejipanga kuongea uongo na kutoa taarifa za uongo kuhusu wewe(upotoshaji). Unashangaa kama vile una roho ya kukataliwa kumbe wenzako wanapandikiza chuki kila eneo unalopita. Mpaka uje ukashituke umekwisha umia sana. Hii detention hutumika kuharibu sifa kwa MTU mhimu.
5. Wachawi: hapa wachawi hutumwa kukushikilia kila eneo ili usienende mbele. Kila unapokuwa wao wameshaandaa maajenti na hutajua kabisa mpaka uje ugundue umeumia sana. Mara nyingi mbinu hii huitwa JESHI, utasikia Fulani tumeshamuwekea Jeshi, hapo jua wachawi wanamzunguuka kila kona. (Pigana vita hii kiroho)
6. Kufedheheshwa: hapa unakuwa unapewa tuhuma zisizo zako, kila jambo baya unazushiwa wewe uonekane mbaya mpaka ukashituke umeumia sana.
7. Njia nyingine ni kuku Stress au kuku Frustrate ili uchanganyikiwe ña kuamua kujiua. Mpaka ujue hilo unahitaji kuwa makini sana.
8. Kukuvurugua familia na ndoa, maana wanaamini ukiwa peke yako itakuwa rahisi kukuangamiza
9. Kukufungulia mashtaka ambayo yatakupeleka gerezani au kukusumbua sumbua kila mara, mara uitwe polisi mara uitwe na wakubwa fulani yaani kama kukutisha fulani hivi ili ubabaike na wafanikiwe kuharibu malengo yako.
10. Kama ni mwajiriwa basi utapewa majukumu mengi sana iliyakushinde na usahau malengo yako. Kuwa makini sana na zijue sheria za kazi ili usianguke.
11. Mwanamke anaweza kutumika kiurahisi kufanya unyama huu.Maana hutumika hasa kipindi ambapo wanahitaji mawazo ya mhusika(aliye detention). Ndio maana kiongozi mmoja afrika alipotoka gerezani alimkataa mkewe na kuoa mwingine.
12. Mbinu zote zikishindikana MTU huwekea ulinzi wa Polisi au Mjeda kumlinda ili asije kuinuka tena.
Yote haya hufanyika kwa kutaka kuwazima watu Wema ili waonekane hawafai, au kuzima watu kudai haki za msingi au kumzima kiongozi sahihi ili asipate nafasi. N.k
Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa ACA tarajiwa.