Utajiri wa Ridhwani wamweka pabaya Kikwete

Status
Not open for further replies.
Anapaswa kujua kuwa juhudi alizokuwa anafanya za kubadilisha baadhi ya majina yake kwenye kumjiliki Ginneries mbalimbali sio siri , zitawasilishwa nyaraka atapata aibu sana huyu kijana mwenzangu.
dU...Kumbe hadi kwenye ginneries ameshajimegea utajiri!!
Ndio maana alikuwa anaongea huku ana wasiwasi!...aibu itampata very soon huyu mtoto!
 
sasa anatia wasiwasi wa pili nje ya ufisadi
kapataje hivyo vyeti vya sheria?
maana utetezi wake huko ovyo kabisa , hiyo shamba alipataje na hizo account kaonyesha BANK STATEMENT zake au ni maneno ya mdogo tu bila mshiko
lakini hakumbuke pia tunajua maisha yake anayoishi na magari anayosukuma, siku kusema una pesa wakati unatanua na BWM ya bei mbaya,
yeye aseme alitoa wapi hizo pesa, je ni kwa mababu huko NIGERIA?
au kuna biashara gani alifanya?
kama ni zile za EPA haturudishie sisi tutaongea MKUU WA KAYA ?
hii familia inaweza kuwa balaa kuliko ya MKAPA na MWINYI kwa waliyofanya ikulu
 

sasa ushahidi siunao wa unayoyapinga? mi nadhani kama unabisha kisomi wewe na akina slaa mdhihirishe huo ushahidi aliouomba. Unajua kaka mtu kuongea unaweza kuongea sana lakini inapofikia kwenye point ya ushahidi basi toa ushahidi wako ulionao kisha sisi watanzania tutapima nani muongo na anaongopa kwa maslahi ya nani
 
Fungeni safari kwenda Morogoro. Kabla ya kufika Morogoro baada ya mashamba ya katani ya Kingorwila, Mkono wa kushoto kwako kama unatoka DSM kabla ya kimji kiitwacho Kingorwila, kuna eneo la wazi liliokuwa linamilikiwa na kampuni ya tumbaku, DIMON. Kuna miti imepandwa . Taarifa zinaonyesha tayari eneo hili liko chini ya miliki ya mtoto huyu. Ndo hiyo anayoita eka 1.5?

Ukifika Moro mjini Kuna mduara (Keep left) inayogawanya barabara ziendazo Dodoma, Iringa na mjini morogoro. Kuna eneo liliokuwa wazi na likiwa limezuiliwa kujengwa chochote. Kuna kituo cha mafuta cha mtoto huyu. Wakati kikijengwa kiliwekewa X sign baadaye ilifutwa mara moja na ujenzi ukaendelea.

Lipo Gorofa moja karibu na stendi ya morogoro linajengwa kama hoteli iitwayo Gwami. kumbe ni mali ya mtoto huyu. linafanana na lingine lijengwalo hapo Bagamoyo na pale Kibaha.

Hapa Dar nasikia Open space zimevamiwa na fuel stations za mtoto huyu kipenzi!

Hilo gamba ni zito! litavuka kweli?
 
dU...Kumbe hadi kwenye ginneries ameshajimegea utajiri!!
Ndio maana alikuwa anaongea huku ana wasiwasi!...aibu itampata very soon huyu mtoto!

Ana 50% ya shea za Ginnery moja iko malampaka .
Nyingine iko misungwi , sasa atawasilishiwa ushahidi na hata ile nyumba pale Mikocheni atapata majibu yake.

Vipi kuhusu Tanga Beach Resort? iliyopo Tanga.
 

Umenikumbusha masomo yake UK. Hivi aliishia wapi? Au vyuo vya huko hawakujua kwamba ni mtoto wa Rais
 
Like father like son, wote ni mafisadi tu!! Kama ni u-billionare sikaupatia ikulu? Hiyo ikithibitika inatosha kabisa kwa Jakaya Mrisho Kikwete kujiudhulu kwa matumizi mabaya ya ikulu. Gamba hapa ni Kikwete mwenyewe sio mtoto wake!!
 

alichoomba ni ushahidi na sio polojo zako hizo ambazo ni hisia. mie mpaka sasa sijajua nani mkweli, yeye kajitokeza na Slaa pamoja na mtikila aliowataja. kaka kwani wewe una akaunti moja? haya tuambie akaunti zako zina balance gani? ivi kaka dhambi ya kumtuhumu mtu unaitambua? maana siamini kama eti kuna dini ambayo haifundishi haya.
 

Huoni watakiwa utoe vivid evidence ili tupate kuchekecha ukweli wa mambo?
naweza sema Riz1 anamiliki hoteli ya kisasa serengeti ili kunogesha habari na kupoteza muda na wajinga watashabikia.
plz hebu tusiaibishe jukwaa hili kwa kuandika chochote ujisikiacho wakati huwezi thibitisha.
 
Jibuni ishu za mashamba kule juu, ambazo mmesema ni 1.5 hectars!...Mbona mnakimbilia hadithi zaidi kuliko kujibu tuhuma za mahoteli na beaches mlizojimegea?
 
Huyu mtoto amesoma sheria gani? Ni nani anayetakiwa kutoa ushahidi wa mali anazomiliki yeye. Mi nadhani yeye ndiye shahidi no 1 wa mali anazomiliki na doc zote anazo yeye. Sasa nani atoe ushahidi tena ndani ya wk 1. Huyo mtu akauchukue kwake? Au mimi ndio sijaelewa? Kama ametaja mali alizonazo, si atoe na ushahidi?
 

Yaani tujenge mashitaka hapa!
Unanikumbusha mashitaka ya 'Dr' Kamala kwa Msemakweli. Aliomba ushahidi na kudai heshima yake, baada ya siku chache akajisajili kusoma PhD.
 
Like father like son, wote ni mafisadi tu!! Kama ni u-billionare sikaupatia ikulu? Hiyo ikithibitika inatosha kabisa kwa Jakaya Mrisho Kikwete kujiudhulu kwa matumizi mabaya ya ikulu. Gamba hapa ni Kikwete mwenyewe sio mtoto wake!!

wewe unaweza kusema utakavyo lakini unavyoombwa ushahidi utoe,mara kadhaa slaa anapewa taarifa za uongo na watu yeye anaowaamini kuwa wanamsaidia kumbe.
 
Eti anasema anamiliki gari moja tu, aina ya Toyota Camry!...Ha ha haaa!
 
Nimemuona sasa hivi ITV anasema anawapa siku 7 wanaomtuhumu kuwa ana mali zaidi, watoe ushahidi, au sio atawafungulia mashtaka.
 
Jibuni ishu za mashamba kule juu, ambazo mmesema ni 1.5 hectars!...Mbona mnakimbilia hadithi zaidi kuliko kujibu tuhuma za mahoteli na beaches mlizojimegea?

kumbe huna hoja. Ridhiwani kaomba ushahidi wa tuhuma, sasa wewe kama unaendelea kumtuhum bila kutoa data nitakuona chizi. Toa data zako ili tujue kati ya Ridhiwan na wewe nani mlopokaji. hilo shamba ni sehemu ya tuhuma sasa toa ushahidi kuwa anamiliki zaidi ya hivo alivosema
 
Mashamba, anamiliki shamba kubwa kule Burka Estate Arusha, kama mnakumbuka hata gazeti la raia mwema liliwahi kuiweka listi ya wenye maeneo waliokuwa wametangazwa na Halimashauri na yeye yumo pamopja na wakina Kimei wa CRDB.
 

Mashamba, anamiliki shamba kubwa kule Burka Estate Arusha, kama mnakumbuka hata gazeti la raia mwema liliwahi kuiweka listi ya wenye maeneo waliokuwa wametangazwa na Halimashauri na yeye yumo pamopja na wakina Kimei wa CRDB.
Kama kusikia husikii, hata picha huoni?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…