Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 9,576
- 14,312
Pamoja na utajiri wote huo, Elon Musk kakataliwa na mwanaye aliyekuwa mvulana na sasa ni mwanamke:-
Kushoto, akiitwa Xavier Alexander Musk, kulia ni muonekano wake wa sasa akiitwa Vivian Jenna Wilson.
Mtoto wa Elon Musk aliyemkataa baba yake alizaliwa kama mwanaume akaitwa Xavier Alexander Musk. Baada ya kufikisha umri wa miaka 18, alibadili jinsia na kuwa mwanamke, akachukua jina la Vivian Jenna Wilson—akitumia ubini wa mama yake, Justine Wilson.
Ili kuhakikisha Elon hamsogelei, Vivian aliwasilisha ombi rasmi mahakamani la kubadili jina na jinsia yake, akitamka wazi kuwa hataki uhusiano wowote au udugu na baba yake wa kibaolojia. Vivian amekataa kabisa utajiri na ukwasi wa Elon Musk, akichagua kuishi maisha huru mbali na fedha hizo.
Kwa sasa, Vivian anaishi maisha ya faragha kama mwanafunzi wa chuo na hajaolewa. Mama yake, Justine, anaunga mkono uamuzi wa mwanae kwa asilimia mia moja na ameeleza kujivunia msimamo wake. Kwa upande wake, Elon Musk ameshtushwa na hatua hiyo, akidai kuwa mwanae "ameuawa na itikadi kali za kisasa" (woke mind virus) na kwamba amempoteza kabisa.