Utajiri wa kishirikina unavyotesa wengi

Ukianza kujihusisha na waganga wa kienyeji ujue hutoacha kuwategemea.... hutojitambua kuwa umefikia hatua mbaya......kibaya zaidi tunaingiza familia zetu matatani sasa au hata baadae kutokana na maagano yako kwa waganga kwa kujua au kutojua.

Utajiri au ulinzi wa kiganga mwisho wake ni mbaya na majuto shetani akiwa ameshahakikisha kakumaliza ndio akili zitakurudia na kuanza kuhaha kwa wachungaji kusubiri huruma ya Mungu ambayo anaitoa kwa mapenzi yake.
Tuwe makini na tupigane na maisha tukimtegemea Mungu pekee. Tuache tamaa zilizopitiliza hadi kugeuka kuwa chukizo kwa muumba wetu.
 
Duh,pori likivamiwa nawewe unahama mh,sasa mshana ile madayetu mbona haikuendelea(kunawatu hufa malambili))

Twende kule dagii naendelea mdogo mdogo
 
Last edited by a moderator:
Inawahusu hasa wale wenzetu wa kutoka wilaya ya Makete. Yaani Wakinga. Full mazingaombwe

Ila wangetoka kaskazini ndo matajiri halali wakitoka kusini sio halali toa evidence ya uchawi kwa Wakinga
 
Kaka usisahau maofisini- tulia angalia mienendo ya watumishi walio wengi yaani ni ushirikina tupu tupu
 
Haswaaa lakini umeniacha na kiu ya kuendelea kufuatilia maelezo, umekatisha mada kwa mtazamo wangu.
 
Haswaaa lakini umeniacha na kiu ya kuendelea kufuatilia maelezo, umekatisha mada kwa mtazamo wangu.

Naelewa ila usijali nitajazia palipopelea ushirikina kwenye maisha yetu upo kila kona na watu wanauabudu sana wengine kwa kificho na wengine waziwazi kabisa
 
Kaka usisahau maofisini- tulia angalia mienendo ya watumishi walio wengi yaani ni ushirikina tupu tupu
Kiyoya hii kitu ni kila mahali mpaka kwenye ndoa na mahusiano hata kwenye dini zetu huwezi amini watu wanaroga sana tu,ila niliamua kuanza na kipengele kimoja kwanza cha utajiri .nitakuja na kingine cha dini ambacho najua nitapata upinzani mkubwa sana
 
Last edited by a moderator:

Aaaah bwana wewe acha ibishi bwana, wakinga wengi walipata utajiri kwa njia za majoka.... unajua nini kuhusu mwakipande
 
Mkuu nimeanza kuelewa kuna kitu unacho ila unakitoa taratiibu, bado naikumbuka ile mada yako ya juzi ya milango ya kuzimu ...anyway, i like it.
 
Utajiri una madaraja na kila daraja lina kafara lake mfano
Milioni 20-50 ni tofauti na milioni 100-200 na kila daraja huhitaji kitu kikubwa zaidi au damu nyingi zaidi

Mkuu mshana nielekeze niende huko nikaukwae huo utajiri
 

Hapo unapo yaandika haya una bonge la hirizi kwenye walleti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…