Pastor Silla
Senior Member
- Sep 22, 2020
- 162
- 166
Nyakati za Sasa dunia pamoja na nchi yetu ya Tanzania imekumbwa na roho chafu ya kutafuta au kupenda mali au utajiri wa kichawi na kishirikina.
Watu waliowengi wapo tayari kuua au kumiliki majini na kutia kafara mbalimbali za damu kwa Shetani ilimradi wapate pesa ,mali na utajiri.
Wapo ambao wanashirikina tendo na Mama zao wazazi,wapo waliowafanya watoto wao mazombi na wapo wengine wanaingiliwa kinyume na maumbile na wapo ambao hawazai au jogoo hapandi mtungi na hana mtoto;wengine wamefunga mizukule kwenye vyumba maalum kwenye nyumba zao.
Ukifanya tafiti utakuta mara nyingi utajiri wowote unaopatikana kutoka kwa Shetani uwa una majuto mengi Sana na uwa haudumu kama utajiri utokao kwa Mungu;pia matajiri hao wakifilisika ushia kuwa masikini wa kutupa .
Neno la Mungu linasema utajiri na heshima upo kwa Bwana.Pia kwenye Mithali inasema "Baraka za Mungu hazina huzuni ndani yake" tofauti na za Shetani zimejaa huzuni nyingi ndani yake ikiwemo kuteseka kwa kafara,kutokwa vidonda ndugu,kujamiana na Mama mzazi ,kutolala usiku na kuua mke au mtoto wako umpendae.
Zingatia;Kataa kuvutwa na utajiri wa kipepo au kishetani utakutesa Sana.Yupo Yesu kwa ajili yako ukimwamini atakusaidia mqamini na fanya kazi kwa bidii utafanikiwa.Hacha tamaa maana tamaa ilisababisha fisi kukosa vyote maana utajiri wa kishetani ukukosesha furaha na amani pia utaishia Jehanamu.
Mithali 3:5-6 inasema vyema Sana kwamba"Mtumaini Bwana kwa kila Jambo Wala usitegemee akili yako peke yako na katika njia zako mkiri yeye naye atanyoosha mapito yako.Kumbuka utajiri na heshima vipo kwa Bwana na si kwa Shetani.
KATAA UTAJIRI WA KICHAWI NA KISHIRIKINA.JENGA MAHUSIANO NA MUNGU NA FANYA KAZI KWA BIDII.
Pastor Silla.