Tape measure
JF-Expert Member
- Nov 26, 2015
- 1,989
- 3,692
Kwa wale wajuvi wa uchumi wanaweza kudadavua kiundani tofauti ya Biashara na uwekezaji.
Nisikupotezee muda kwa kuanza kuongelea Historia ya Sangara katika ziwa Victoria ama idadi ya samaki katika ziwa.
Miongoni mwa biashara zenye faida kubwa na ya haraka ni biashara ya samaki hasa aina ya Sangara -Nile perch
Biashara hii ya samaki ni kama ilivyo ya madini imegawanika katika makundi mbalimbali na kila kundi lina namna yake ya kuweza kujipatia faida.
Kwanza unaweza kuwa mmiliki wa mtumbwi/boat. Ama ukawa mvuvi ama mlanguzi wa samaki wa jumla au kupeleka samaki sokoni. Pia unaweza kufanya bishara ya mabondo ambayo ndio pesa ilipo katika biashara hii ya sangara.
Tofauti na bishara zingine biashara ya samaki haina kanuni maalumu.ya kufuata kusudi utengenze faida huwa inafanyika kulingana na mtu na uzoefu wa kazi na aina ya wategajii/wavuvi wako mfano ukiwa na boati unawapa wategaji vitendea kazi wanaenda kuvua samaki kisha wanakuuzia wewe mmiliki kwa kg kulingana na bei ya mda husika kisha wew unawauza hao samaki kwa bei ya juu zaidi kwa walanguzi ama unapeleka kiwandani unatoa mabondo kisha unauza mnofu kwa kg.....au mlanguzi anapeleka samaki sokoni kisha anauzia wauza samaki na wao wanauza kwa walaji wa mwisho na kila mtu anakuwa kapata faida HII CHAIN NDIO CHANZO CHA KUPANDA BEI YA SANGARA
Katika hii biashara faida ni kubwa sana na pia hasara ni kubwa TAMBUA kila mtu aliye kwenye hii biashara anapata changamoto tofauti na mwenzie mfano mwenye boat atapambana na wavuvi mambo ya kwenda saloon/kuiba mzigo nk dalali nae atapata changamoto tofauti na muuzaji wa mwisho hivyo taarifa sahihi ndio mwanzo wa kufanikiwa.
TOFAUTI unaweza kununua 50kg za samaki ukaenda kuuza ukapata loss lakini mwenzio alienunua kilo sawa na bei sawa na wewe akaenda kuuza na kupata supper profit hapo ndio utachanganyikiwa inakuaje ?? Same applies kwa walanguzi wana mbinu mbali mbali ikiwemo kuchezea mzan kidogo na mambo ya asili asili ndio maana nikatanguliza hii biashara ukifanya usipofanikiwa usiseme hailipi sema mimi haikunilipa.
UWEKEZAJI
Uwekezaji unaanza pale unapokuwa umekamilisha kutengeneza boat zako na kununua vifaa vyote vya uvuvi wategaji wanakwenda day one unapata loss kidogo next day wanarudi na loss kiasi Mara ya tatu unapata profit ya 300k unasema sasa mambo yanaanza kujipa unanunua, na kuongeza vifaa kama ndoano zilizopotea katika awamu 2 za nyuma kusudi upate zaidi kweli unapata faida 500k siku inayofuata mnaibiwa mgonzo ama wategaji wanarudi na loss na bila vitendea kazi kama nyamvu na ndoano hapo tambua wategaji wanasuburi uwawezeshe vinginevyo kazi ndio inakua imekwisha
Hapa unakuwa ni mwendo wa kuongeza mtaji kila mara unaweza anza na 2m baada ya mwezi unakuta ushatumia 4m hapo ndio game inaanza kukolea inakubidi ukomae zaidi kusudi urudishe pesa yako na ukifika stage hiyo ndio uko likely kufanikiwa...kama nilivosema mwanzo unaweza usifikie stage hiyo na ukawa tayari umefanikiwa kumudu biashara.
Kinachosumbua zaidi kwenye biashara ya samaki na madini ni uzoefu mtu anaweza kuwa na kila kitu na biashara ikakushinda wakati mwenzio mwenye maarifa na uzoefu yeye akiwa na robo ya mtaji wako anaendesha biashara bila shida.
Niseme tu hii biashara ina vitu vingi na vingine ata kama umewahi kuifanya kwa miaka kadhaa bado kuna mambo kibao unaweza usiyafahamu cha muhimu uwe unapata faida kwani mambo na utaratibu unatofautiana mwalo na mwalo
Nimeeleza kwa uchache kuhusu sangara sijataka kuchanganya mambo ya marine fish, na wale wa mapambo ambayo inafanywa na wadau weng wenye kampun Dar hizo nazo changamoto zao ni nyingi haswa kuanzia kodi, usafiri na bei ya ushindani sokoni .....USICHEKE unapeleka mzigo then unasubiri uliompelekea ndio akuambie live fish walikuwa wangapi na dead crab ni wangap? Ni biashara kichaa zenye pesa ndefu ila ukiingia bila taarifa sahihi unapotea kama babu wa Loliondo.
BONDO la sangara /Swim bladder/fish maws/Chinese delicacy
Bondo ndio lililobeba thamani katika sangara na ukubwa wa bondo unategemea samaki kama ni wa kwenye kina kirefu ama kifupi pia mara nyingine sio uhakika
Mabondo yamegawanyika katika sizes mbalimbali pia ni tofauti nchi na nchi hapa naongelea Kenya na Uganda
Kuna chips , small, Smaller , medium na large
Bondo huuzwa kwa grams chini ya gram 7 halinunuliwi kwani litakua limetoka kwa undersize/degere
KWANINI BONDO LINATHAMANI KUBWA HIVYO
kwa uchache bondo hutumika kutengeneza vifaa vya magari kama buggat, ndege, lens za miwani, phamacetical industries, hutibu magonjwa kibao ikiwemo uhanisi, kutoshika mimba....bondo la sangara ni dawa/pesa hahaa unakula tu kama mboga n.k
1kg ya bondo kwa China inafika karibu 6m kutegemea na seasons mabondo yanathamani zaidi Uganda so sio lazima ufikirie kupeleka China mambo ya kupata vibali ya exports as individuals ni ngumu unless uwe agents wa brokages mostly from China mfano ukiwa na bondo la samaki wa 8kg linaweza range 245gram Tanzania walanguzi watakupa 74k Uganda unaweza pata 110k Wakati China unaweza pata 320k
Mara ingine samaki anaweza kuwa mkubwa lakini bondo likawa jepesi na akawa mdogo likawa zito.
Wewe unataka kuwekeza wapi??Jipime unaweza kumudu changamoto zipi na ngapi? Everything is easy when you spent time practicing.