Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 3,910
- 6,704
Maneno ya Mungu yanasema hivi: Ni rahisi kwa ngamia (sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu.
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji.
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyoofu, huruma, utu, wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara, dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho.
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana alafu uuze kwa faida kubwa.
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako.
Itabidi ununue hata kuuza mali za wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi.
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi.
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako.
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendeleza kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako.
Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.
Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamii, lakini kile unachotoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa msaada.
Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya matamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.
Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja.
Sent using Jamii Forums mobile app